1 Wakorintho 1:1-17 NEN

1 Wakorintho 1:1-17

Salamu

1:1 Rum 1:1; Efe 1:1; 2Kor 1:1; 2Tim 1:1; Mdo 18:17Paulo, niliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Kristo Yesu, na Sosthene ndugu yetu.

1:2 1Kor 10:32; Mdo 2:21; 18:1; Rum 1:17Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale waliotakaswa katika Kristo Yesu na walioitwa kuwa watakatifu, pamoja na wale wote ambao kila mahali wanaliitia Jina la Kristo Yesu Bwana wetu, aliye Bwana wao na wetu pia:

1:3 Rum 1:7; 1Kor 1:2; Efe 1:2; 1Pet 1:2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.

Shukrani

1:4 Rum 1:8Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu. 1:5 2Kor 8:7; 1Kor 12:8; 2Kor 9:11Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kusema kwenu na katika maarifa yenu yote, 1:6 2The 1:10; 1Tim 2:6; Ufu 1:2kwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Kristo ulithibitishwa ndani yenu. 1:7 Rum 1:11; 1Kor 12:1-3; Mt 16:27; Lk 17:30; Ufu 1:7; 1The 1:10; 2:19; Tit 2:13; Yak 5:7-8; 1Pet 1:13; 2Pet 3:12Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 1:8 1The 3:13; 5:2; Amo 5:18; 1Kor 5:5; Flp 1:6; 2:16Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 1:9 Rum 8:28; 1Yn 1:3; Isa 49:7; Kum 7:9; 1Kor 10:13; 1The 3:3; 1Tim 2:13; Ebr 10:23; 11:11Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Yesu Kristo, Bwana wetu ni mwaminifu.

Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa

1:10 Rum 7:1; 15:5; 1Kor 11:18Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. 1:11 Mdo 11:14Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu. 1:12 1Kor 3:4-22; Mdo 18:24; Yn 1:42; 1Kor 3:22; 9:5Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo”; mwingine, “Mimi ni wa Apolo”; mwingine, “Mimi ni wa Kefa,”1:12 Yaani Petro. na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”

Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye alisulubishwa kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa kwa jina la Paulo? 1:14 Mdo 18:8; 19:29; Rum 16:23Nashukuru kwamba sikumbatiza mtu yeyote isipokuwa Krispo na Gayo. Kwa hiyo hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kwamba alibatizwa kwa jina langu. 1:16 Mdo 11:14; 1Kor 16:15(Naam, niliwabatiza pia watu wa nyumbani mwa Stefana. Lakini zaidi ya hao sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.) 1:17 Yn 4:2; Mdo 2:38; 1Kor 2:1-13Kwa maana Kristo hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili; sio kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili msalaba wa Kristo usije ukakosa nguvu yake.

Read More of 1 Wakorintho 1