Yoshua 6 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 6:1-27

Yeriko Yatekwa Na Kuangamizwa

16:1 Yos 24:11Basi malango ya Yeriko yalifungwa kwa uthabiti kwa ajili ya Waisraeli. Hakuna mtu yeyote aliyetoka au kuingia.

26:2 Kum 7:24; Yos 8:1; Amu 11:21; 2Sam 5:19; Neh 9:24; Dan 5:18-19Kisha Bwana akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wote wenye silaha. Fanya hivi kwa siku sita. 46:4 Kut 19:13; Law 25:9; Hes 10:8; Amu 7:16Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo dume mbele ya Sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 56:5 Kut 19:13; 1Sam 6:15; Ezr 3:11; 10:12; Za 42:4; 95:1; Isa 8:9; 42:13Utakapowasikia wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele.”

6Ndipo Yoshua mwana wa Nuni akaita makuhani na kuwaambia, “Chukueni Sanduku la Agano la Bwana na makuhani saba wachukue baragumu za pembe za kondoo dume mbele yake.” 76:7 Kut 14:15; Hes 10:35; 1Sam 4:3; 7:1Naye akawaagiza watu, “Songeni mbele! Mkauzunguke mji, na walinzi wenye silaha watangulie mbele ya Sanduku la Bwana.”

86:8 Yos 4:13Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba wenye kuzibeba zile baragumu saba mbele za Bwana, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano la Bwana likawafuata. 96:9 Hes 2:31; Isa 52:12, 13; Hes 10:25; Isa 42:11-13Walinzi waliokuwa na silaha wakaenda mbele ya hao makuhani waliopiga hizo baragumu na hao walinzi wa nyuma wakafuata Sanduku. Wakati wote huu baragumu zilikuwa zikipigwa. 106:10 1Sam 4:5; Ezr 3:11Bali Yoshua alikuwa amewaagiza watu, “Msipige kelele ya vita, msipaze sauti zenu, wala kusema neno lolote mpaka siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!” 11Basi akalipeleka Sanduku la Bwana kuzungushwa huo mji, likizungushwa mara moja. Kisha watu wakarudi kambini kulala.

126:12 Kum 31:25Yoshua akaamka mapema asubuhi iliyofuata nao makuhani wakalichukua Sanduku la Bwana. 136:13 1Nya 15:26; Gal 6:9Wale Makuhani saba wakizibeba zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la Bwana wakizipiga. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao na walinzi wa nyuma wakalifuata Sanduku la Bwana, huku baragumu hizo zikiendelea kulia. 14Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja na kurudi kambini. Wakafanya hivi kwa siku sita.

156:15 1Fal 18:44; 2Fal 4:35; 5:14Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakauzunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba. 166:16 Amu 7:20; 2Nya 14:14Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipopiga baragumu kwa sauti kubwa, Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maana Bwana amewapa mji huu! 176:17 Law 27:28; Kum 20:17; Isa 13:5; 24:1; 34:2-5; Mal 4:6; Yos 2:14; Mwa 13:3; 1Sam 15:6; Mt 10:41; 25:40; Ebr 6:10; 11:31; Yak 2:25Mji huu pamoja na vyote vilivyomo ndani yake utawekwa wakfu kwa Bwana. Ila Rahabu tu, yule kahaba na wote ambao wako pamoja naye nyumbani mwake ndio watakaosalimishwa, kwa sababu aliwaficha wale wapelelezi tuliowatuma. 186:18 Yos 7:1, 12, 25, 26; 1Nya 2:7; Kum 7:26; 13:17; Isa 52:11; Rum 12:9; 2Kor 6:17; Efe 5:11; 1The 5:2; 1Fal 18:17, 18Lakini mjiepushe na vitu vilivyowekwa wakfu, msije mkachukua chochote katika hivyo, msije mkajiletea maangamizi katika maskani ya Israeli na kuiletea taabu. 196:19 Hes 31:22Fedha yote na dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa Bwana, lazima viletwe katika hazina yake.”

206:20 Law 25:9; Amu 6:34; 7:22; 1Fal 1:41; Isa 18:3; Yer 4:21; 42:14; Amo 2:2; Ebr 11:30Wakati baragumu zilipopigwa, watu walipiga kelele, na katika sauti ya baragumu, na watu kupaza sauti, ukuta ukaanguka; hivyo kila mtu akapanda akiendelea mbele na kuuteka mji. 216:21 Kum 20:16; 1Sam 15:3, 8; 1Fal 20:42; Yer 48:18; Ufu 18:21Wakauweka mji wakfu kwa Bwana, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, ngʼombe, kondoo na punda.

