Matendo 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Matendo 1:1-26

Kanisa La Kwanza

(1:1–5:42)

Ahadi Ya Roho Mtakatifu

11:1 Lk 1:14; 3:23Katika kitabu changu cha kwanza nilikuandikia, mpendwa Theofilo, kuhusu mambo yote Yesu aliyofanya na kufundisha tangu mwanzo, 21:2 Mk 16:19; 6:30; Mt 28:19-20; 10:1-4; Yn 13:18hadi siku ile alipochukuliwa kwenda mbinguni, baada ya kuwapa maagizo kupitia kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua. 31:3 1Kor 15:5-7; Mt 28:17; Lk 24:39-43Baada ya mateso yake, alijionyesha kwao na kuwathibitishia kwa njia nyingi kwamba yeye yu hai. Katika muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake aliwatokea na kunena kuhusu Ufalme wa Mungu. 41:4 Lk 24:49; Yn 14:16; Mdo 2:33Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake. 51:5 Mk 1:4, 8; Mt 3:11; Mdo 11:16; 19:4; Yoe 3:18; Mdo 2:4; 11:15Yohana aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Yesu Apaa Mbinguni

(Marko 16:19-20; Luka 24:50-53)

61:6 Mt 17:11; Mdo 3:21; Lk 24:21; Isa 1:26; Dan 7:27; Amo 9:11Mitume walipokuwa wamekusanyika pamoja, wakamuuliza Yesu, “Bwana, je, huu ndio wakati wa kuwarudishia Israeli ufalme?”

71:7 Za 102:13; Mt 24:48Yesu akawaambia, “Si juu yenu kujua nyakati na majira ambayo Baba ameyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. 81:8 Mdo 2:1-4; Lk 24:48Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria, hadi miisho ya dunia.”

91:9 Mk 16:19; Lk 24:51; Yn 6:62Baada ya kusema mambo haya, walipokuwa wanatazama, akachukuliwa juu mbinguni mbele ya macho yao na wingu likampokea wasimwone tena.

101:10 Lk 24:4; Yn 20:12; Mt 28:3; Mk 16:5; Mdo 10:3, 30Walipokuwa bado wakikaza macho yao kuelekea juu alipokuwa akienda zake Mbinguni, tazama ghafula, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe wakasimama karibu nao, 111:11 Mdo 2:7; Mt 16:27; Lk 21:27; 1Tim 3:16; Mdo 1:7wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda Mbinguni, atarudi tena jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake Mbinguni.”

Mathiya Achaguliwa Badala Ya Yuda

(Mathayo 27:3-10)

121:12 Lk 24:52; Mt 21:1Ndipo waliporudi Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni, uliokuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa mwendo wa Sabato1:12 Mwendo wa Sabato hapa ina maana umbali wa mita 1,100. kutoka mjini. 131:13 Mdo 9:37; 20:8; Mt 10:2-4; Mk 3:16-19Walipowasili mjini Yerusalemu, walikwenda ghorofani kwenye chumba walichokuwa wakiishi. Wale waliokuwepo walikuwa: Petro, Yohana, Yakobo, Andrea, Filipo, Tomaso, Bartholomayo, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote1:13 Zelote hapa ina maana alikuwa mwanachama wa Wazelote, kikundi cha Kiyahudi cha kupinga jeuri ya Warumi. na Yuda mwana wa Yakobo. 141:14 Lk 18:1; 23:49-55; Mt 12:46Hawa wote waliungana pamoja katika maombi. Pamoja nao walikuwepo wanawake kadha, na Maria mama yake Yesu, pamoja na ndugu zake Yesu.

151:15 Ufu 3:4Katika siku hizo Petro akasimama katikati ya waumini (jumla yao wote walikuwa watu wapatao 120), akasema, 161:16 Mt 10:4; Yn 13:18“Ndugu zangu, ilibidi Andiko litimie ambalo Roho Mtakatifu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda aliyewaongoza wale waliomkamata Yesu. 171:17 Yn 6:70-71; Mt 10:4; Lk 6:16; Mdo 12:25; 20:24; 21:19Yuda alikuwa mmoja wetu, kwa maana na yeye alichaguliwa ashiriki katika huduma hii.”

181:18 Mt 26:14-15; 27:3-10(Basi Yuda alinunua shamba kwa zile fedha za uovu alizopata; akiwa huko shambani akaanguka, akapasuka na matumbo yote yakatoka nje. 191:19 Yn 5:2Kila mtu Yerusalemu akasikia habari hizi, kwa hiyo wakapaita mahali hapo kwa lugha yao, Akeldama, yaani Shamba la Damu).

