Zaburi 129
Maombi Dhidi Ya Adui Za Israeli
Wimbo wa kwenda juu.
1129:1 Kut 1:13; Eze 23:3; Za 88:15; 124:1; Hos 2:15Wamenionea mno tangu ujana wangu;
Israeli na aseme sasa:
2129:2 Yer 1:19; 15:20; 20:11wamenionea mno tangu ujana wangu,
lakini bado hawajanishinda.
3129:3 Ebr 11:26Wakulima wamelima mgongo wangu,
na kufanya mifereji yao mirefu.
4129:4 Kut 9:27; 2The 1:6; Za 37:9; 140:5Lakini Bwana ni mwenye haki;
amenifungua toka kamba za waovu.
5129:5 Mik 4:11; Za 70:2Wale wote waichukiao Sayuni
na warudishwe nyuma kwa aibu.
6129:6 Isa 37:27; 2Fal 19:26; Za 102:11; 37:2; Yer 17:5-6Wawe kama majani juu ya paa,
ambayo hunyauka kabla hayajakua;
7129:7 Kum 28:38; Za 79:12kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,
wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8129:8 Za 118:26; Rut 2:4Wale wapitao karibu na wasiseme,
“Baraka ya Bwana iwe juu yako;
tunakubariki katika jina la Bwana.”