Marko 15 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Marko 15:1-47

Yesu Mbele Ya Pilato

(Mathayo 27:1-14; Luka 23:1-5; Yohana 18:28-38)

115:1 Mt 27:1-2; Lk 22:66; Mt 5:22Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.

215:2 Mt 2:2Pilato akamuuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akajibu, “Wewe umesema.”

3Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. 415:4 Mt 27:13Pilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.”

515:5 Mk 14:61Lakini Yesu hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa.

Pilato Amtoa Yesu Asulubiwe

(Mathayo 27:15-26; Luka 23:13-25; Yohana 18:39–19:16)

615:6 Mt 27:15; Lk 23:17; Yn 18:39Ilikuwa desturi wakati wa Sikukuu ya Pasaka kumfungulia mfungwa yeyote ambaye watu wangemtaka. 7Wakati huo, mtu aliyeitwa Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wametekeleza uuaji wakati wa maasi. 8Ule umati wa watu ukamjia Pilato na kumwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi yake.

9Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie huyu Mfalme wa Wayahudi?” 1015:10 Yn 11:48; 12:19; Mt 27:38Kwa maana yeye alitambua kuwa viongozi wa makuhani walikuwa wamemtia Yesu mikononi mwake kwa ajili ya wivu. 1115:11 Mdo 3:14Lakini viongozi wa makuhani wakauchochea ule umati wa watu wamwombe awafungulie Baraba badala yake.

12Pilato akawauliza tena, “Basi mnataka nifanye nini na huyu mtu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?”

13Wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe!”

14Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?”

Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, wakisema, “Msulubishe!”

1515:15 Isa 53:6; Mt 27:26; Yn 19:1, 36Pilato, akitaka kuuridhisha ule umati wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.

Askari Wamdhihaki Yesu

(Mathayo 27:27-31; Yohana 19:2-3)

1615:16 Yn 18:28-33; 19:9Askari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio,15:16 Praitorio maana yake ni makao makuu ya mtawala; ni jumba la kifalme lililokuwa linakaliwa na Pontio Pilato huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu. wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17Wakamvalisha Yesu joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani. 18Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” 19Wakampiga kwa fimbo ya mwanzi tena na tena kichwani na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake, wakamsujudia kwa kumdhihaki. 2015:20 Ebr 13:12Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe.

Kusulubiwa Kwa Yesu

(Mathayo 27:32-44; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27)

2115:21 Mt 27:32; Lk 23:36Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Aleksanda na Rufo, alikuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shamba, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 2215:22 Mt 27:33; Lk 23:33; Yn 19:17Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 2315:23 Za 69:21; Mit 31:6Nao wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini hakuinywa. 2415:24 Za 22; 18Basi wakamsulubisha, nazo nguo zake wakagawana miongoni mwao kwa kuzipigia kura ili kuamua ni gani kila mtu ataichukua.

2515:25 Mt 27:45; Lk 23:44; Yn 19:14Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 2615:26 Mt 27:37; Yn 19:19; Mk 15:2Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: “Mfalme wa Wayahudi.” 2715:27 Mt 27:38Pamoja naye walisulubiwa wanyangʼanyi wawili, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. [ 2815:28 Isa 51:12; Lk 22:37Nayo maandiko yakatimizwa, yale yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na watenda dhambi.]” 2915:29 Za 22:7; 109:25; Mk 14:58; Yn 2:19Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao na kusema, “Aha! Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, 30basi shuka kutoka msalabani na ujiokoe mwenyewe!”

3115:31 Za 22:7Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa sheria wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! 3215:32 Mk 14:61; 15:2Basi huyu Kristo,15:32 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. huyu Mfalme wa Israeli, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.

Kifo Cha Yesu Msalabani

(Mathayo 27:45-56; Luka 23:44-49; Yohana 19:28-30)

3315:33 Amo 8:9Ilipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa. 3415:34 Za 21:1; Mt 27:46Mnamo saa tisa, Yesu akapaza sauti, akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”)

35Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni, anamwita Eliya.”

3615:36 Mk 15:23; Za 69:21Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”

3715:37 Yn 19:30Kisha Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.

3815:38 Ebr 10:19-20Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini. 3915:39 Mt 4:3; Mk 9:7Basi yule jemadari aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Yesu aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

4015:40 Za 38:11; Lk 24:10; Yn 19:25Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwepo Maria Magdalene, na Maria mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome. 4115:41 Mt 27:55-56; Lk 8:2-3Hawa walifuatana na Yesu na kushughulikia mahitaji yake alipokuwa Galilaya. Pia walikuwepo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja pamoja naye Yerusalemu.

