129:1 2Nya 36:16; Mit 6:15Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi,
ataangamia ghafula, wala hapati dawa.
229:2 2Fal 11:20; Es 8:15; Mit 28:12Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi;
waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
329:3 1Fal 1:48; Mit 10:1; 23:15-16; 5:8-10; Lk 15:11-32Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake,
bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
429:4 Mit 8:15-16Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti,
bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
529:5 Ay 32:21; Mit 26:28Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili,
anautandaza wavu kuitega miguu yake.
629:6 Ay 5:13; Mhu 9:12Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe
bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.
729:7 Ay 29:16; Za 41:1; Isa 35:3-4Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini,
bali mwovu hajishughulishi na hilo.
829:8 Mit 11:11; 16:14Wenye mzaha huuchochea mji,
bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.
929:9 Mt 11:17Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu,
mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
1029:10 Mwa 4:5-8; 1Yn 3:12Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu
na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
1129:11 Ay 15:13; Mit 12:16Mpumbavu huonyesha hasira yake yote,
bali mwenye hekima hujizuia.
1229:12 2Fal 21:9; Ay 34:30Kama mtawala akisikiliza uongo,
maafisa wake wote huwa waovu.
1329:13 Mit 22:2; Mt 5:45Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili:
Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.
1429:14 Mit 29:4; Za 72:1-5; Mit 16:12Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki,
kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
1529:15 Mit 29:17; 13:24Fimbo ya maonyo hutia hekima,
bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo
humwaibisha mama yake.
1629:16 Za 37:36; 58:10; 91:8Wakati waovu wanapostawi,
pia dhambi vivyo hivyo,
lakini wenye haki wataliona anguko lao.
1729:17 Mit 13:24; 29:15Mrudi mwanao, naye atakupa amani,
atakufurahisha nafsi yako.
1829:18 Za 19:11; Yn 13:17; Amo 8:11-12; 1Sam 3:1Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia,
bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
19Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu,
ajapoelewa, hataitikia.
2029:20 Mit 14:17Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka?
Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.
21Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani,
atamletea sikitiko mwishoni.
2229:22 Mit 14:17Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi,
naye mtu mwenye hasira ya haraka
hutenda dhambi nyingi.
2329:23 Isa 66:2; Mt 23:12; Yak 4:6Kiburi cha mtu humshusha,
bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu
hupata heshima.
2429:24 Law 5:1Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe;
huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.
2529:25 1Sam 15:24; Mit 28:25; 16:20Kuwaogopa watu huwa ni mtego,
bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.
2629:26 Mit 19:6; 16:33Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala,
bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.
2729:27 Mit 29:10Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu;
waovu huwachukia sana wenye haki.