Sefania 3:1-20
Hatima Ya Yerusalemu
13:1 Yer 6:6; Kum 21:18; Eze 23:30Ole mji wa wadhalimu,
waasi na waliotiwa unajisi!
23:2 Yer 5:3; 7:28; 22:21; Kum 1:32; Law 26:33; Za 78:23Hautii mtu yeyote,
haukubali maonyo.
Haumtumaini Bwana,
haukaribii karibu na Mungu wake.
33:3 Za 22:13; Mwa 49:27; Mik 3:3Maafisa wake ni simba wangurumao,
watawala wake ni mbwa mwitu wa jioni,
ambao hawabakizi chochote
kwa ajili ya asubuhi.
43:4 Za 25:3; Isa 48:8; Yer 3:20; 9:4; 23:11; Mal 2:10; Eze 22:26Manabii wake ni wenye kiburi,
ni wadanganyifu.
Makuhani wake hunajisi patakatifu
na kuihalifu sheria.
53:5 Ezr 9:15; Kum 32:4; Za 5:3; 99:3, 4; Mao 3:23; Yer 3:3; Eze 18:25Bwana aliye ndani yake ni mwenye haki,
hafanyi kosa.
Asubuhi kwa asubuhi hutoa haki yake,
kila kukipambazuka huitimiza,
bali mtu dhalimu hana aibu.
63:6 Law 26:31“Nimeyafutilia mbali mataifa,
ngome zao zimebomolewa.
Nimeziacha barabara ukiwa,
hakuna anayepita humo.
Miji yao imeharibiwa;
hakuna mmoja atakayeachwa:
hakuna hata mmoja.
73:7 Yer 7:28; Mwa 6:12; Hos 9:9Niliuambia huo mji,
‘Hakika utaniogopa na kukubali maonyo!’
Ndipo makao yake hayatafutiliwa mbali,
wala adhabu zangu zote hazitakuja juu yake.
Lakini walikuwa bado na shauku
kutenda kwa upotovu katika yote waliyofanya.”
83:8 Za 27:14; 79:6; Yoe 3:2; 3:11; Isa 2:3; Mit 20:22; Ufu 16:1; Yer 10:25; Mao 4:11; Sef 1:18Bwana anasema,
“Kwa hiyo ningojee mimi,
siku nitakayosimama kuteka nyara.
Nimeamua kukusanya mataifa,
kukusanya falme
na kumimina ghadhabu yangu juu yao,
hasira yangu kali yote.
Dunia yote itateketezwa
kwa moto wa wivu wa hasira yangu.
93:9 Sef 2:11; Mwa 4:26; Isa 19:18“Ndipo nitatakasa midomo ya mataifa,
kwamba wote waweze kuliitia jina la Bwana
na kumtumikia kwa pamoja.
103:10 Mwa 10:6; Za 68:31; Mal 1:11; Isa 60:7; Mdo 8:27; 2Nya 32:23Kutoka ngʼambo ya mito ya Kushi
watu wangu wanaoniabudu,
watu wangu waliotawanyika,
wataniletea sadaka.
113:11 Isa 29:22; Yoe 2:26-27; Mwa 50:15; Kut 15:17; Za 59:12; Mt 3:9; Law 26:19Siku hiyo hutaaibishwa
kwa ajili ya makosa yote ulionitendea,
kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu
wale wote wanaoshangilia
katika kiburi chao.
Kamwe hutajivuna tena
katika kilima changu kitakatifu.
123:12 Isa 14:32; Mt 5:3; Lk 6:20; Isa 57:15; Yer 29:12; Nah 1:7Lakini nitakuachia ndani yako
wapole na wanyenyekevu,
ambao wanatumaini jina la Bwana.
133:13 Isa 4:3; 10:21; Za 119:3; Yer 33:16; Ufu 14:5; Ay 16:17; Eze 34:25-28Mabaki ya Israeli hayatafanya kosa;
hawatasema uongo,
wala udanganyifu hautakuwa
katika vinywa vyao.
Watakula na kulala
wala hakuna yeyote
atakayewaogopesha.”
143:14 Za 9:14; 14:7; Zek 2:10; Isa 12:6; 51:11Imba, ee Binti Sayuni;
paza sauti, ee Israeli!
Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote,
ee Binti Yerusalemu!
153:15 Yn 1:49; Eze 37:26-28; 48:35; Ufu 21:3; Isa 54:14; Zek 9:9Bwana amekuondolea adhabu yako,
amewarudisha nyuma adui zako.
Bwana, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe;
kamwe hutaogopa tena madhara yoyote.
163:16 2Fal 19:26; Ebr 12:12; Ay 4:3; Isa 35:3-4Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu,
“Usiogope, ee Sayuni;
usiiache mikono yako ilegee.
173:17 Isa 40:1; 62:4; 63:1; Yoe 2:21; Kum 28:63; Hos 14:4Bwana Mungu wako yu pamoja nawe,
yeye ni mwenye nguvu kuokoa.
Atakufurahia kwa furaha kubwa,
atakutuliza kwa pendo lake,
atakufurahia kwa kuimba.”
183:18 Mao 2:6“Huzuni katika sikukuu zilizoamriwa
nitaziondoa kwenu;
hizo ni mzigo na fedheha kwenu.
193:19 Isa 14:2; 60:18; Eze 34:16; Mik 4:6Wakati huo nitawashughulikia
wote waliokudhulumu;
nitaokoa vilema na kukusanya
wale ambao wametawanywa.
Nitawapa sifa na heshima
katika kila nchi ambayo waliaibishwa.
203:20 Yer 29:14; Eze 37:12; Za 22:27; Isa 56:5; 60:18; 66:22; Kum 26:19Wakati huo nitawakusanya;
wakati huo nitawaleta nyumbani.
Nitawapa sifa na heshima
miongoni mwa mataifa yote ya dunia
wakati nitakapowarudishia mateka yenu
mbele ya macho yenu hasa,”
asema Bwana.