Yeremia 31:16-18
31:16 Za 30:5; Isa 25:8; Rut 2:12; Eze 11:17-18; 2Nya 15:7; Yer 30:3; Isa 30:19Hili ndilo asemalo Bwana:
“Izuie sauti yako kulia,
na macho yako yasitoe machozi,
kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,”
asema Bwana.
“Watarudi kutoka nchi ya adui.
Kwa hiyo kuna tumaini kwa siku zijazo,”
asema Bwana.
“Watoto wako watarudi nchi yao yenyewe.
31:18 Ay 5:17; Hos 4:16; 10:11; Za 80:3-4; Mao 5:21; Yer 50:11“Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu:
‘Ulinirudi kama ndama mkaidi,
nami nimekubali kutii.
Unirudishe, nami nitarudi,
kwa sababu wewe ndiwe Bwana, Mungu wangu.