Zaburi 109
Lalamiko La Mtu Aliyeko Kwenye Shida
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1109:1 Kut 15:2; Yer 17:14; Ay 34:29; Za 83:1Ee Mungu, ambaye ninakusifu,
usiwe kimya,
2109:2 Za 43:1; 52:4kwa maana watu waovu na wadanganyifu
wamefungua vinywa vyao dhidi yangu;
wasema dhidi yangu
kwa ndimi za udanganyifu.
3109:3 Za 69:4; 35:7; 35:7, 10; Yn 15:25; 1Sam 19:4, 5Wamenizunguka kwa maneno ya chuki,
wananishambulia bila sababu.
4109:4 Za 69:13; 141:5Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki,
lakini mimi ninawaombea.
5109:5 Mwa 44:4; Za 38:20Wananilipiza mabaya kwa mema,
chuki badala ya urafiki wangu.
6109:6 1Nya 21:1; Ay 1:6; Zek 3:1Agiza mtu mwovu ampinge,
mshtaki109:6 Mshtaki hapa maana yake ni Shetani. asimame mkono wake wa kuume.
7109:7 Za 1:5; Mit 28:9; Zek 3:1Anapohukumiwa, apatikane na hatia,
nayo maombi yake yamhukumu.
8109:8 Ay 15:32; Mdo 1:20Siku zake za kuishi na ziwe chache,
nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine.
9109:9 Kut 22:24; Yer 18:21Watoto wake na waachwe yatima,
mke wake na awe mjane.
10109:10 Mwa 4:12Watoto wake na watangetange wakiomba,
na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao.
11109:11 Hes 14:3; Isa 1:7; 6:11; 36:1; Mao 5:2; Neh 5:3; Ay 20:18; 18:9Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo,
matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni.
12109:12 Ay 5:4Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema
wala wa kuwahurumia yatima wake.
13109:13 Za 21:10; 9:5; 37:28; Hes 14:12; Mit 10:7; Ay 18:19Uzao wake na ukatiliwe mbali,
majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.
14109:14 Kut 20:5Maovu ya baba zake na yakumbukwe
mbele za Bwana,
dhambi ya mama yake
isifutwe kamwe.
15109:15 Za 90:8; Kut 17:14; Kum 32:26; Ay 18:17Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana,
ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.
16109:16 Ay 20:19; Za 35:10; 34:18Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema,
bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,
aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.
17109:17 Mit 28:27; Mt 7:2Alipenda kulaani,
nayo laana ikampata;
hakupenda kubariki,
kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.
18109:18 Za 10:7; Hes 5:22Alivaa kulaani kama vazi lake,
nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji,
kwenye mifupa yake kama mafuta.
19109:19 Za 109:29; 73:6; Eze 7:27Na iwe kama joho alilozungushiwa,
kama mshipi aliofungiwa daima.
20109:20 Kut 32:34; Za 54:5; 94:23; 7:10; Isa 3:11; 2Tim 4:14Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu,
kwa wale wanaoninenea mabaya.
21109:21 Kut 9:16; Za 3:7; 23:3; 69:16Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi,
unitendee wema kwa ajili ya jina lako,
uniokoe kwa wema wa pendo lako.
22Maana mimi ni maskini na mhitaji,
moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23109:23 Ay 14:2Ninafifia kama kivuli cha jioni,
nimerushwa-rushwa kama nzige.
24109:24 Ebr 12:12; Ay 16:8; Za 35:13Magoti yangu yamelegea kwa kufunga,
mwili wangu umedhoofika na kukonda.
25109:25 Za 22:6; Ay 16:4; Mt 27:39; Mk 15:29; Isa 37:22Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu,
wanionapo, hutikisa vichwa vyao.
26109:26 Za 12:1; 119:86Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie,
niokoe sawasawa na upendo wako.
27109:27 Ay 37:7Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako,
kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.
28109:28 2Sam 16:12; Za 66:4; Isa 35:10; 51:11; 54:1; 65:14; Hes 22:12Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki,
watakaposhambulia wataaibishwa,
lakini mtumishi wako atashangilia.
29109:29 Za 35:26Washtaki wangu watavikwa fedheha,
na kufunikwa na aibu kama joho.
30109:30 Za 35:18Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana,
katika umati mkubwa nitamsifu.
31109:31 Za 16:8; 108:6Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji,
kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.