121:1 Es 5:1; Yer 39:11-12Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana;
huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo.
221:2 Mit 24:12; Lk 16:15; Yer 17:10; 1Sam 16:7Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake,
bali Bwana huupima moyo.
321:3 Hos 6:6; Mik 6:6-8Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika
zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.
421:4 Ay 41:34; Mit 6:17Macho ya kudharau na moyo wa kiburi,
ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!
521:5 Mit 10:4Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida,
kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.
621:6 Mit 10:2; 2Pet 2:3Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo
ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.
721:7 Mit 11:5Jeuri ya waovu itawaburuta mbali,
kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa.
821:8 Mit 2:15Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu,
bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu.
921:9 Mit 21:19; 19:13; 25:24Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba,
kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.
1021:10 Yak 4:5Mtu mwovu hutamani sana ubaya,
jirani yake hapati huruma kutoka kwake.
1121:11 Mit 19:25Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa,
mjinga hupata hekima;
wakati mtu mwenye hekima afundishwapo,
hupata maarifa.
1221:12 1Kor 10:10; Rum 2:8; Mit 14:11Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu,
naye atawaangamiza waovu.
1321:13 Ay 29:12; Zek 7:11; Mdo 7:57; Yak 2:13Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini,
yeye pia atalia, wala hatajibiwa.
1421:14 Mwa 32:20; Mit 18:16Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira
na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali.
1521:15 Mit 21:9Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki,
bali kitisho kwa watenda mabaya.
1621:16 Za 49:14; Eze 18:24Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu,
hupumzika katika kundi la waliokufa.
1721:17 Mit 23:20-21, 29-35Mtu apendaye anasa atakuwa maskini,
yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri.
1821:18 Isa 43:3-4; Mit 11:8Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki,
nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu.
1921:19 Mit 21:9Ni afadhali kuishi jangwani
kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.
2021:20 Za 112:3; Mit 10:22; Mt 25:3Katika nyumba ya mwenye hekima
kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta,
lakini mtu mpumbavu
hutafuna vyote alivyo navyo.
2121:21 1Kor 15:58; Za 25:13; Mt 5:6Yeye afuatiaye haki na upendo
hupata uzima, mafanikio na heshima.
2221:22 Mit 8:14; Mhu 9:15-16Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu,
na kuangusha ngome wanazozitegemea.
2321:23 Za 34:13; Yak 3:2; Mit 12:13Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake
hujilinda na maafa.
2421:24 Yer 43:2Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake;
hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.
2521:25 Mit 13:4Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake,
kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.
2621:26 Law 25:35; Mt 5:42Mchana kutwa hutamani zaidi,
lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.
2721:27 1Fal 14:24; Amo 5:22; Mit 15:8Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo,
si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya!
2821:28 Isa 29:21; Mit 19:5Shahidi wa uongo ataangamia,
bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu.
2921:29 Mit 14:8Mtu mwovu ana uso wa ushupavu,
bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake.
3021:30 Ay 12:13; Yer 9:23; 2Nya 13:12; Mdo 5:39Hakuna hekima, wala akili, wala mpango
unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.
3121:31 Isa 31:1; Za 3:8Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita,
bali ushindi huwa kwa Bwana.