1 Samuel 22 – NIV & NEN

New International Version

1 Samuel 22:1-23

David at Adullam and Mizpah

1David left Gath and escaped to the cave of Adullam. When his brothers and his father’s household heard about it, they went down to him there. 2All those who were in distress or in debt or discontented gathered around him, and he became their commander. About four hundred men were with him.

3From there David went to Mizpah in Moab and said to the king of Moab, “Would you let my father and mother come and stay with you until I learn what God will do for me?” 4So he left them with the king of Moab, and they stayed with him as long as David was in the stronghold.

5But the prophet Gad said to David, “Do not stay in the stronghold. Go into the land of Judah.” So David left and went to the forest of Hereth.

Saul Kills the Priests of Nob

6Now Saul heard that David and his men had been discovered. And Saul was seated, spear in hand, under the tamarisk tree on the hill at Gibeah, with all his officials standing at his side. 7He said to them, “Listen, men of Benjamin! Will the son of Jesse give all of you fields and vineyards? Will he make all of you commanders of thousands and commanders of hundreds? 8Is that why you have all conspired against me? No one tells me when my son makes a covenant with the son of Jesse. None of you is concerned about me or tells me that my son has incited my servant to lie in wait for me, as he does today.”

9But Doeg the Edomite, who was standing with Saul’s officials, said, “I saw the son of Jesse come to Ahimelek son of Ahitub at Nob. 10Ahimelek inquired of the Lord for him; he also gave him provisions and the sword of Goliath the Philistine.”

11Then the king sent for the priest Ahimelek son of Ahitub and all the men of his family, who were the priests at Nob, and they all came to the king. 12Saul said, “Listen now, son of Ahitub.”

“Yes, my lord,” he answered.

13Saul said to him, “Why have you conspired against me, you and the son of Jesse, giving him bread and a sword and inquiring of God for him, so that he has rebelled against me and lies in wait for me, as he does today?”

14Ahimelek answered the king, “Who of all your servants is as loyal as David, the king’s son-in-law, captain of your bodyguard and highly respected in your household? 15Was that day the first time I inquired of God for him? Of course not! Let not the king accuse your servant or any of his father’s family, for your servant knows nothing at all about this whole affair.”

16But the king said, “You will surely die, Ahimelek, you and your whole family.”

17Then the king ordered the guards at his side: “Turn and kill the priests of the Lord, because they too have sided with David. They knew he was fleeing, yet they did not tell me.”

But the king’s officials were unwilling to raise a hand to strike the priests of the Lord.

18The king then ordered Doeg, “You turn and strike down the priests.” So Doeg the Edomite turned and struck them down. That day he killed eighty-five men who wore the linen ephod. 19He also put to the sword Nob, the town of the priests, with its men and women, its children and infants, and its cattle, donkeys and sheep.

20But one son of Ahimelek son of Ahitub, named Abiathar, escaped and fled to join David. 21He told David that Saul had killed the priests of the Lord. 22Then David said to Abiathar, “That day, when Doeg the Edomite was there, I knew he would be sure to tell Saul. I am responsible for the death of your whole family. 23Stay with me; don’t be afraid. The man who wants to kill you is trying to kill me too. You will be safe with me.”

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 22:1-23

Daudi Akiwa Adulamu Na Mispa

122:1 Mwa 38:1Daudi akaondoka Gathi na kukimbilia kwenye pango la Adulamu. Ndugu zake na watu wa nyumba ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. 222:2 1Sam 23:13; 25:13; 2Sam 15:20; Amu 11:3Wale wote waliokuwa katika dhiki au waliokuwa na madeni au wale ambao hawakuridhika wakamkusanyikia Daudi, naye akawa kiongozi wao. Watu wapatao 400 walikuwa pamoja naye.

322:3 Mwa 47:11; Kut 20:12; Law 19:3; Kum 5:16; Mit 10:1; 23:24; Mt 19:19; Yn 19:25-27; Efe 6:2; 1Tim 5:4Kutoka huko Daudi akaenda Mispa huko Moabu na kumwambia mfalme wa Moabu, “Naomba uwaruhusu baba yangu na mama yangu waje kukaa nawe mpaka nijue nini Mungu atakachonifanyia.” 422:4 Mwa 19:37Hivyo akawaacha wazazi wake wakae na mfalme wa Moabu, nao wakakaa naye muda wote ambao Daudi alikuwa ngomeni.

522:5 2Sam 24:11; 1Nya 21:9; 29:29; 2Nya 29:25; 23:14Ndipo nabii Gadi akamwambia Daudi, “Usikae ngomeni. Nenda katika nchi ya Yuda.” Hivyo Daudi akaondoka na kwenda katika msitu wa Herethi.

