111:1 Law 19:36; Ay 6:2; Mit 16:11; Eze 45:10Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,
bali vipimo sahihi ni furaha yake.
211:2 Dan 4:30; Mit 16:18; 18:12Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,
bali unyenyekevu huja na hekima.
311:3 Mit 13:6Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,
bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
411:4 Ay 20:20; Eze 7:19; Sef 1:18Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu,
bali haki huokoa kutoka mautini.
511:5 1Fal 8:36; Mit 5:21-23; 13:6; 21:7Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka,
bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
611:6 Es 7:9; 1Tim 4:8; Mhu 10:8Haki ya wanyofu huwaokoa,
bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
711:7 Ay 8:13; Mit 10:28Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka;
yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
811:8 Mit 21:8Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu,
naye mtu mwovu huingia humo badala yake.
911:9 Mit 12:6; Yer 45:5; Ay 8:13Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu
humwangamiza jirani yake,
bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.
1011:10 2Fal 11:20; Mit 28:12; Es 8:15Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi;
mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
1111:11 Mit 14:34; 29:8Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa,
bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.
1211:12 Mit 14:21; Ay 6:24Mtu asiye na akili humdharau jirani yake,
bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.
1311:13 Law 19:16; 1Tim 5:13; Mit 20:19; 10:14Masengenyo husaliti tumaini,
bali mtu mwaminifu hutunza siri.
1411:14 Mit 20:18; 24:6; 2Sam 15:34; 1Fal 12:1; Mit 20:18; 2Sam 15:34; Mit 15:22; 24:6; 1Fal 12:1Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka,
bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.
1511:15 Mit 6:1; 17:18; 22:26-27Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka,
bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
1611:16 Mit 31:31Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima,
bali wanaume wakorofi hupata mali tu.
1711:17 Mt 25:34Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe,
bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe.
1811:18 Hos 10:12; Kut 1:20; Ay 4:8Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu,
bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.
1911:19 Kum 30:15; Mit 10:2; 1Sam 2:6; Za 89:48; Mit 1:18-19; Mhu 7:2; Yer 43:1Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima,
bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.
2011:20 1Nya 29:17; Za 52:7Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu,
bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.
2111:21 Mit 16:5; Za 112:2Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa,
bali wenye haki watakuwa huru.
22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe
ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.
2311:23 Rum 2:8, 9Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema,
bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.
2411:24 Za 112:9Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi,
mwingine huzuia, lakini huwa maskini.
2511:25 Mit 22:9; 2Kor 9:6-9; Mt 5:7Mtu mkarimu atastawi;
yeye awaburudishaye wengine
ataburudishwa mwenyewe.
2611:26 Amo 8:5; Ay 29:13Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka,
bali baraka itamkalia kichwani kama taji
yeye aliye radhi kuiuza.
2711:27 Es 7:10; Za 7:15-16Yeye atafutaye mema hupata ukarimu,
bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.
2811:28 Yer 9:23; 17:8; Mk 10:25; Za 52:8Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka,
bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
2911:29 Mhu 5:16; Mit 14:19Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo,
naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.
3011:30 Mwa 2:9; Yak 5:20Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima,
naye mwenye hekima huvuta roho za watu.
3111:31 Yer 25:29; 49:12; 1Pet 4:18Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani,
si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?