201:20 Za 69:25; 109:8“Kama vile ilivyoandikwa katika kitabu cha Zaburi,

“ ‘Mahali pake na pawe ukiwa,

wala asiwepo yeyote atakayeishi humo,’

na,

“ ‘Mtu mwingine aichukue nafasi yake ya uongozi.’

211:21 Yn 15:27Kwa hiyo inatubidi tumchague mtu mwingine miongoni mwa wale ambao wamekuwa pamoja nasi wakati wote Bwana Yesu alipoingia na kutoka katikati yenu, 221:22 Mk 1:4; Lk 24:48kuanzia ubatizo wa Yohana mpaka siku aliyochukuliwa kutoka kwetu kwenda Mbinguni. Kwa kuwa mmoja wao inabidi awe shahidi pamoja nasi wa ufufuo wake.”

231:23 Mdo 15:22Wakapendekeza majina ya watu wawili: Yosefu, aitwaye Barsaba (ambaye pia alijulikana kama Yusto) na Mathiya. 241:24 Mdo 13:3; 14:23; 1Sam 16:7; Ufu 2:23Kisha wakaomba, wakasema, “Bwana, wewe waujua moyo wa kila mtu. Tuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua 251:25 Mdo 1:17ili achukue nafasi ya huduma ya utume ambayo Yuda aliiacha ili aende mahali pake mwenyewe.” 261:26 Mdo 2:14Kisha wakawapigia kura, nayo kura ikamwangukia Mathiya, naye akaongezwa kwenye wale mitume kumi na mmoja.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

使徒行传 1:1-26

应许圣灵降临

1提阿非罗啊,在前一封信中,我从耶稣的生平和教导开始, 2一直谈到祂借着圣灵吩咐了自己所选立的使徒,然后被接回天上。 3祂受难后用许多确据向使徒显明自己活着,在四十天之内屡次向他们显现,并谈论上帝的国。 4有一次,耶稣和他们在一起吃饭的时候,叮嘱他们:“你们不要离开耶路撒冷,要在那里等候我对你们说过的天父的应许。 5因为从前约翰用水施洗,但过不了多少天,你们要受圣灵的洗。”

6他们跟耶稣在一起的时候问祂:“主啊,你要在这时候复兴以色列国吗?” 7耶稣回答说:“天父照自己的权柄定下的时间、日期不是你们可以知道的。 8但圣灵降临在你们身上后,你们必得到能力,在耶路撒冷犹太全境和撒玛利亚,直到地极,做我的见证人。”

9耶稣说完这些话,就在他们注视下被提升天,被一朵云彩接去,离开了他们的视线。 10祂上升时,他们都定睛望着天空,忽然有两个身穿白衣的人站在他们身旁, 11说:“加利利人啊!你们为什么站在这里望着天空呢?这位离开你们被接到天上的耶稣,你们看见祂怎样升天,将来祂还要怎样回来。”

选立新使徒

12于是,他们从橄榄山回到耶路撒冷。橄榄山距离耶路撒冷不远,约是安息日允许走的路程1:12 按犹太人的传统,在安息日只能走约一公里远。13他们进城后,来到楼上所住的房间。当时有彼得约翰雅各安得烈腓力多马巴多罗买马太亚勒腓的儿子雅各、激进党人西门雅各的儿子犹大14他们同几个妇女,以及耶稣的弟弟们和母亲玛丽亚在一起同心合意地恒切祷告。

15那时,约有一百二十人在聚会,彼得从他们当中站起来说: 16“弟兄们,关于带人抓耶稣的犹大,圣灵借着大卫的口早已预言,这经文必须要应验。 17犹大原本是我们中间的一员,与我们同担使徒的职分。”

18他用作恶得来的钱买了一块田,他头朝下栽倒在地,肚破肠流。 19这消息很快传遍了耶路撒冷,当地人称那块田为“亚革大马”,就是“血田”的意思。

20彼得继续说:“诗篇上写道,‘愿他的家园一片荒凉,无人居住’1:20 诗篇69:25,又说,‘愿别人取代他的职位。’1:20 诗篇109:8 21-22所以,我们必须另选一个人代替犹大,与我们一同为主耶稣的复活做见证。他必须是从主耶稣接受约翰的洗礼起一直到主升天,始终与我们在一起的人。”

23于是他们推荐两个人:别号巴撒巴又叫犹士都约瑟马提亚24-25大家便祷告说:“主啊!你洞悉每个人的内心,求你指明这二人中你选了谁来担负使徒的职分。犹大丢弃了这职分,去了他该去的地方。” 26然后,他们抽签,抽中了马提亚,就把他加到十一位使徒的行列。