Daily Manna for Friday, May 7, 2021

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Zaburi 145:1-7

Zaburi 145

145:1 Za 30:1; 34:1; 2:6; 5:2; 54:6Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme,

nitalisifu jina lako milele na milele.

145:2 Za 71:6; 34:1; Isa 25:1; 26:8Kila siku nitakusifu

na kulitukuza jina lako milele na milele.

145:3 2Sam 22:4; Ay 5:9; Za 95:3; 96:4Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,

ukuu wake haupimiki.

145:4 Za 22:30; 71:16; Kum 11:19Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine,

watasimulia matendo yako makuu.

145:5 Za 96:6; 148:13; 75:1Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako,

nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.

145:6 Kum 32:3; Za 75:1; 78:4; 66:3; 106:2Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha,

nami nitatangaza matendo yako makuu.

145:7 Kut 18:9; Za 5:11; 27:13; 138:5; 101:1Wataadhimisha wema wako mwingi,

na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.