Zaburi 43
Maombi Ya Mtu Aliyeko Uhamishoni Yanaendelea
143:1 Amu 6:31; Za 25:20; 36:3; 109:2; 7:8Ee Mungu unihukumu,
nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu,
niokoe na watu wadanganyifu na waovu.
243:2 Za 44:9; 74:1; 88:14; 89:38; 35:14; 42:9; 28:7; Isa 26:4Wewe ni Mungu ngome yangu.
Kwa nini umenikataa?
Kwa nini niendelee kuomboleza,
nikiwa nimeonewa na adui?
343:3 Za 2:6; 3:4; 27:1; 26:3; 25:5; 2Sam 15:25Tuma hima nuru yako na kweli yako
na viniongoze;
vinilete mpaka mlima wako mtakatifu,
mpaka mahali unapoishi.
443:4 Za 42:2; 26:6; 84:3; 21:6; 16:3; Mwa 4:21Ndipo nitakwenda madhabahuni pa Mungu,
kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu.
Nitakusifu kwa kinubi,
Ee Mungu, Mungu wangu.
543:5 Za 42:5, 6, 11Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa sababu bado nitamsifu
Mwokozi wangu na Mungu wangu.