Yeremia 6 – NEN & NVI

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 6:1-30

Yerusalemu Imezingirwa Na Jeshi

16:1 Yos 18:28; Neh 3:14; Yer 4:6; Hes 10:7; Yer 4:21; 2Nya 11:6“Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini!

Kimbieni kutoka Yerusalemu!

Pigeni tarumbeta katika Tekoa!

Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu!

Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini,

na uharibifu wa kutisha.

26:2 Za 9:14; Mao 4:5Nitamwangamiza Binti Sayuni,

aliye mzuri sana na mwororo.

36:3 Yer 12:10; 2Fal 25:4; Lk 19:43Wachungaji pamoja na makundi yao

watakuja dhidi yake;

watapiga mahema yao kumzunguka,

kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.”

46:4 Yer 15:8; 22:7“Jiandaeni kwa vita dhidi yake!

Inukeni tumshambulie mchana!

Lakini, ole wetu, mchana unaisha,

na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu.

5Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku,

na kuharibu ngome zake!”

66:6 Kum 20:19-20; 2Sam 20:15; Eze 26:6-8; Kum 28:33; Yer 25:38; Sef 3:1Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Kateni miti mjenge boma

kuzunguka Yerusalemu.

Mji huu ni lazima uadhibiwe,

umejazwa na uonevu.

76:7 Isa 58:4; Yer 20:8; Mik 7:2-3; Za 55:9-11Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake,

ndivyo anavyomwaga uovu wake.

Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake,

ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.

86:8 Eze 23:18; Hos 9:12Pokea onyo, ee Yerusalemu,

la sivyo nitageukia mbali nawe

na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa,

asiweze mtu kuishi ndani yake.”

9Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli

kwa uangalifu kama kwenye mzabibu;

pitisha mkono wako kwenye matawi tena,

kama yeye avunaye zabibu.”

106:10 Kut 6:12; Yer 15:10-15; Mdo 7:51; Yer 20:8; 7:13; 35:15; Isa 42:20Niseme na nani na kumpa onyo?

Ni nani atakayenisikiliza mimi?

Masikio yao yameziba,6:10 Masikio yameziba kwa Kiebrania ina maana kwamba masikio yao hayajatahiriwa.

kwa hiyo hawawezi kusikia.

Neno la Bwana ni chukizo kwao,

hawalifurahii.

116:11 Yer 7:20; Ay 32:20; 2Nya 36:17; Isa 40:30; Yer 15:17; Mao 2:21Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana,

nami siwezi kuizuia.

“Wamwagie watoto walioko barabarani,

na juu ya vijana waume waliokusanyika;

mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake,

hata nao wazee waliolemewa na miaka.

126:12 Kum 28:30; Yer 8:10; Mik 2:4; Yer 43:6; Sef 1:4; Eze 6:14; Yer 43:6; 38:22Nyumba zao zitapewa watu wengine,

pamoja na mashamba yao na wake zao,

nitakapounyoosha mkono wangu

dhidi ya wale waishio katika nchi,”

asema Bwana.

136:13 Isa 56:11; Yer 8:10; Mao 4:13; Yer 2:29“Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

wote wana tamaa ya kupata faida zaidi;

manabii na makuhani wanafanana,

wote wanafanya udanganyifu.

146:14 Eze 13:10; Isa 30:10; Yer 4; 10Wanafunga majeraha ya watu wangu

bila uangalifu.

Wanasema, ‘Amani, amani,’

wakati hakuna amani.

156:15 Mik 3:7; Zek 13:7; Yer 3:3; 8:10-12; 2Nya 25:16; Yer 27:15Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao

inayochukiza mno?

Hapana, hawana aibu hata kidogo;

hawajui hata kuona haya.

Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,

watashushwa chini nitakapowaadhibu,”

asema Bwana.

166:16 Yer 18:15; Lk 16:29; Yos 1:13; Mt 11:29; 1Fal 8:36; Isa 11:10Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Simama kwenye njia panda utazame,

ulizia mapito ya zamani,

ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo,

nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’

176:17 Yer 25:4; Isa 52:8; Eze 3:17; 33:4; Kut 20:18; Yer 11:7-8Niliweka walinzi juu yenu na kusema,

‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’

Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’

186:18 Mit 1:31; Eze 20:13; Kum 4:26; Amo 2:4; Yer 22:29; Yos 23:15; Yer 11:11; 29:19Kwa hiyo sikilizeni, enyi mataifa,

angalieni, enyi mashahidi,

lile litakalowatokea.

