Zaburi 96 – NEN & NAV

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 96:1-13

Zaburi 96

Mungu Mfalme Mkuu

(1 Nyakati 16:23-33)

196:1 Za 30:4; 33:3; 40:4; 98:1; 144:9; Isa 42:10; Ufu 5:9Mwimbieni Bwana wimbo mpya;

mwimbieni Bwana dunia yote.

296:2 Isa 42:10; Ufu 5:9; Za 68:4; 27:1; 71:15Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake;

tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

396:3 Za 8:1; 71:17; 15:3Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

496:4 Za 48:1; 89:7; 95:3; Kum 28:58; 1Nya 16:25Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;

yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

596:5 Mwa 1:1; Isa 42:5; 41:24; Law 19:4; Yer 10:11; 2Nya 2:12; Hab 2:18-20; Mdo 19:26; 1Kor 8:4, 5Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,

lakini Bwana aliziumba mbingu.

696:6 Za 21:5; 29:1; 89:17Fahari na enzi viko mbele yake;

nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

796:7 Za 29:1; 22:27Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,

mpeni Bwana utukufu na nguvu.

896:8 Za 45:12; 51:19; 72:10; 65:4; 84:10; 92:13; 100:4Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;

leteni sadaka na mje katika nyua zake.

996:9 Kut 15:14; 23:25; Yon 1:9; Za 93:5; 114:7; 33:8Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake;

dunia yote na itetemeke mbele zake.

1096:10 Za 97:1; 24:2; 78:69; 119:90; 93:1; 58:11; 67:4; 98:9Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.”

Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa;

atawahukumu watu kwa uadilifu.

1196:11 Ufu 12:12; Za 97:1; Isa 49:13Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;

bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

1296:12 Isa 44:23; 55:12; Eze 17:24; Za 65:13mashamba na yashangilie,

pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.

Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;

1396:13 Ufu 19:11; Za 7:11; Mdo 17:31; Za 86:11itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja,

anakuja kuihukumu dunia.

Ataihukumu dunia kwa haki,

na mataifa katika kweli yake.

New Arabic Version

مزمور 96:1-13

الْمَزْمُورُ السَّادِسُ وَالتِّسْعُونَ

1رَنِّمُوا لِلرَّبِّ تَرْنِيمَةً جَدِيدَةً. رَنِّمُوا لِلرَّبِّ يَا سَاكِنِي الأَرْضِ جَمِيعاً. 2رَنِّمُوا للرَّبِّ. بَارِكُوا اسْمَهُ. بَشِّرُوا بِخَلاصِهِ يَوْماً فَيَوْماً. 3أَعْلِنُوا مَجْدَهُ بَيْنَ الأُمَمِ، وَعَجَائِبَهُ بَيْنَ الشُّعُوبِ كُلِّهَا. 4فَإِنَّ الرَّبَّ عَظِيمٌ وَجَدِيرٌ بِكُلِّ حَمْدٍ؛ هُوَ مَرْهُوبٌ أَكْثَرَ جِدّاً مِنْ جَمِيعِ الآلِهَةِ. 5لأَنَّ كُلَّ آلِهَةِ الشُّعُوبِ أَصْنَامٌ بَاطِلَةٌ أَمَّا الرَّبُّ فَهُوَ صَانِعُ السَّمَاوَاتِ. 6الْجَلالُ وَالْبَهَاءُ أَمَامَهُ، الْقُوَّةُ وَالْجَمَالُ فِي مَقْدِسِهِ.

7قَدِّمُوا لِلرَّبِّ يَا جَمِيعَ قَبَائِلِ الشُّعُوبِ، قَدِّمُوا لِلرَّبِّ مَجْداً وَقُوَّةً. 8قَدِّمُوا لِلرَّبِّ الْمَجْدَ الْوَاجِبَ لاسْمِهِ. أَحْضِرُوا تَقْدِمَةً وَادْخُلُوا هَيْكَلَهُ وَاعْبُدُوهُ 9اسْجُدُوا لِلرَّبِّ بِزِينَةٍ مُقَدَّسَةٍ، ارْتَعِدُوا أَمَامَهُ يَا جَمِيعَ سَاكِنِي الأَرْضِ. 10نَادُوا بَيْنَ الأُمَمِ أَنَّ الرَّبَّ قَدْ مَلَكَ. هُوَذَا الأَرْضُ قَدِ اسْتَقَرَّتْ مُطْمَئِنَّةً لأَنَّهُ يَدِينُ الشُّعُوبَ بِالإِنْصَافِ. 11لِتَفْرَحِ السَّمَاوَاتُ وَلْتَبْتَهِجِ الأَرْضُ وَلْيَهْدِرِ الْبَحْرُ بَهْجَةً بِأَمْوَاجِهِ وَبِكُلِّ مَا يَحْوِيهِ. 12لِيَتَهَلَّلِ الْحَقْلُ وَكُلُّ مَا فِيهِ، فَتَتَرَنَّمَ فَرَحاً جَمِيعُ أَشْجَارِ الْغَابَةِ 13فِي حَضْرَةِ الرَّبِّ لأَنَّهُ آتٍ لِيَدِينَ الْعَالَمَ بِالْعَدْلِ وَالشُّعُوبَ بِالْحَقِّ.