Walawi 6 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 6:1-30

Kurudisha Kilichochukuliwa

1Bwana akamwambia Mose: 26:2 Hes 5:6; Za 73:27; Mdo 5:4; Kol 3:9; Law 19:11; Yer 9:4-5; Kut 22:7; Mwa 31:7; Mit 24:28“Kama mtu yeyote akitenda dhambi, naye si mwaminifu kwa Bwana kwa kumdanganya jirani yake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa, au kimeachwa chini ya utunzaji wake, au kimeibwa, au kama akimdanganya, 36:3 Kut 23:4; 22:11; Kum 22:1-3; Law 19:12; Yer 7:9; Zek 5:4au akiokota mali iliyopotea na akadanganya, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu waweza kuitenda; 46:4 Law 5:16; Eze 33:15; Lk 19:8wakati akitenda dhambi hizo na kuwa mwenye hatia, ni lazima arudishe kile alichokuwa amekiiba au amekichukua kwa dhuluma, au alichokuwa amekabidhiwa, au mali iliyokuwa imepotea akaipata, 56:5 Hes 5:7; Law 5:15; 2Sam 12:6; Lk 19:8au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia. 66:6 Law 5:15; Hes 5:8; Kut 12:5; Kum 15:21; Efe 5:27; Ebr 9:14; 10:1-17Kisha kama adhabu lazima amletee kuhani, yaani kwa Bwana, kama sadaka yake ya hatia, kondoo dume asiye na dosari na mwenye thamani kamili kutoka kundi lake. 76:7 Kut 32:30; Law 4:26Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana, naye atasamehewa kwa kosa lolote katika mambo hayo aliyoyatenda yaliyomfanya kuwa na hatia.”

Sadaka Ya Kuteketezwa

8Bwana akamwambia Mose: 96:9 Law 7:37“Mpe Aroni na wanawe agizo hili: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa itabaki kwenye moto juu ya madhabahu usiku kucha, mpaka asubuhi, nao moto lazima uwe unaendelea kuwaka juu ya madhabahu. 106:10 Kut 39:27, 28; 28:39-43; Law 1:16; Eze 44:17Kisha kuhani atavaa mavazi yake ya kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani mwilini wake, na aondoe majivu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo moto umeteketeza juu ya madhabahu, na kuyaweka kando ya madhabahu. 116:11 Law 4:12Kisha atayavua mavazi haya na kuvaa mengine, naye achukue yale majivu nje ya kambi na kuyapeleka mahali palipo safi kwa kawaida ya ibada. 126:12 Law 1:7; Kut 29:13; 32:6Moto ulio juu ya madhabahu lazima uwe unaendelea kuwaka, kamwe usizimike. Kila asubuhi kuhani ataongeza kuni na kupanga sadaka ya kuteketezwa juu ya moto, na kuteketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake. 136:13 Isa 33:14; Dan 7:10; Mt 25:41Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike.

Sadaka Ya Nafaka

146:14 Law 2:1; Hes 6:15; 15:4; 28:13“ ‘Haya ndiyo masharti ya sadaka ya nafaka: Wana wa Aroni wataileta mbele za Bwana, mbele za madhabahu. 156:15 Law 2:1, 9Kuhani atachukua konzi ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote ulioko juu ya sadaka ya nafaka, ateketeze sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 166:16 Law 2:2-3, 11; 8:31; 10:13; 16:24; 24:9; Eze 44:29; Kut 27:9; 29:11, 31; Hes 18:10Aroni na wanawe watakula sehemu iliyobaki, lakini italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu, nao wataila kwenye ua wa Hema la Kukutania. 176:17 Hes 5:9; 18:9-10; Kut 29:28; 40:10; Law 7:7; 10:12; 21:22Kamwe haitaokwa na chachu; nimewapa kama fungu lao la sadaka iliyotolewa kwangu kwa moto. Ni takatifu sana, kama vile ilivyo sadaka ya dhambi na ya hatia. 186:18 Law 2:3; 7:6; Hes 18:9-10; 5:9; Mwa 9:12; Kut 30:29Kila mwanaume mzao wa Aroni aweza kuila. Ni fungu lake la kawaida la sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto kwa vizazi vijavyo. Chochote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”

19Tena Bwana akamwambia Mose, 206:20 Kut 28:41; 16:36; 29:2; Hes 4:16; 5:15; 28:5; Law 23:13“Hii ni sadaka ambayo Aroni na wanawe wanapaswa kuleta kwa Bwana siku atakapotiwa mafuta: sehemu ya kumi ya efa6:20 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja. ya unga laini kama sadaka ya kawaida ya nafaka. Nusu yake ataitoa asubuhi na nusu nyingine jioni. 216:21 Law 2:5; 6:22; Kut 28:41; 29:30; Law 1:9; Isa 53:10; Mt 20:28; Dan 9:26Iandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri, na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 22Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyetiwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la kawaida la Bwana, nalo litateketezwa kabisa. 23Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itateketezwa kabisa; kamwe haitaliwa.”

