Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mhubiri 1:1-18

Kila Kitu Ni Ubatili Mtupu

11:1 Mhu 7:27; 12:10Maneno ya Mhubiri, mwana wa Daudi, mfalme huko Yerusalemu:

21:2 Za 39:5-6; 62:9; Rum 8:20-21; Mhu 4:4-6; 12:8“Ubatili mtupu! Ubatili mtupu!”

Mhubiri anasema.

“Ubatili mtupu!

Kila kitu ni ubatili.”

31:3 Mhu 3:9; 5:15-16; 2:11-22Mwanadamu anafaidi nini kutokana na kazi yake yote

anayotaabikia chini ya jua?

41:4 2Pet 3:10; Za 104:5; Ay 8:19Vizazi huja na vizazi hupita,

lakini dunia inadumu milele.

51:5 Za 19:5-6Jua huchomoza na jua huzama,

nalo huharakisha kurudi mawioni.

6Upepo huvuma kuelekea kusini

na kugeukia kaskazini,

hurudia mzunguko huo huo,

daima ukirudia njia yake.

71:7 Ay 36:28; 38:10Mito yote hutiririka baharini,

hata hivyo bahari kamwe haijai.

Mahali mito inapotoka,

huko hurudi tena.

81:8 Mhu 3:1; Mit 27:20Vitu vyote vinachosha,

zaidi kuliko mtu anavyoweza kusema.

Jicho kamwe halitosheki kutazama,

wala sikio halishibi kusikia.

91:9 Mwa 8:22; Mhu 3:15; 2:12Kile kilichokuwepo kitakuwepo tena,

kile kilichofanyika kitafanyika tena,

hakuna kilicho kipya chini ya jua.

10Kuna kitu chochote ambacho mtu anaweza kusema,

“Tazama! Kitu hiki ni kipya”?

Kilikuwepo tangu zamani za kale,

kilikuwepo kabla ya wakati wetu.

111:11 Mhu 8:10; 9:5, 15; 2:16; Za 88:12; Mwa 40:23Hakuna kumbukumbu ya watu wa zamani,

hata na wale ambao hawajaja bado

hawatakumbukwa

na wale watakaofuata baadaye.

Hekima Ni Ubatili

12Mimi, Mhubiri, nilikuwa mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. 131:13 Mwa 3:17-19; Mhu 3:10; Ay 28:3Nilitumia muda wangu wote kujifunza na kuvumbua kwa hekima yote yanayofanyika chini ya mbingu. Jinsi gani Mungu ameweka mzigo mzito juu ya wanadamu! 141:14 Mhu 2:11; 4:4; 6:9Nimeshaona mambo yote yanayotendeka chini ya jua, hayo yote ni ubatili, hii ni kukimbiza upepo.

151:15 Mhu 7:13Kilichopindika hakiwezi kunyooshwa,

kile ambacho hakipo haiwezekani kukihesabu.

161:16 1Fal 3:12; 4:30; Mhu 2:9Niliwaza mwenyewe, “Tazama, nimekua na kuongezeka katika hekima kuliko yeyote aliyewahi kutawala Yerusalemu kabla yangu. Nimekuwa na uzoefu mkubwa wa hekima na maarifa.” 171:17 1The 5:21; Mhu 7:23, 25; 2:3, 12; 8:16Ndipo nilipojitahidi kufahamu kutofautisha hekima, wazimu na upumbavu, lakini nikatambua hata hili nalo ni kukimbiza upepo.

181:18 Mhu 2:23; 12:12; 7:16; Ay 28:28; Yer 45:3Kwa kuwa hekima nyingi huleta huzuni kubwa;

maarifa yanapoongezeka, masikitiko yanaongezeka.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

傳道書 1:1-18

萬事虛空

1以下是在耶路撒冷做王的大衛之子——傳道者的話。

2傳道者說:虛空的虛空,

虛空的虛空,一切都是虛空。

3人在日光之下的一切勞碌有什麼益處呢?

4一代過去,一代又來,

大地卻永遠長存。

5太陽升起,太陽落下,

匆忙回到升起之地。

6風吹向南,又轉向北,

循環不息,周而復始。

7江河湧流入海,海卻不會滿溢;

江河從何處流出,又返回何處。

8萬事令人厭煩,人述說不盡。

眼看,看不飽;

耳聽,聽不夠。

9以往發生的事,將來還會發生;

先前做過的事,將來也必再做。

日光之下,根本沒有新事。

10人可以指著哪件事說:

「看啊,這是新事」?

所謂的新事在我們以前早就有了。

11過去的事無人記得,

將來的事後人也不記得。

智慧之虛空

12我傳道者曾在耶路撒冷以色列的王。 13我專心用智慧去研究、探索天下各樣的事,發現上帝給世人的是極重的苦工。 14我觀察一切日光之下所做的事,看啊,都是虛空,好像捕風。 15彎曲的不能變直,缺少的無法補足1·15 補足」希伯來文是「數算」。16我心裡想:「我獲得極大的智慧,遠超過以前統治耶路撒冷的人。我擁有豐富的智慧和知識。」 17我又專心察明智慧和知識、狂妄和愚昧,卻發現這也是捕風。 18因為智慧越高,愁煩越多;知識越多,痛苦越深。