Daily Manna for Saturday, April 10, 2021

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Warumi 15:5-11

15:5 2Kor 13:11; Efe 4:3Mungu atoaye saburi na faraja, awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 15:6 Ufu 1; 6; Za 34:3; Mdo 4:24, 32ili kwa moyo mmoja mpate kumtukuza Mungu aliye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

15:7 Rum 14:1; 5:2Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu. 15:8 Mt 15:24; Mdo 3:25, 26; 2Kor 1:20Kwa maana nawaambia kwamba, Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, 15:9 Rum 3:29; Mt 9:8; 2Sam 22:50; Za 18:49pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa:

“Kwa hiyo nitakutukuza katikati ya watu wa Mataifa;

nitaliimbia sifa jina lako.”

15:10 Kum 32:43Tena yasema,

“Enyi watu wa Mataifa, furahini

pamoja na watu wa Mungu.”

15:11 Za 117:1Tena,

“Msifuni Bwana, ninyi watu wa Mataifa wote,

na kumwimbia sifa, enyi watu wote.”