Sadaka Ya Dhambi

24Bwana akamwambia Mose, 256:25 Kut 29:11; 30:10; Law 4:24; 1:3; Za 93:5“Mwambie Aroni na wanawe: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjiwa mbele za Bwana mahali sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, ni takatifu sana. 266:26 Kut 27:9, 21; 40:2; Hes 18:9; Eze 44:27-28Kuhani anayeitoa ndiye atakayeikula; itakuliwa katika mahali patakatifu, katika ua wa Hema la Kukutania. 276:27 Kut 29:37; Law 10:10; Eze 44:19; 46:20; Hag 2:12Chochote kitakachogusa nyama yoyote ya hiyo sadaka kitakuwa kitakatifu, na kama hiyo damu itadondokea juu ya vazi, lazima uifulie mahali patakatifu. 286:28 Law 11:33; 15:12; Hes 19:15Chungu cha udongo kitakachopikiwa nyama lazima kivunjwe, lakini kama imepikiwa kwenye chombo cha shaba, chombo hicho kitasuguliwa na kusuuzwa kwa maji. 296:29 Eze 42:13Kila mwanaume katika familia ya kuhani aweza kula nyama hiyo; ni takatifu sana. 306:30 Eze 45:15; Law 4:12, 18; 16:27; Ebr 13:11Lakini kila sadaka ya dhambi ambayo damu yake imeletwa ndani ya Hema la Kukutania kufanya upatanisho katika Mahali Patakatifu kamwe haitaliwa; lazima iteketezwe.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

利未記 6:1-30

1耶和華對摩西說: 2-3「如果有人拒絕歸還同胞委託他保管的物品或抵押品,或搶掠同胞,或欺騙同胞,或撿到失物卻矢口否認,或起假誓,或犯其他類似的罪,因而失信於耶和華, 4一旦他意識到自己犯了罪,必須歸還一切靠偷盜、欺詐、侵佔、拾遺、 5或起假誓得來的東西,他必須在獻贖過祭那天如數歸還物主,並加賠五分之一。 6他要從羊群中選一隻毫無殘疾的公綿羊,或把同等價值的銀子帶到祭司那裡,獻給耶和華作贖過祭。 7祭司要在耶和華面前為他贖罪,他的過犯就會得到赦免。」

祭司獻燔祭的條例

8耶和華對摩西說: 9「你要吩咐亞倫及其子孫遵行以下獻燔祭的條例。

「燔祭要整夜留在祭壇上,壇上的火要不停地燃燒。 10早晨,祭司要穿上細麻衣袍和內衣,將燔祭壇上的灰燼清理好,放在祭壇旁邊。 11然後,他要更換衣服,把灰燼拿到營外潔淨的地方。 12祭壇上的火要不斷燃燒,不能熄滅。祭司每天早上要在壇上加柴,擺上燔祭,在上面燒平安祭牲的脂肪。 13壇上的火必須不斷燃燒,不可熄滅。

祭司獻素祭的條例

14「以下是獻素祭的條例。

亞倫的子孫要在祭壇前向耶和華獻素祭。 15祭司要從素祭中拿一把調油的細麵粉和所有的乳香,作為象徵放在壇上焚燒,作蒙耶和華悅納的馨香之祭。 16亞倫及其子孫要吃剩下的祭物,要在會幕院子裡的聖潔之處做無酵餅吃。 17做餅時不可加酵。這些祭物是我從獻給我的火祭中賜給他們的,像贖罪祭和贖過祭一樣是至聖之物。 18亞倫的子孫中,男子都可以吃耶和華的火祭。這是他們世世代代應得之份。凡接觸到這些祭物的都會變得聖潔。」

19耶和華對摩西說: 20亞倫及其子孫受膏那天,要獻給耶和華一公斤細麵粉作為日常獻的素祭,早晚各獻一半。 21要把這些細麵粉調上油,用煎鍋做餅,切成塊獻上,作為蒙耶和華悅納的馨香素祭。 22亞倫子孫中繼任大祭司的,受膏時要獻上素祭。這種祭物必須全部燒掉獻給耶和華,這是永遠的律例。 23祭司獻的這種素祭不可吃,要全部燒掉。」

祭司獻贖罪祭的條例

24耶和華對摩西說: 25「你把以下贖罪祭的條例告訴亞倫及其子孫。

「贖罪祭是至聖的,要在殺燔祭牲的地方,在耶和華面前宰祭牲。 26獻贖罪祭的祭司要在會幕院子裡的聖潔之處吃這祭牲。 27凡接觸到這些祭肉的,都會變得聖潔。如果衣服被濺上血,則要在聖潔之處把衣服洗淨。 28用來煮祭肉的瓦鍋,用後都要打碎。如果用的是銅鍋,要擦乾淨並用水沖洗。 29這些祭肉是至聖之物,祭司家族中的男子都可以吃。 30如果贖罪祭牲的血被帶進會幕,在聖所內進行贖罪,就不可吃祭肉,必須全部燒掉。