Salamu
11:1 Rum 1:1; Efe 1:1; 2Kor 1:1; 2Tim 1:1; Mdo 18:17Paulo, niliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Kristo Yesu, na Sosthene ndugu yetu.
21:2 1Kor 10:32; Mdo 2:21; 18:1; Rum 1:17Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale waliotakaswa katika Kristo Yesu na walioitwa kuwa watakatifu, pamoja na wale wote ambao kila mahali wanaliitia Jina la Kristo Yesu Bwana wetu, aliye Bwana wao na wetu pia:
31:3 Rum 1:7; 1Kor 1:2; Efe 1:2; 1Pet 1:2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.
Shukrani
41:4 Rum 1:8Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu. 51:5 2Kor 8:7; 1Kor 12:8; 2Kor 9:11Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kusema kwenu na katika maarifa yenu yote, 61:6 2The 1:10; 1Tim 2:6; Ufu 1:2kwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Kristo ulithibitishwa ndani yenu. 71:7 Rum 1:11; 1Kor 12:1-3; Mt 16:27; Lk 17:30; Ufu 1:7; 1The 1:10; 2:19; Tit 2:13; Yak 5:7-8; 1Pet 1:13; 2Pet 3:12Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 81:8 1The 3:13; 5:2; Amo 5:18; 1Kor 5:5; Flp 1:6; 2:16Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 91:9 Rum 8:28; 1Yn 1:3; Isa 49:7; Kum 7:9; 1Kor 10:13; 1The 3:3; 1Tim 2:13; Ebr 10:23; 11:11Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Yesu Kristo, Bwana wetu ni mwaminifu.
Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa
101:10 Rum 7:1; 15:5; 1Kor 11:18Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. 111:11 Mdo 11:14Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu. 121:12 1Kor 3:4-22; Mdo 18:24; Yn 1:42; 1Kor 3:22; 9:5Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo”; mwingine, “Mimi ni wa Apolo”; mwingine, “Mimi ni wa Kefa,”1:12 Yaani Petro. na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”
13Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye alisulubishwa kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa kwa jina la Paulo? 141:14 Mdo 18:8; 19:29; Rum 16:23Nashukuru kwamba sikumbatiza mtu yeyote isipokuwa Krispo na Gayo. 15Kwa hiyo hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kwamba alibatizwa kwa jina langu. 161:16 Mdo 11:14; 1Kor 16:15(Naam, niliwabatiza pia watu wa nyumbani mwa Stefana. Lakini zaidi ya hao sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.) 171:17 Yn 4:2; Mdo 2:38; 1Kor 2:1-13Kwa maana Kristo hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili; sio kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili msalaba wa Kristo usije ukakosa nguvu yake.
Kristo Ni Hekima Na Nguvu Ya Mungu
181:18 1Kor 2:14; 2Kor 2:15; 4:3; 2The 2:10; Mdo 2:47; Rum 1:16Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 191:19 Isa 29:14; Ay 5:12, 13; Yer 8:9Kwa maana imeandikwa:
“Nitaiharibu hekima ya wenye hekima,
na kubatilisha akili ya wenye akili.”
201:20 Isa 19:11-12; 1Kor 2:6-8; 3:18; 2Kor 4:4; Gal 1:4; Ay 12:17; Isa 44:25; Yer 8:9; Rum 1:22; 1Kor 3:18-19Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? 211:21 1Kor 6:2; 11:32; Rum 11:14; 3:22Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. 221:22 Mt 12:38; Yn 2:11; 4:48Wayahudi wanadai ishara za miujiza na Wayunani wanatafuta hekima. 231:23 1Kor 2:2; Gal 3:1; Lk 2:34Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi. 241:24 Rum 8:28; 1:16; Kol 2:3Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, Wayahudi na pia Wayunani, Kristo ndiye nguvu ya Mungu na pia hekima ya Mungu. 251:25 2Kor 13:4; 1Kor 1:18Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.
261:26 Rum 8:28; 1Kor 1:20; Yn 7:48Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. 271:27 Yak 2:5; Rum 1:22; 1Kor 3:18-19Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu. 281:28 Rum 4:17; 1Kor 2:6Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, 291:29 Efe 2:9ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. 301:30 Rum 16:3; Yer 5:5-6; 33:16; 2Kor 5:21; Flp 3:9; 1Kor 1:2; Rum 3:24Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi. 311:31 Yer 9:23; Za 34:2; 44:8; 2Kor 10:17Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”