Zaburi 1010 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Sala Kwa Ajili Ya Haki
110:1 Za 13:1; 22:1, 11; 35:22; 38:21; 71:12Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali?
Kwa nini unajificha wakati wa shida?
210:2 Ay 20:19; Mit 5:22; 10:3; Za 49:6; 94:4; Yer 48:30; Ay 1:5Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini,
waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.
3Hujivunia tamaa za moyo wake;
humbariki mlafi na kumtukana Bwana.
410:4 Za 12:3-5; 36:1; 2Fal 18:35; Ay 21:15Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu,
katika mawazo yake yote
hakuna nafasi ya Mungu.
510:5 Za 18:27; 105:5; Mit 6:17; Isa 13:11; Yer 48:29Njia zake daima hufanikiwa;
hujivuna na amri zako ziko mbali naye,
huwacheka kwa dharau adui zake wote.
610:6 Ufu 18:7Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa,
daima nitakuwa na furaha,
kamwe sitakuwa na shida.”
710:7 Mhu 4:1; Rum 3:14; Isa 30:12; Ay 20:12; Za 73:8; 119:134Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho;
shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.
810:8 Za 37:32; 59:3; 71:10; Mit 1:11; Yer 5:26; Mik 7:2; Hos 6:9Huvizia karibu na vijiji;
kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia,
akivizia wapitaji.
910:9 Ay 18:8Huvizia kama simba aliye mawindoni;
huvizia kumkamata mnyonge,
huwakamata wanyonge na kuwaburuza
katika wavu wake.
1010:10 Ay 9:17Mateka wake hupondwa, huzimia;
wanaanguka katika nguvu zake.
1110:11 Ay 22:13; 22:14; Za 42:9; 77:9Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau,
huficha uso wake na haoni kabisa.”
1210:12 Za 3:7; 9:12, 13; 17:7; 20:6; 106:26; Isa 26:11; Mik 5:9Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu.
Usiwasahau wanyonge.
1310:13 Ay 31:14Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?
Kwa nini anajiambia mwenyewe,
“Hataniita nitoe hesabu?”
1410:14 Za 22:11; 37:5; Kum 33:29Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,
umekubali kuyapokea mkononi mwako.
Mhanga anajisalimisha kwako,
wewe ni msaada wa yatima.
1510:15 Ay 31:22Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya,
mwite atoe hesabu ya maovu yake
ambayo yasingejulikana.
1610:16 Kut 15:18; Kum 8:20Bwana ni Mfalme milele na milele,
mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
1710:17 Za 9:12; Kut 22:23Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa,
wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,
1810:18 Kum 24:17; Za 146:9; 9:9ukiwatetea yatima na walioonewa,
ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.