19Sikia, ee nchi:

Ninaleta maafa juu ya watu hawa,

matunda ya mipango yao,

kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu

na wameikataa sheria yangu.

206:20 Kut 30:23; Isa 60:6; Amo 5:22; Za 50:8-10; Hos 8:13; Mik 6:6-8; Mwa 10:7Unanifaa nini uvumba kutoka Sheba,

au udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?

Sadaka zako za kuteketezwa hazikubaliki,

dhabihu zako hazinifurahishi mimi.”

216:21 Isa 8:14; Ay 5:12; Yer 13:16; Law 26:37Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa.

Baba na wana wao watajikwaa juu yake,

majirani na marafiki wataangamia.”

226:22 Yer 4:6; Kum 28:49Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Tazama, jeshi linakuja

kutoka nchi ya kaskazini,

taifa kubwa linaamshwa

kutoka miisho ya dunia.

236:23 Isa 5:30; 13:18; Yer 4:29; Za 18:4; 93:3; Isa 10:32Wamejifunga pinde na mkuki,

ni wakatili na hawana huruma.

Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma

wanapoendesha farasi zao.

Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita

ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.”

246:24 Za 48:6; Yer 4:19, 31; 50:41-43; Isa 13:7Tumesikia taarifa zao,

nayo mikono yetu imelegea.

Uchungu umetushika,

maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

256:25 Ay 15:21; Za 31:13; Amo 5:6; Yer 49:29Usitoke kwenda mashambani

au kutembea barabarani,

kwa kuwa adui ana upanga,

na kuna vitisho kila upande.

266:26 Yer 4:8; Ay 2:8; Yon 3:6; Zek 12:10; Mwa 12:16; Yer 25:34; Eze 27:30; Kut 12:23Enyi watu wangu, vaeni magunia

mjivingirishe kwenye majivu,

ombolezeni kwa kilio cha uchungu

kama amliliaye mwana pekee,

kwa maana ghafula

mharabu atatujia.

276:27 Yer 9:7; Zek 13:9“Nimekufanya wewe kuwa kitu cha kujaribu chuma,

nao watu wangu kama mawe yenye madini,

ili upate kuzijua na kuzijaribu njia zao.

286:28 Yer 5:23; Eze 22:18; Yer 9:4; Law 19:16Wote ni waasi sugu,

wakienda huku na huko kusengenya.

Wao ni shaba na chuma,

wote wanatenda upotovu.

29Mivuo inavuma kwa nguvu,

kinachoungua kwa huo moto ni risasi,

lakini pamoja na kusafisha kote huku ni bure;

waovu hawaondolewi.

306:30 Za 53:5; Mao 5:22; Hos 9:17; Mit 17:3; Eze 22; 18; Yer 7:29Wanaitwa fedha iliyokataliwa,

kwa sababu Bwana amewakataa.”

Nueva Versión Internacional

Jeremías 6:1-30

Jerusalén es sitiada

1»¡Huyan a un lugar seguro, benjamitas!

¡Huyan de Jerusalén!

¡Toquen la trompeta en Tecoa!

¡Levanten señal en Bet Haqueren!

Porque una desgracia, una gran destrucción,

nos amenaza desde el norte.

2Estoy por destruir a Sión,

tan hermosa y delicada.

3Los pastores y sus rebaños vienen contra ella:

acampan a su alrededor,

y cada uno escoge su pastizal».

4«¡Prepárense para pelear contra ella!

¡Ataquémosla al mediodía!

Pero ¡ay de nosotros, que el día se acaba

porque se extienden las sombras del anochecer!

5¡Vamos, ataquémosla de noche

y destruyamos sus fortalezas!».

6Así dice el Señor de los Ejércitos:

«¡Talen árboles

y levanten una rampa contra Jerusalén!

Esta ciudad debe ser castigada,

pues en ella no hay más que opresión.

