Zaburi 32
Furaha Ya Msamaha
Zaburi ya Daudi. Funzo.
132:1 Za 85:2; 103:3; Rum 4:6Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,
ambaye dhambi zake zimefunikwa.
232:2 Rum 4:7-8; 5:13; Yn 1:47; Ufu 14:5; 2Kor 1:12; Law 17:4Heri mtu yule ambaye Bwana
hamhesabii dhambi,
na ambaye rohoni mwake
hamna udanganyifu.
332:3 Ay 31:34; 31:10; 3:24; Za 6:6Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa
kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.
432:4 1Sam 5:6; Ay 9:34; Za 38:2; 39:10; 22:15Usiku na mchana
mkono wako ulinilemea,
nguvu zangu zilinyonywa
kama vile katika joto la kiangazi.
532:5 Ay 31:33; Mit 28:13; Lk 15:18; Za 103:12; Law 26:40; Yn 1:9Kisha nilikujulisha dhambi yangu
wala sikuficha uovu wangu.
Nilisema, “Nitaungama
makosa yangu kwa Bwana.”
Ndipo uliponisamehe
hatia ya dhambi yangu.
632:6 Za 69:13; Yn 7:34; Isa 55:6; Za 69:1; 43:2; Kut 15:10; 1Tim 1:16Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe
wakati unapopatikana,
hakika maji makuu yatakapofurika
hayatamfikia yeye.
732:7 Za 9:9; Amu 9:35; 5:1; Mit 18:10; Isa 4:6; Mt 23:37; Kol 3:3Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,
utaniepusha na taabu
na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.
832:8 Za 25:8; 34:11; 33:18; Isa 48:17Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;
nitakushauri na kukuangalia.
932:9 Ay 30:11; 39:10; Yak 3:3Usiwe kama farasi au nyumbu
wasio na akili,
ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu
la sivyo hawatakukaribia.
1032:10 Rum 2:9; Za 4:5; Mit 16:20; Yer 17:7; Mit 13:21; 16:20Mtu mwovu ana taabu nyingi,
bali upendo usio na kikomo wa Bwana
unamzunguka mtu anayemtumaini.
1132:11 Za 64:10Shangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki!
Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!