Zaburi 84
Kuionea Shauku Nyumba Ya Mungu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora.
184:1 Kum 33:27; Za 27:4; 43:3; 90:1; 132:5; 26:8; 27:4; Ebr 9:23; Ufu 21:2, 3Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
makao yako yapendeza kama nini!
284:2 Ay 19:27; Yos 3:10Nafsi yangu inatamani sana,
naam, hata kuona shauku,
kwa ajili ya nyua za Bwana;
moyo wangu na mwili wangu
vinamlilia Mungu Aliye Hai.
384:3 Za 2:6; 5:2; 43:4; Yer 44:11Hata shomoro amejipatia makao,
mbayuwayu amejipatia kiota
mahali awezapo kuweka makinda yake:
mahali karibu na madhabahu yako,
Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,
wanaokusifu wewe daima.
584:5 Za 81:1; Yer 31:6Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,
na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
684:6 Ay 38:26; Yoe 2:23Wanapopita katika Bonde la Baka,84:6 Yaani Bonde la Vilio.
hulifanya mahali pa chemchemi,
pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.84:6 Au: baraka.
784:7 Ay 17:9; Kum 16:16; 1Fal 8:1Huendelea toka nguvu hadi nguvu,
hadi kila mmoja afikapo
mbele za Mungu huko Sayuni.
884:8 Za 4:1Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu;
nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.
984:9 1Sam 16:6; Za 2:2; 59:11; 18:50; 132:17Ee Mungu, uitazame ngao yetu,
mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.
1084:10 1Nya 23:5Siku moja katika nyua zako ni bora
kuliko siku elfu mahali pengine;
afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu
kuliko kukaa katika mahema ya waovu.
1184:11 Isa 60:19; Yer 43:13; Ufu 21:23; Mwa 15:1; Za 34:10Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao,
Bwana hutoa wema na heshima;
hakuna kitu chema anachowanyima
wale ambao hawana hatia.
1284:12 Za 2:12Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.