Zaburi 19
Utukufu Wa Mungu Katika Uumbaji
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
119:1 Isa 6:3; 40:22; Za 4:2; 97:6; 89:5; 50:6; 8:1, 6; 148:3; 103:22; Rum 1:19; Mwa 1:8Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu,
anga zahubiri kazi ya mikono yake.
219:2 Za 74:16Siku baada ya siku zinatoa habari,
usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.
3Hakuna msemo wala lugha,
ambapo sauti zao hazisikiki.
419:4 Rum 10:18; Za 104:2; Ay 36:29; Amu 5:31Sauti yao imeenea duniani pote,
nayo maneno yao yameenea
hadi miisho ya ulimwengu.
Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,
519:5 1Sam 17:4; Mhu 11:7; Yoe 2:16; Ay 36:29linafanana na bwana arusi
akitoka chumbani mwake,
kama shujaa afurahiavyo
kukamilisha kushindana kwake.
619:6 Kum 30:4; Za 11:3; Mhu 1:5Huchomoza upande mmoja wa mbingu,
na kufanya mzunguko wake
hadi upande mwingine.
Hakuna kilichojificha joto lake.
719:7 Yak 1:25; Kum 4:6; Za 1:2; 23:3; 93:5; 119:130, 138, 142, 144; 11:7Sheria ya Bwana ni kamilifu,
ikihuisha nafsi.
Shuhuda za Bwana ni za kuaminika,
zikimpa mjinga hekima.
819:8 Za 33:4; 38:10; 119:14, 128; Ezr 9:7; Neh 9:13; Rum 7:12Maagizo ya Bwana ni kamili,
nayo hufurahisha moyo.
Amri za Bwana huangaza,
zatia nuru machoni.
919:9 Mhu 12:13; Isa 33:6; Za 34:11; 111:10; 119:138; Mit 1:7Kumcha Bwana ni utakatifu,
nako kwadumu milele.
Amri za Bwana ni za hakika,
nazo zina haki.
1019:10 Ay 22:24; Eze 3:3; Mit 8:10; 1Sam 14:27; Za 119:72, 103Ni za thamani kuliko dhahabu,
kuliko dhahabu iliyo safi sana,
ni tamu kuliko asali,
kuliko asali kutoka kwenye sega.
1119:11 Mit 6:22Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,
katika kuzishika kuna thawabu kubwa.
1219:12 Za 51:2; 90:8; Mhu 12:14Ni nani awezaye kutambua makosa yake?
Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.
1319:13 Hes 15:30; Mwa 6:9; Za 18:32; 119:133Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi,
nazo zisinitawale.
Ndipo nitakapokuwa sina lawama,
wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.
1419:14 Za 104:34; 18:31; Kut 6:6; Isa 44:6; Ay 19:25Maneno ya kinywa changu
na mawazo ya moyo wangu,
yapate kibali mbele zako, Ee Bwana,
Mwamba wangu na Mkombozi wangu.