Ufunuo 16 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 16:1-21

Mabakuli Saba Ya Ghadhabu Ya Mungu

116:1 Ufu 15:1; 11:19; 15:1; 16:2-21; Za 79:6; Sef 3:8Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mle Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, “Nendeni, mkayamwage duniani hayo mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”

216:2 Ufu 8:7; 13:15; 17; Kut 9:9-11Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.

316:3 Kut 7:17-21; Ufu 6:11Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.

416:4 Ufu 8:10Malaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu. 516:5 Ufu 15:3-4; 15:3; 1:4; 15:4; 6:10Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema:

“Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa,

wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu,

kwa sababu umehukumu hivyo;

616:6 Isa 49:26kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako

na manabii wako,

nawe umewapa damu wanywe

kama walivyostahili.”

716:7 Ufu 9:6; 15:3; 19:2Nikasikia madhabahu ikiitikia,

“Naam, Bwana Mungu Mwenyezi,

hukumu zako ni kweli na haki.”

816:8 Ufu 8:12; 14:18Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto. 916:9 Ufu 2:21; 11:13Watu wakaunguzwa na hilo joto kali, wakalaani Jina la Mungu, aliyekuwa na uwezo juu ya mapigo haya, tena wakakataa kutubu na kumtukuza Mungu.

1016:10 Ufu 13:2; 9:2Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha enzi cha yule mnyama, nao ufalme wake ukagubikwa na giza. Watu wakatafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu, 1116:11 Ufu 11:13; 2:21; 16:9, 21wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu na majeraha yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.

1216:12 Ufu 9:14; Isa 41:2Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Frati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme watokao Mashariki. 1316:13 Ufu 12:3; 13:1; 19:20Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 1416:14 1Tim 4:1; Ufu 17:14Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.

1516:15 Lk 12:3“Tazama, naja kama mwizi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.”

1616:16 Ufu 9:11; Amu 5:19Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo Armagedoni16:16 Armagedoni au Har-Magedoni ina maana Mlima Megido, mahali pa kinabii ambapo wafalme wote wa dunia watakusanyika kwa vita katika siku ya Mungu Mwenyezi. kwa Kiebrania.

1716:17 Efe 2:2; Ufu 14:15; 11:15; 21:6Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!” 1816:18 Ufu 4:5; 6:12; Dan 12:1Kukawa na mianga ya umeme wa radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawa kamwe na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, hivyo lilikuwa tetemeko kubwa ajabu. 1916:19 Ufu 17:18; 18:5; 14:8Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akaukumbuka Babeli Mkuu na kumpa kikombe kilichojaa mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake. 2016:20 Ufu 6:14Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana. 2116:21 Eze 13:13; Kut 9:23-25Mvua kubwa ya mawe yenye uzito wa talanta moja16:21 Talanta moja ni kama kilo 34. ikashuka kutoka mbinguni, ikawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

启示录 16:1-21

1我听见殿中有宏亮的声音对七位天使说:“去将那盛满上帝烈怒的七个碗倾倒在地上。”

2第一位天使去将碗倒在了地上,那些有怪兽的印记、敬拜兽像的人身上长出可怕的毒疮。

3第二位天使将碗倒在了海洋里,海水变得像死人的血,海中的活物都死光了。

4第三位天使将碗倒在了江河与水泉里,水就变成了血。 5我听见掌管众水的天使说:

“昔在今在的圣者啊!

你是公义的,

因为你施行了审判。

6他们流了众圣徒和先知们的血,

所以你使他们喝血,

这正是他们应得的报应。”

7我又听见从祭坛发出的声音说:

“是的,全能的主上帝,

你的判决真实公义。”

8第四位天使将碗倒在太阳上,使太阳可以用它的火炙烤世人。 9世人被高温炙烤,就亵渎掌管这些灾祸的上帝的名,他们毫无悔意,不肯归荣耀给上帝。

10第五位天使将碗倒在怪兽的座位上,它的国便被黑暗笼罩,它的国民痛苦不堪,咬自己的舌头。 11他们因为痛苦和毒疮就亵渎天上的上帝,不肯为自己的所作所为悔改。

12第六位天使将碗倒在幼发拉底大河上,河水就干了,为东方各国的王预备了道路。 13我又看见三个像青蛙一样的污鬼分别从巨龙、怪兽和假先知的口里跳出来。 14它们都是鬼魔的灵,能行奇迹。它们到普天下召集各王,预备在全能上帝的大日子争战。

15“看啊!我来的时候像贼一样。那警醒等候,穿好衣裳的人有福了!他们不会赤身行走,在人前蒙羞。”

16三个污鬼把众王召集到一个希伯来话叫哈米吉多顿的地方。

17第七位天使将碗倒在空中时,从殿里的宝座上传出响亮的声音说:“成了!” 18随后雷电交加,伴随着巨响,还有空前剧烈的大地震。 19巴比伦大城裂作三段,其他各国的城邑也都倒塌了。上帝并没有忘记巴比伦大城的罪恶,要把那杯盛满祂烈怒的酒给她喝。 20海岛都沉没了,山岭也都不见了, 21又有四十公斤重的巨型冰雹从天而降,打在世人身上。世人因为可怕的雹灾,就亵渎上帝。