Zaburi 150
Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake
1150:1 Za 112:1; 73:17; 68:24-26; 102:19; 148:1Msifuni Bwana.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake,
msifuni katika mbingu zake kuu.
2150:2 Kum 3:24; Kut 15:7Msifuni kwa matendo yake makuu,
msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3150:3 Hes 10:2; Za 57:8Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,
msifuni kwa kinubi na zeze,
4150:4 Kut 15:20; Za 45:8; Isa 38:20; Mwa 4:21msifuni kwa matari na kucheza,
msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
5150:5 2Sam 6:5msifuni kwa matoazi yaliayo,
msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6150:6 Za 103:22; Ufu 5:13Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.
Msifuni Bwana!