Zekaria 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 5:1-11

Maono Ya Sita: Kitabu Kinachoruka

15:1 Za 10:7; Yer 36:4Nikatazama tena: na hapo mbele yangu kulikuwa na kitabu kilichoruka!

25:2 Yer 1:13Akaniuliza, “Unaona nini?”

Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka chenye, urefu wa dhiraa ishirini5:2 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. na upana wa dhiraa kumi.”5:2 Dhiraa 10 ni sawa mita 4.5.

35:3 Mal 3:9; Kut 20:15; 20:7; Isa 48:1Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atafukuziwa mbali, pia kufuatana na yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atafukuziwa mbali. 45:4 Zek 8:17; Law 14:34-35; Mit 3:33; Hab 2:9-11; Mal 3:5Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, ‘Nitaituma hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa Jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ”

Maono Ya Saba: Mwanamke Ndani Ya Kikapu

55:5 Mik 6:10Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone ni nini kile kinachojitokeza.”

6Nikamuuliza, “Ni kitu gani?”

Akanijibu, “Ni kikapu cha kupimia.” Kisha akaongeza kusema, “Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.”

7Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuwako mwanamke ameketi! 85:8 Mit 6:11Akasema, “Huu ni uovu,” tena akamsukumia ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu.

95:9 Law 11:19Kisha nikatazama juu: na pale mbele yangu, walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu na nchi.

10Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Wanakipeleka wapi hicho kikapu?”

115:11 Mwa 10:10; Yer 29:5, 28; Dan 1:2Akanijibu, “Wanakipeleka katika nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale mahali pake.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒迦利亚书 5:1-11

飞行的书卷

1我又举目观看,见有书卷在飞。 2天使问我:“你看见什么?”我说:“我看见一本飞行的书卷,长九米,宽四米半。” 3他说:“这是临到全天下的咒诅,因为书卷一面写着‘凡偷盗的必被清除’,另一面写着‘凡起假誓的必被清除’。” 4万军之耶和华说:“我要使这咒诅进入盗贼和奉我的名起假誓者的家,留在他们家里,直到毁灭一切,不留一木一石。”

量器中的女子

5与我说话的天使又来对我说:“你举目观看,看看出现了什么?” 6我问道:“这是什么?”他说:“这是一个量器。”接着他又说:“里面盛着天下人的罪。” 7只见量器的铅盖打开了,里面坐着一个女子。 8天使说:“这是罪恶。”他把女子推回量器中,盖上铅盖。 9我又举目观看,见有两个女子展翅飞来,她们的翅膀像鹳鸟的翅膀。她们把量器提到空中。 10我问与我说话的天使:“她们要把量器带到哪里?” 11他说:“要带到示拿5:11 “示拿”巴比伦的别名。,在那里为它建造房屋,建好后就把它安置在底座上。”