Yoshua 8 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 8:1-35

Mji Wa Ai Waangamizwa

18:1 Mwa 26:24; Kum 31:6; Hes 14:9; Kum 1:21; Yos 10:7; 7:2; 9:3; 10:1; 12:9; 6:2Ndipo Bwana akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usivunjike moyo. Chukua jeshi lote la vita uende pamoja nalo kuishambulia Ai. Kwa kuwa nimeshamweka mikononi mwako mfalme wa Ai, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake. 28:2 Mwa 49:27; Kum 20:14; Amu 9:43; 20:29; Yos 6:21Utafanya Ai na mfalme wake kama ulivyofanya kwa mji wa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mnaweza kuchukua mateka wake na mifugo wake, kwa ajili yenu. Weka waviziaji upande wa nyuma ya mji.”

3Basi Yoshua na jeshi lote wakainuka kushambulia Ai. Akachagua watu mashujaa elfu thelathini walio bora miongoni mwa wapiganaji wake, akawapeleka wakati wa usiku 48:4 Amu 20:29; 2Nya 13:13akiwaagiza: “Sikilizeni kwa makini. Mtavizia nyuma ya mji. Msiende mbali sana na mji. Wote kuweni macho. 58:5 Amu 20:35Mimi na watu walio pamoja nami, tutaukabili mji, kisha itakuwa hapo watu watakapotoka nje kupigana nasi, kama walivyofanya hapo kwanza, sisi tutawakimbia. 6Watatufuatilia mpaka tutakapokuwa tumewavuta mbali na mji kwa kuwa watasema, ‘Wanatukimbia, kama walivyofanya hapo awali.’ Hivyo tutakapowakimbia, 78:7 Amu 7:7; 1Sam 23:4ninyi inawapasa mwinuke mtoke huko mafichoni na kuuteka mji. Bwana Mungu wenu atautia mkononi mwenu. 88:8 Amu 20:29-38; 2Sam 13:28; Yos 1:16Mtakapokuwa mmeuteka mji, uteketezeni kwa moto. Fanyeni kama vile Bwana alivyoamuru. Angalieni, nimewaagiza.”

98:9 2Nya 13:13Ndipo Yoshua akawatuma watu, nao wakaenda mahali pa kujificha, wakawa wanavizia kati ya Betheli na Ai, kuelekea upande wa magharibi wa Ai, lakini Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku huo.

108:10 Mwa 22:3; Yos 7:6; 6:12; Za 101:8; 119:60; Mhu 9:10; Yer 21:12Asubuhi na mapema siku iliyofuatia, Yoshua akawakutanisha watu wake, na yeye na viongozi wa Israeli wakawa mbele ya watu kwenda Ai. 11Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda, wakakaribia na kufika mbele ya mji. Wakapiga kambi kaskazini mwa Ai, pakiwa na bonde kati yao na huo mji. 128:12 Mwa 12:8; 28:19Yoshua alikuwa amewachukua watu wapatao elfu tano, akawaweka katika uavizi kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa mji. 13Wakawaweka askari katika maeneo yao: wale wote waliokuwa kambini wakawa kaskazini ya mji na wale waliokuwa wakivizia wakawa upande wa magharibi. Usiku huo Yoshua akaenda katika lile bonde.

148:14 Kum 1:1; Amu 20:34; Mt 24:39; 1The 5:1-3; 2Pet 2:3Mfalme wa Ai alipoona jambo hili, yeye pamoja na watu wote wa mji wakatoka kwa haraka asubuhi na mapema, ili kukutana na Israeli katika vita mahali fulani panapotazamana na Araba. Lakini hakujua kwamba kulikuwa kumewekwa waviziaji dhidi yake nyuma ya mji. 158:15 Amu 20:36; Yos 15:61; 18:12Yoshua na Israeli wote wakaruhusu kurudishwa nyuma mbele yao, na kuelekea jangwani. 168:16 Amu 20:31; Kut 14:3-4; Za 9:16Watu wote wa Ai wakaitwa ili kuwafuatia, nao wakavutwa kumfuatia Yoshua mbali na mji. 17Hakuna hata mwanaume mmoja aliyebakia Ai wala Betheli ambaye hakufuatia Israeli. Wakauacha mji wazi na kuwafuatia Israeli.

188:18 Ay 41:26; Za 35:3; Kut 4:2; 17:9-12; 14:16; Kum 7:23-24; 9:3; Yos 1:5; Yer 49:3Ndipo Bwana akamwambia Yoshua, “Inua huo mkuki ulio mkononi mwako kuuelekeza Ai, kwa kuwa nitautia huo mji mkononi mwako.” Hivyo Yoshua akauelekeza mkuki wake Ai. 198:19 Amu 20:33Mara tu alipofanya hivi, wale watu waliokuwa mavizioni wakaondoka upesi kutoka mahali pao na kukimbilia mbele. Wakaingia ndani ya mji, wakauteka na kuutia moto kwa haraka.

