Onyo Dhidi Ya Uzinzi
15:1 Mit 1:8Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu,
sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,
25:2 Mwa 2:7ili uweze kutunza busara
na midomo yako ihifadhi maarifa.
35:3 Za 55:21; Mit 2:16Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba
hudondoza asali,
na maneno ya kinywa chake
ni laini kuliko mafuta;
45:4 Mhu 7:26; Ebr 4:12lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,
mkali kama upanga ukatao kuwili.
55:5 Za 9:17; Mit 2:18Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;
hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.5:5 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
65:6 Mit 9:13; 30:20Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima;
njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.
75:7 Mit 1:8-9Sasa basi wanangu, nisikilizeni;
msiache ninalowaambia.
85:8 Mit 6:20-29; 7:1-27Njia zenu ziwe mbali naye,
msiende karibu na mlango wa nyumba yake,
9usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine
na miaka yako kwa aliye mkatili,
105:10 Mit 29:3wageni wasije wakasherehekea utajiri wako
na jitihada yako ikatajirisha
nyumba ya mwanaume mwingine.
11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,
wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!
Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!
13Sikuwatii walimu wangu
wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
145:14 Mit 1:24-27; 6:33; 31:3Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa
katikati ya kusanyiko lote.”
15Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe,
maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.
16Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji
na vijito vyako vya maji viwanjani?
17Na viwe vyako mwenyewe,
kamwe visishirikishwe wageni.
185:18 Wim 4:12-15; Kum 20:7; Mal 2:14Chemchemi yako na ibarikiwe
na umfurahie mke wa ujana wako.
195:19 Wim 2:9; 8:14Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri:
matiti yake na yakutosheleze siku zote,
nawe utekwe daima na upendo wake.
205:20 Mit 2:16; 7:5Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba?
Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?
215:21 Za 119:168; Hos 7:2; Yer 16:17; Ay 10:4; Ebr 4:13Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana,
naye huyapima mapito yake yote.
225:22 Za 9:16; Hes 32:23; Ay 18:9Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe;
kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.
235:23 Ay 4:21; 36:12Atakufa kwa kukosa nidhamu,
akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.