226:22 Mwa 42:9; Yos 2:4; Hes 21:32; Yos 2:14; Ebr 11:30-31Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani kwa yule kahaba, mleteni pamoja na wote waliomo nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.” 236:23 Yos 2:13Basi wale vijana waliofanya upelelezi wakaenda kumleta Rahabu, baba yake na mama yake, na ndugu zake na watu wote waliokuwa pamoja naye. Wakaleta jamaa yake yote na kuwaweka mahali nje ya kambi ya Israeli.

246:24 Hes 31:10; Kum 13:16Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwamo ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na vya chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba ya Bwana. 256:25 Amu 1:25; Yos 2:1; 2:1, 6; Ebr 11:31Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu yule kahaba, jamaa yake yote na wote waliokuwa wa kwake, kwa sababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko, naye anaishi miongoni mwa Waisraeli hata leo.

266:26 1Sam 14:24; Hes 5:21; 1Fal 16:34Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Aliyelaaniwa mbele za Bwana ni mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko:

“Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume

ataiweka misingi yake;

kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho

atayaweka malango yake.”

276:27 Mwa 39:2; Hes 14:43; Yos 9:1; 1Nya 14:17; Amu 1:9; 2Sam 7:9; Rum 8:31; 1Sam 2:30Hivyo Bwana alikuwa pamoja na Yoshua, na sifa zake zikaenea katika nchi yote.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

约书亚记 6:1-27

耶利哥城塌陷

1因为害怕以色列人,耶利哥城门紧闭,无人出入。 2耶和华对约书亚说:“看啊,我已经把耶利哥及其王和英勇的战士都交在你手中了。 3所有军队要每天绕城一圈,连续六天, 4让七个祭司拿着七个羊角号走在约柜前面。到了第七天,你们要绕城七圈,祭司要吹响号角。 5当你们听到号角长鸣时,所有人都要高声呐喊,城墙就会坍塌,众人便可以直冲上去。” 6的儿子约书亚便召来祭司,对他们说:“你们抬起约柜,派七位祭司拿着七个羊角号走在耶和华的约柜前面。” 7他又对民众说:“你们要前去绕着城墙走,军队要走在耶和华的约柜前面。”

8约书亚吩咐完毕,七个祭司便在耶和华面前拿着羊角号边走边吹,耶和华的约柜就跟在他们后面, 9军队走在吹号的祭司前面,殿后军队跟在约柜后面。祭司一路上吹着号角。 10约书亚吩咐民众:“我哪天叫你们呐喊,你们再呐喊。在此之前,不许作声,一句话也不许说。” 11这样,约书亚让人抬着耶和华的约柜绕城一圈,然后众人各自回营过夜。

12第二天,约书亚一早起来,祭司又抬起耶和华的约柜。 13七个祭司拿着七个羊角号走在耶和华的约柜前面,一边走一边吹号。军队走在祭司前面,殿后军队跟在耶和华的约柜后面,伴随着持续不断的号角声。 14这一天他们又绕城一圈,然后各自回营。六天都是这样。

15第七天黎明时分,他们起来照样绕城,只是这一天他们绕城七次。 16绕到第七次,祭司吹响了号角,约书亚吩咐民众说:“呐喊吧!因为耶和华已经将这城交给你们了。 17要把这座城和城里所有的东西毁灭,作为献给耶和华之物。只有妓女喇合和她家中所有的人可以活命,因为她曾把我们派去的探子隐藏起来。 18你们要小心,不可私拿任何应当毁灭的东西,免得你们自取灭亡,并使以色列全营遭受灭顶之灾。 19所有金银和铜铁器皿都是耶和华的圣物,要放进耶和华的库房。” 20于是,民众呐喊,号角响起,当民众伴随着号角声高声呐喊时,城墙坍塌了。民众便一拥而上,占领了耶利哥城, 21用刀杀了城里所有的男女老少、牛羊和驴。

22约书亚对那两个探子说:“你们到那个妓女家里,照着你们向她起过的誓,把她和她的家人都带出来。” 23于是,那两个年轻探子便进去,把喇合和她的父母、兄弟及所有的亲人都带出来,安置在以色列人的营外。 24以色列人烧毁全城和城内的一切,只把金银和铜铁器皿放在耶和华的库房里。 25约书亚因为妓女喇合把两个派到耶利哥的探子隐藏起来,就饶了她和她一家人的性命。他们至今仍住在以色列人当中。

26之后,约书亚起誓说:

“重建耶利哥城的人必定在耶和华面前受咒诅,

他立地基的时候必死长子,

建城门的时候必丧幼子。”

27耶和华与约书亚同在,他的声名传遍整个地方。