208:20 Amu 20:40Watu wa Ai wakaangalia nyuma, wakauona moshi wa huo mji ukielekea angani lakini hawakuwa na nafasi ya kutoroka kwa upande wowote, kwa kuwa wale Waisraeli waliokuwa wanawakimbia kuelekea jangwani walikuwa wamegeuka nyuma kuwakabili wakimbizaji wao. 21Basi Yoshua na Israeli wote walipoona kwamba waviziaji wameshauteka mji na moshi ulikuwa unapaa juu kutoka kwenye mji, wakawageukia watu wa Ai na kuwashambulia. 228:22 Kum 7:2; Yos 10:1; Law 27:29; Ay 20:5; Lk 17:26-30Wale waviziaji nao pia wakatoka nje ya mji dhidi yao, hivi kwamba wakashikiwa katikati, Waisraeli wakiwa pande zote mbili. Israeli wakawaua, bila kuwaachia yeyote aliyenusurika wala aliyetoroka. 238:23 1Sam 15:8Lakini wakamchukua mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua.

24Israeli ilipomaliza kuwaua wanaume wote wa Ai katika mashamba na jangwani walipokuwa wamewafukuzia, na baada ya kila mmoja wao kuuawa kwa upanga, Waisraeli wote wakarudi Ai na kuwaua wale waliokuwa wamebakia mjini. 258:25 Kum 20:16-18Watu kumi na mbili elfu, waume kwa wake, waliangamia siku ile, yaani watu wote wa Ai. 268:26 Hes 21:2; 17:12Kwa maana Yoshua hakuurudisha ule mkono wake uliokuwa umeuinua mkuki hadi alipomaliza kuwaangamiza wote walioishi Ai. 278:27 Hes 31:22, 26; Mt 20:15Lakini Israeli wakajichukulia mifugo na nyara za mji huu, kama vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Yoshua.

288:28 Hes 31:10; Yos 7:2; Yer 49:3; Kum 13:16; Yos 10:1; Mwa 35:20; 2Fal 19:25; Isa 17:1; 25:2; Yer 9:11Kwa hiyo Yoshua akauchoma moto mji wa Ai na kuufanya kuwa lundo la magofu la kudumu, mahali pa ukiwa hadi leo. 298:29 Kum 21:23; Yn 19:31; 2Sam 18:17; Yos 10:26, 27; Za 107:40; 110:5; Yos 7:26; 10:27Akamwangika mfalme wa Ai kwenye mti na kumwacha hapo mpaka jioni. Wakati wa jua kutua, Yoshua akawaamuru wautoe mwili wake kwenye mti na kuutupa kwenye ingilio la lango la mji. Kisha wakalundika mawe makubwa mengi juu yake, ambayo yamesalia mpaka leo.

Agano Linafanywa Upya Katika Mlima Ebali

308:30 Kum 11:29; Kut 20:24; Mwa 8:20; 12:7-8Kisha Yoshua akajenga madhabahu ya Bwana, Mungu wa Israeli, katika Mlima wa Ebali, 318:31 Kut 20:24-25; Kum 27:6-7kama Mose mtumishi wa Bwana alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Sheria ya Mose: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.8:31 Sadaka za ushirika. 328:32 Kum 27:8Pale, mbele ya Waisraeli Yoshua akanakili juu ya hayo mawe sheria ya Mose, aliyokuwa ameiandika. 338:33 Law 16:29; Kum 31:12; 11:29; Yn 4:20; 1Nya 15:11-13; Law 24:22; Hes 15:16Israeli yote, wageni na wazawa sawasawa, wakiwa na wazee wao, maafisa na waamuzi, walikuwa wamesimama pande zote mbili za Sanduku la Agano la Bwana, wakiwaelekea wale waliokuwa wamelichukua, yaani makuhani, ambao ni Walawi. Nusu ya watu ilisimama mbele ya Mlima Gerizimu na nusu hiyo ingine ikasimama mbele ya Mlima Ebali, kama vile Mose mtumishi wa Bwana alivyokuwa ameamuru hapo mwanzo alipotoa maagizo ya kuwabariki watu wa Israeli.