7Como un pozo que hace brotar agua,

así Jerusalén hace brotar su maldad.

En ella se oye de violencia y destrucción;

no veo otra cosa que enfermedades y heridas.

8¡Escarmienta, Jerusalén,

para que no me aparte de ti!

De lo contrario, te dejaré devastada,

en una tierra inhabitable».

9Así dice el Señor de los Ejércitos:

«Busquen al remanente de Israel.

Rebusquen, como en una viña;

repasen las ramas,

como lo hace el vendimiador».

10¿A quién hablaré?

¿A quién advertiré?

¿Quién podrá escucharme?

Tienen tapados6:10 tapados. Lit. incircuncisos. los oídos

y no pueden comprender.

La palabra del Señor los ofende;

no se complacen en ella.

11Pero yo estoy lleno de la ira del Señor,

y ya no puedo contenerme.

«Derrama tu ira en la calle sobre los niños,

sobre los grupos de jóvenes,

porque serán capturados el marido y la mujer,

la gente madura y la entrada en años.

12Sus casas, sus campos y sus mujeres

caerán en manos extrañas,

porque yo voy a extender mi mano

contra los habitantes del país»,

afirma el Señor.

13«Desde el más pequeño hasta el más grande,

todos codician ganancias injustas;

desde el profeta hasta el sacerdote,

todos practican el engaño.

14Curan por encima la herida de mi pueblo

y les desean: “¡Paz, paz!”,

cuando en realidad no hay paz.

15¿Acaso se han avergonzado de la abominación que han cometido?

¡No, no se han avergonzado de nada

y ni siquiera saben lo que es la vergüenza!

Por eso, caerán con los que caigan;

cuando los castigue, serán derribados»,

dice el Señor.

16Así dice el Señor:

«Deténganse en los caminos y miren;

pregunten por los senderos antiguos.

Pregunten por el buen camino,

¡y sigan por él!

Así hallarán el descanso anhelado.

Pero ellos dijeron:

“¡No lo seguiremos!”.

17Yo aposté centinelas para ustedes y dije:

“Presten atención al toque de trompeta”.

Pero ellos dijeron:

“No prestaremos atención”.

18Por eso, ¡escuchen, naciones!

¡Comunidad, conoce lo que te espera!

19Escucha, tierra:

Traigo sobre este pueblo una desgracia,

fruto de sus maquinaciones,

porque no prestaron atención a mis palabras,

sino que rechazaron mi Ley.

20¿De qué me sirve este incienso que llega de Sabá

o la caña dulce de un país lejano?

Sus holocaustos no me gustan;

sus sacrificios no me agradan».

21Por eso, así dice el Señor:

«Voy a ponerle obstáculos a este pueblo.

Padres e hijos tropezarán contra ellos,

vecinos y amigos perecerán».

22Así dice el Señor:

«¡Miren! Del norte viene un ejército;

una gran nación se moviliza

desde los confines de la tierra.

23Empuñan el arco y la lanza;

son crueles y no tienen compasión.

Lanzan gritos como bramidos del mar

y cabalgan sobre sus corceles.

¡Vienen contra ti, hija de Sión,

alineados para la batalla como un solo hombre!».

24Nos ha llegado la noticia

y nuestras manos flaquean;

la angustia nos domina,

como si tuviéramos dolores de parto.

25¡Viene el enemigo armado con espada!

No salgan al campo

ni transiten por los caminos.

¡Hay terror por todas partes!

26Vístete de luto, pueblo mío;

revuélcate en las cenizas.

Llora amargamente,

como lo harías por un hijo único,

porque nos cae por sorpresa

el que viene a destruirnos.

27«Te he puesto entre mi pueblo

como probador de metales y fortaleza,

para que escudriñes

y examines su conducta.

28Todos ellos son muy rebeldes

y andan sembrando calumnias;

sean de bronce o de hierro,

todos son unos corruptos.

29Los fuelles soplan con furor

y el plomo se derrite en el fuego,

pero los malvados no se purifican;

¡de nada sirve que se les refine!

30Por eso se les llama “Plata desechada”;

¡para el Señor son un desecho!».