Onyo Dhidi Ya Mwanamke Mzinzi
17:1 Mt 1:8Mwanangu, shika maneno yangu
na kuzihifadhi amri zangu ndani yako.
27:2 Mit 4:4; Law 18:5; Kum 32:10Shika amri zangu nawe utaishi;
linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
37:3 Kum 6:8; Mit 3:3; Isa 30:8; 2Kor 3:3Yafunge katika vidole vyako;
yaandike katika kibao cha moyo wako.
4Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,”
uite ufahamu jamaa yako;
57:5 Ay 31:9; Mit 2:16watakuepusha na mwanamke mzinzi,
kutokana na mwanamke mpotovu
na maneno yake ya kubembeleza.
6Kwenye dirisha la nyumba yangu
nilitazama nje kupitia upenyo
kwenye mwimo wa dirisha.
77:7 Mit 6:32Niliona miongoni mwa wajinga,
nikagundua miongoni mwa wanaume vijana,
kijana asiye na akili.
8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake,
akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
97:9 Ay 24:15wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake,
giza la usiku lilipokuwa likiingia.
107:10 1Tim 2:9Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki,
hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
117:11 Mit 9:13; 1Tim 5:13(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi,
miguu yake haitulii nyumbani;
127:12 Mit 8:1-36; 23:26-28mara kwenye barabara za mji,
mara kwenye viwanja vikubwa,
kwenye kila pembe huvizia.)
137:13 Mwa 39:12; Mit 1:20Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu,
na kwa uso usio na haya akamwambia:
147:14 Law 7:11-18“Nina sadaka za amani nyumbani;
leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki;
nimekutafuta na nimekupata!
167:16 Isa 19:9Nimetandika kitanda changu
kwa kitani za rangi kutoka Misri.
177:17 Amo 6:4; Mwa 37:25Nimetia manukato kitanda changu
kwa manemane, udi na mdalasini.
187:18 Mwa 39:7Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi;
tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19Mume wangu hayupo nyumbani;
amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha
na hatakuwepo nyumbani karibuni.”
217:21 Mit 1:8-9; 8:32Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha;
alimshawishi kwa maneno yake laini.
227:22 Ay 18:10Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke
kama fahali aendaye machinjoni,
kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
237:23 Ay 15:22; 16:13; Mit 6:26; Mhu 9:12mpaka mshale umchome ini lake,
kama ndege anayenaswa kwenye mtego,
bila kujua itamgharimu maisha yake.
247:24 Mit 1:8-9; 8:32Sasa basi wanangu, nisikilizeni;
sikilizeni kwa makini nisemalo.
257:25 Mit 5:7-8Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke,
wala usitangetange katika mapito yake.
267:26 Neh 13:26Aliowaangusha ni wengi;
aliowachinja ni kundi kubwa.
277:27 Amu 16:19; Ufu 22:15Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini,7:27 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.