Sauli Awaua Makuhani Wa Nobu

622:6 Amu 4:5; Mwa 21:23Basi Sauli akasikia kwamba Daudi na watu wake wameonekana. Sauli akiwa na mkuki mkononi, alikuwa ameketi chini ya mti wa mkwaju kwenye kilima huko Gibea, maafisa wake wote wakiwa wamesimama kumzunguka. 722:7 Kum 1:15; 1Sam 8:14Sauli akawaambia, “Sikilizeni enyi watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa ninyi nyote mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya ninyi nyote majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia? 822:8 1Sam 18:3; 20:16; 23:21Je, ndiyo sababu ninyi mkapanga hila mbaya dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu ambaye ameniambia ni lini mwanangu alifanya agano na mwana wa Yese. Hapana hata mmoja wenu anayejishughulisha nami wala anayeniambia kwamba mwanangu amechochea mtumishi wangu kunivizia, kama afanyavyo leo.”

922:9 1Sam 21:7; 14:3; 21:1; Za 52Lakini Doegi Mwedomu, ambaye alikuwa akisimama na maafisa wa Sauli, akasema, “Nilimwona mwana wa Yese akija kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu huko Nobu. 1022:10 Mwa 25:22; 1Sam 23:2; 21:6; 17:51; Hes 27:21; 27:21Ahimeleki akamuuliza Bwana kwa ajili yake; pia akampa vyakula na ule upanga wa Goliathi Mfilisti.”

11Kisha mfalme akatuma watu wamwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu, na jamaa yote ya baba yake, waliokuwa makuhani huko Nobu, nao wote wakaja kwa mfalme. 12Sauli akasema, “Sikiliza sasa, mwana wa Ahitubu.”

Akajibu, “Naam, bwana wangu.”

13Sauli akamwambia, “Kwa nini umepanga shauri baya dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, ukampa vyakula na upanga, tena hukumuuliza Mungu kwa ajili yake, na kwa sababu hiyo ameasi dhidi yangu na kunivizia, kama afanyavyo leo?”

1422:14 1Sam 19:4; 19:5; 20:32; 24:11; Mit 31:9Ahimeleki akamjibu mfalme, “Ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliye mwaminifu kama Daudi, mkwewe mfalme, kiongozi wa walinzi wako na anayeheshimika sana katika watu wa nyumbani mwako? 15Je, siku hiyo ilikuwa ndiyo ya kwanza kumwomba Mungu kwa ajili yake? La hasha! Mfalme na usiwashutumu watumishi wako wala yeyote wa jamaa ya baba yake, kwa kuwa mtumishi wako hafahamu lolote kabisa kuhusu jambo hili lote.”

1622:16 1Sam 2:31Lakini mfalme akasema, “Ahimeleki, hakika utakufa, wewe na jamaa yote ya baba yako.”

1722:17 Kut 1:17; Mdo 4:19; 5:29Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake waliokuwa kando yake: “Geukeni na kuwaua makuhani wa Bwana, kwa sababu nao pia wamejiunga na Daudi. Walijua kuwa alikuwa anakimbia, wala hawakuniambia.”

Lakini maafisa wa mfalme hawakuwa radhi kuinua mkono kuwaua makuhani wa Bwana.

1822:18 1Sam 4:17; 2:18; 2:31; Za 12:5; Mit 28:15; Kut 28:40Kisha mfalme akamwagiza Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Hivyo basi Doegi Mwedomu, akageuka na kuwaua. Siku ile aliwaua watu themanini na watano wavaao visibau vya kitani. 1922:19 1Sam 15:3; 21:1; Neh 11:32; Isa 10:32; Ay 20:19, 20; Za 10:1-18; Isa 26:13Pia akaupiga Nobu kwa upanga, mji wa makuhani, wakiwemo wanaume na wanawake, watoto wadogo na wale wanyonyao, ngʼombe wake, punda na kondoo.

2022:20 1Sam 23:6; 30:7; 2Sam 15:24; 20:25; 1Fal 1:7; 2:22, 26-27; 2Fal 4:4; 1Nya 15:11; 27:34; 1Sam 14:3; 2:32Lakini Abiathari, mwana wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, akatoroka, akakimbia na kujiunga na Daudi. 21Akamwambia Daudi kuwa Sauli amewaua makuhani wa Bwana. 2222:22 1Sam 21:7Kisha Daudi akamwambia Abiathari: “Siku ile, wakati Doegi Mwedomu alipokuwa pale, nilijua atahakikisha amemwambia Sauli. Mimi ninawajibika kwa vifo vya jamaa ya baba yako yote. 2322:23 1Sam 20:1Kaa pamoja nami; usiogope. Mtu anayeutafuta uhai wako anautafuta uhai wangu pia. Ukiwa pamoja nami utakuwa salama.”