Isaya 43:18-21
43:18 Isa 41:22“Msiyakumbuke mambo yaliyopita,
wala msiyatafakari mambo ya zamani.
43:19 Hes 20:11; Yer 23:8-9; Ufu 21:5; Isa 40:3; 41:22; Yer 16:14-15; 2Kor 5:17; Isa 35:7Tazama, nitafanya jambo jipya!
Sasa litachipuka, je, hamtalitambua?
Nitafanya njia jangwani
na vijito vya maji katika nchi kame.
43:20 Hes 20:8; Isa 48:21; 41:17; Za 148:10; Isa 13:22Wanyama wa mwituni wataniheshimu,
mbweha na bundi,
kwa sababu ninawapatia maji jangwani,
na vijito katika nchi kame,
ili kuwapa watu wangu maji, wale niliowachagua,
43:21 Za 66:2; 1Pet 2:9; Mwa 2:7; Mal 3:17; Za 102:18watu wale niliowaumba kwa ajili yangu,
ili wapate kutangaza sifa zangu.