Maziko Ya Yesu

(Mathayo 27:57-61; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42)

4215:42 Mt 27:62; Yn 19:31Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa Siku ya Maandalizi, yaani siku moja kabla ya Sabato, 4315:43 Mt 5:22; 3:2; Lk 2:25, 38Yosefu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na ambaye alikuwa anautarajia Ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Yesu. 44Pilato alikuwa akijiuliza kama Yesu alikuwa amekwisha kufa. Hivyo akamwita yule jemadari, akamuuliza iwapo Yesu alikuwa amekwisha kufa. 4515:45 Mk 15:39Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yosefu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. 4615:46 Mk 16:3Hivyo Yosefu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi. 47Maria Magdalene na Maria mamaye Yose walipaona mahali pale alipolazwa.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马可福音 15:1-47

耶稣在彼拉多面前受审

1清早,祭司长、长老、律法教师和全公会的人商定后,便把耶稣绑起来押送到彼拉多那里。

2彼拉多问耶稣:“你是犹太人的王吗?”

耶稣回答说:“如你所言。”

3祭司长控告耶稣许多罪。

4彼拉多又问道:“你看,他们控告你这么多,你都不回答吗?”

5耶稣仍旧一言不发,彼拉多感到惊奇。

6每逢逾越节,彼拉多都会照惯例按民众的要求释放一个囚犯。 7那时,有一个囚犯名叫巴拉巴,与其他作乱时杀过人的囚犯关在一起。 8百姓聚来,要求彼拉多照惯例释放一个囚犯。

9彼拉多问:“你们要我为你们释放犹太人的王吗?” 10因为他知道祭司长把耶稣押来是出于嫉妒。 11但祭司长却煽动百姓,叫他们要求彼拉多释放巴拉巴

12彼拉多又问他们:“那么,这位你们称为犹太人之王的,我如何处置呢?”

13他们高喊:“把祂钉在十字架上!”

14彼拉多问:“为什么?祂犯了什么罪?”

他们却更大声地喊:“把祂钉在十字架上!”

15为了取悦众人,彼拉多释放了巴拉巴,下令将耶稣鞭打后交出去钉十字架。

耶稣受辱

16于是,士兵把耶稣押进总督府的院子,集合了全营的士兵。 17他们给祂穿上紫袍,用荆棘编成冠冕戴在祂头上, 18向祂行礼,并高呼:“犹太人的王万岁!” 19他们用苇秆打祂的头,向祂吐唾沫,跪拜祂。 20戏弄完了,就脱去祂的紫袍,给祂穿上原来的衣服,押祂出去钉十字架。

钉十字架

21亚历山大鲁孚的父亲古利奈西门从乡下来,途经那地方,卫兵就强迫他背耶稣的十字架。 22他们把耶稣带到各各他——意思是“髑髅地”, 23拿没药调和的酒给祂喝,但祂不肯喝。 24他们把耶稣钉在十字架上,还抽签分祂的衣服。 25他们钉祂十字架的时间是在上午九点钟。 26祂的罪状牌上写着“犹太人的王”。

27他们还把两个强盗钉在十字架上,一个在祂右边,一个在祂左边, 28这应验了圣经的话:“祂被列在罪犯中。”15:28 有古卷无28节。 29过路的人都嘲笑祂,摇着头说:“哈,你这要把圣殿拆毁又在三天内重建的人啊, 30救救你自己,从十字架上下来吧!”

31祭司长和律法教师也同样嘲讽祂,彼此议论说:“祂救了别人,却救不了自己! 32以色列的王基督,现在从十字架上下来吧!让我们看看,我们就信了!”与祂同钉十字架的强盗也嘲笑祂。

耶稣之死

33正午时分,黑暗笼罩着整个大地,一直到下午三点。 34大约下午三点,耶稣大声呼喊:“以罗伊,以罗伊,拉马撒巴各大尼?”意思是:“我的上帝,我的上帝,你为什么离弃我?”15:34 诗篇22:1

35有些站在旁边的人听见了,就说:“听,祂在呼叫以利亚。”

36有人跑去把一块海绵蘸满酸酒,绑在苇秆上送给祂喝,说:“等着吧,我们看看以利亚会不会救祂下来。”

37耶稣大叫一声,就断了气。 38圣殿的幔子从上到下裂成两半。 39站在对面的百夫长看见耶稣喊叫15:39 有古卷无“喊叫”二字。断气的情形,便说:“这人真是上帝的儿子!”

40有些妇女在远处观看,其中有抹大拉玛丽亚、小雅各约西的母亲玛丽亚撒罗米41耶稣在加利利时,她们就跟随祂、服侍祂了。此外还有好些跟着祂上耶路撒冷的妇女。

安葬耶稣

42那天是犹太人的预备日,也就是安息日的前一天。傍晚, 43亚利马太约瑟鼓起勇气去见彼拉多,要求领取耶稣的遗体。他是一位德高望重的公会议员,一直在等候上帝的国。 44彼拉多听见耶稣已经死了,十分惊讶,便把百夫长召来问个明白, 45得知耶稣确实已死,便将耶稣的遗体交给约瑟

46约瑟把耶稣的遗体取下来,用买来的细麻布裹好,安放在一个在岩壁上凿出的墓穴里,又滚来一块大石头堵住墓口。 47抹大拉玛丽亚约西的母亲玛丽亚都看到了安葬耶稣的地方。