Waamuzi 15 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 15:1-20

Kisasi Cha Samsoni Kwa Wafilisti

115:1 Mwa 30:14; Amu 13:24; Mwa 38:17; 29:21Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia.

215:2 Amu 14:20Huyo baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimkataa, hivyo mimi nikampa rafiki yako. Je, mdogo wake wa kike si mzuri zaidi kuliko yeye? Mchukue huyo badala yake.”

3Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.” 415:4 Wim 2:15; Mwa 15:17Hivyo Samsoni akatoka akawakamata mbweha 300 na kuwafunga wawili wawili kwa mikia yao kila mmoja kwa mwingine. Kisha akafungia mwenge wa moto, kwenye mikia ya kila jozi moja ya mbweha aliyokuwa ameifunga, 515:5 Mwa 15:17; Kut 22:6; 2Sam 14:30-31akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka zilizosimama, pamoja na mashamba ya mizabibu na viunga vya mizeituni.

615:6 Amu 14:20; Mwa 38:24; Amu 14:15Ndipo Wafilisti wakauliza, “Ni nani aliyetenda jambo hili?” Wakaambiwa, “Ni Samsoni, yule mkwewe Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake.”

Hivyo Wafilisti wakapanda wakamteketeza kwa moto yeye huyo mwanamke pamoja na baba yake. 7Samsoni akawaambia, “Kwa kuwa mmetenda hivyo, hakika sitatulia mpaka niwe nimelipiza kisasi juu yenu.” 815:8 Isa 2:21Akawashambulia kwa ukali kwa mapigo makuu na kuwaua watu wengi sana. Kisha akateremka na kukaa katika ufa kwenye mwamba wa Etamu.

9Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi. 10Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?”

Wakawajibu, “Tumekuja ili kumkamata Samsoni na kumtenda kama alivyotutendea.”

1115:11 Amu 13:1; 14:4; Za 106:40-42Ndipo watu 3,000 toka Yuda walipoteremka na kwenda kwenye ufa wa mwamba huko Etamu, na kumwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?”

Akawajibu, “Mimi nimewatendea tu kile walichonitendea.”

1215:12 Mwa 47:31Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.”

Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.”

1315:13 Amu 16:11-12Wakamjibu, “Sisi hatutakuua, bali tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya. Wakamchukua toka huko kwenye ufa katika mwamba. 1415:14 Amu 3:10; Yos 2:6; Amu 14:19; 1Sam 11:6Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Bwana akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. 1515:15 Law 26:8; Yos 23:10Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao 1,000.

1615:16 Yer 22:19Ndipo Samsoni akasema,

“Kwa taya la punda

malundo juu ya malundo.

Kwa taya la punda

nimeua watu 1,000.”

17Alipomaliza kusema, akautupa ule mfupa wa taya; na mahali pale pakaitwa Ramath-Lehi.15:17 Ramath-Lehi maana yake Kilima cha Taya.

1815:18 Amu 16:28; Kum 20:4Kwa kuwa alikuwa amesikia kiu sana, akamlilia Bwana akisema, “Umempa mtumishi wako ushindi huu mkuu. Je, sasa nife kwa kiu na kuangukia mikononi mwa hawa watu wasiotahiriwa?” 1915:19 Mwa 45:27; 1Sam 30:12; Isa 40:29; Kut 17:6Bwana akafunua shimo huko Lehi, pakatoka maji. Samsoni alipoyanywa, nguvu zikamrudia na kuhuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore,15:19 En-Hakore maana yake ni Chemchemi ya Aliyeita. nayo iko mpaka leo huko Lehi.

2015:20 Amu 13:1; 16:31; Ebr 11:32Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

士师记 15:1-20

参孙向非利士人报仇

1过了些日子,在割麦的时候,参孙带着一只山羊羔去探望他妻子。他说:“我要进内室见我妻子。”他岳父却不让他进去, 2并对他说:“我以为你非常恨她,所以我把她改嫁给你的伴郎了。她妹子不是比她更美吗?你可以娶来代替她。”

3参孙说:“这次我要加害非利士人,可不能怪我了。”

4于是,他出去捉了三百只狐狸,把它们的尾巴一对一对绑起来,将火把绑在两条尾巴中间, 5然后点燃火把,把狐狸放进非利士人的麦田里,将割好的麦捆和未割的麦子、葡萄园和橄榄园都烧毁了。 6非利士人问:“这是谁干的?”有人回答说:“是亭拿人的女婿参孙干的,因为他岳父把他的妻子嫁给了他的伴郎。”非利士人就去放火烧死了参孙的妻子和岳父。 7参孙说:“你们既然这样做,我不向你们报仇誓不罢休。” 8参孙大肆击杀他们,杀死了很多人。事后,他下到以坦,住在那里的岩洞里。

9非利士人进犯犹大,在利希一带扎营。 10犹大人问他们:“你们为什么来攻打我们?”非利士人回答说:“我们来捉拿参孙,向他以报还报。” 11于是,有三千犹大人去以坦的岩洞找参孙,对他说:“难道你不知道非利士人是我们的统治者吗?你为什么连累我们?”参孙回答说:“我只是以牙还牙。” 12犹大人说:“我们来是要捉拿你,把你交给非利士人。”参孙说:“你们要起誓不会亲手杀我。” 13他们说:“我们不会杀你,只将你绑起来交给非利士人。”于是,他们用两根新绳子把参孙捆绑起来带出岩洞。

14参孙来到利希非利士人就呐喊着迎了上去。耶和华的灵突然降在参孙身上,绑在他手臂上的绳子就像被火烧的麻线一样脱落下来。 15他看到一块还没有干的驴腮骨,就捡起来用它杀了一千个非利士人。 16参孙说:

“用这驴腮骨,我杀人成堆;

用这驴腮骨,我杀死千人。”

17说完,他扔掉了手中的驴腮骨。因此,那地方叫拉末·利希15:17 “拉末·利希”意思是“腮骨岗”。

18参孙觉得非常口渴,便向耶和华呼求说:“你既然借着仆人的手大败敌人,难道你会让我渴死、落在这些未受割礼的人手中吗?” 19于是,上帝使利希的一处洼地裂开,涌出水来。参孙喝后恢复了精神。因此,那水泉叫隐·哈歌利15:19 “隐·哈歌利”意思是“呼求者的泉”。。那水泉今天还在利希20非利士人统治期间,参孙以色列的士师二十年。