348:34 Kum 28:61; 31:11; Neh 8:3; Kum 29:20-21Hatimaye, Yoshua akasoma maneno yote ya sheria, yaani baraka na laana, kama vile ilivyoandikwa katika Kitabu cha Sheria. 358:35 Kut 12:38; Kum 31:12; Yos 1:8Hakuna neno lolote katika yale yote ambayo Mose alikuwa ameamuru ambalo Yoshua hakulisomea kusanyiko lote la Israeli, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, na wageni walioishi miongoni mwao.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

約書亞記 8:1-35

艾城之戰

1耶和華對約書亞說:「不要驚慌害怕。只管率領全軍去攻打城,我已經將城的王、他的人民、城池和土地都交在你手裡了。 2你怎樣對待耶利哥耶利哥王,也要照樣對待城和城的王。不過你們可以拿城中的財物和牲畜。你要在城後設下伏兵。」

3於是,約書亞率領全軍前往城。他挑選了三萬精兵,派他們在黑夜出發, 4並吩咐他們說:「你們要在城後埋伏,不可離城太遠,全體保持戒備。 5我會率領軍隊正面攻城,當敵人像上次那樣出城應戰時,我們便逃跑。 6他們必定乘勝追擊,我們便引他們離城,因為敵人一定會以為我們又像上次一樣臨陣逃跑。 7那時,你們便從埋伏的地方衝出來攻佔城,你們的上帝耶和華一定會把城交在你們手裡。 8你們攻陷城後,要照耶和華的話放火焚城。這是我的命令。」 9於是,約書亞派遣他們出去。他們去埋伏在伯特利城之間,就是城的西面。那一夜,約書亞住在民眾當中。

10清早,約書亞召集民眾,與以色列的眾首領率全軍前往城。 11隨他同去的軍隊都向前推進,來到城外,在城的北面紮營,與城相隔一個山谷。 12約書亞選了五千人,讓他們埋伏在城和伯特利之間,就是城的西面。 13於是,城北的主力軍隊和城西的伏兵都部署好了。當晚,約書亞在山谷裡過夜。 14城的王見以色列人兵臨城下,清早便急忙和全城的人起來出城迎戰,在亞拉巴谷附近跟以色列軍交鋒,他不知道城後有伏兵。 15約書亞帶領以色列軍詐敗,沿著通往曠野的路逃跑。 16城的人都被召去追趕以色列人,他們追擊約書亞,被誘出城來。 17這樣,伯特利城的人傾巢而出,追殺以色列人,他們的城門大開。

18耶和華對約書亞說:「把你手中的矛指向城,因為我要將這城交在你手裡。」約書亞就把手中的矛指向城。 19他一伸手,城後的伏兵立即行動,迅速衝進城去,一舉佔領城,隨即放火燒城。 20城的人回頭發現城內煙氣沖天,卻無路可逃,因為那些逃往曠野的以色列人已掉頭攻擊他們。 21約書亞以色列全軍見伏兵已經佔領城,城中濃煙滾滾,便掉頭攻擊城的人。 22伏兵也出城追擊城的人。以色列軍前後夾攻,把敵人圍困在中間全部殲滅,無一漏網。 23他們生擒了城的王,將他押到約書亞那裡。

24以色列軍在田間和曠野用刀殺盡了追趕他們的城人後,又進城殺了留在城裡的人, 25當天被殺的城人男男女女共有一萬二千人。 26一直到城所有的人都被殺光了,約書亞才收回手中的矛。 27以色列人照耶和華對約書亞的吩咐,只帶走了城中的牲畜和財物。 28約書亞燒毀全城,使城永遠成為一堆廢墟,至今仍一片荒涼。 29約書亞又將城王的屍體掛在樹上示眾。黃昏時,他才吩咐人把屍體取下來扔在城門口,又在屍體上堆了一大堆石頭。石堆至今還在。

重申律法

30-31約書亞照耶和華的僕人摩西以色列人的吩咐,在以巴路山上為以色列的上帝耶和華築了一座祭壇。這壇是按照摩西律法書的記載,用未經鐵器鑿過的原石築的。以色列人就在這壇上把燔祭和平安祭獻給耶和華。 32約書亞又在眾人面前,將摩西所寫的律法刻在石頭上。 33所有以色列人與他們的長老、官員和審判官都站在耶和華的約櫃兩旁,面對著抬約櫃的利未祭司,寄居的外族人和本族人都在場。他們一半人站在基利心山前,一半人站在以巴路山前,正如耶和華的僕人摩西從前祝福他們時所吩咐的。 34隨後,約書亞按照摩西律法書的記載,向民眾宣讀一切祝福和咒詛的話。 35他在全體會眾,包括婦女、小孩以及住在他們中間的外族人面前,一字不漏地宣讀摩西的一切吩咐。