Daily Manna for Saturday, June 12, 2021

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Zaburi 6:1-10

Zaburi 6

6:1 Za 2:5Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,

wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

6:2 Za 4:1; 26:11; 61:2; 77:3; 142:3; Yer 3:12; 8:18; 12:15; 31:20; Hos 6:1; Isa 40:31; Za 32:3; 38:3; 42:10; 102:3Unirehemu Bwana,

kwa maana nimedhoofika;

Ee Bwana, uniponye,

kwa maana mifupa yangu

ina maumivu makali.

6:3 Ay 7:11; Za 4:2; 31:7; 38:8; 55:4; 89:46; Yn 12:27; Isa 6:11; Rum 9:2; 2Kor 2:4; Hab 1:12; 1Sam 1:14; 1Fal 18:21; Yer 4:14; Mt 26:38; Mit 18:14Nafsi yangu ina uchungu mwingi.

Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?

6:4 Za 25:16; 69:16; 71:2; 86:16; 88:2; 102:2; 119:132; 13:5; 31:2, 16; 77:8; 85:7; 119:41; Isa 54:8, 10Geuka Ee Bwana, unikomboe,

uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.

6:5 Za 30:9; 88:10-12; 115:17; Isa 38:18; Mhu 9:10Hakuna mtu anayekukumbuka

akiwa amekufa.

Ni nani awezaye kukusifu

akiwa kuzimu?

6:6 Ay 3:24; 16:16; 7:3; Lk 7:38; Za 77:3; 102:5; 12:5; Mdo 20:19; Mao 1:8, 11, 21, 22; Amu 8:5Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;

usiku kucha nafurikisha

kitanda changu kwa machozi;

nimelowesha viti vyangu vya fahari

kwa machozi.

6:7 Ay 16:8; Za 31:9; 69:3; 119:82; Isa 38:14Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,

yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.

6:8 Za 119:115; 5:5; 139:19; Mt 7:23Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,

kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.

6:9 Za 31:22; 116:1; 3:4; 40:1, 2; 28:6Bwana amesikia kilio changu kwa huruma,

Bwana amekubali sala yangu.

6:10 2Fal 19:26; Za 40:14Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,

watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.