Kutoka 38 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 38:1-31

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

(Kutoka 27:1-8)

138:1 Kut 27:1; 2Nya 29:23, 24; Za 51:15-19; Isa 61:8; Eze 44:11; 45:17; Ebr 9:14; 13:10Akatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu;38:1 Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35. nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wa dhiraa tano38:1 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. 238:2 2Nya 1:5; 1Fal 7:45Akatengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu zikawa zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. 338:3 Kut 31:9; 35:16Akatengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama na vyombo vya kuchukulia moto. 4Akatengeneza wavu wa shaba chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. 5Akasubu pete za shaba za kushikilia ile mipiko kwa ajili ya zile pembe nne za huo wavu wa shaba. 6Akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuifunika kwa shaba. 7Akaiingiza ile mipiko kwenye zile pete, ili iwe pande mbili za madhabahu kwa ajili ya kuibeba. Akaitengeneza madhabahu yenye uvungu ndani yake akitumia mbao.

Sinia La Kunawia

(Kutoka 30:18)

838:8 Kut 30:18; 40:7; Kum 23:17; 1Sam 2:22; 1Fal 14:24; 2Fal 16:17; 2Nya 4:2; Za 26:6; Zek 13:1; Eze 36:25; 2Kor 7:1; Ebr 10:22; 1Yn 5:6Akatengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kutoka kwa vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake waliohudumu pale ingilio la Hema la Kukutania.

Ua Wa Hema La Kukutania

(Kutoka 27:9-19)

938:9 Kut 27:9; Za 84:2; 92:13Kisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja,38:9 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45. na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, 10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

12Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini38:12 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, pia ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano38:14 Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75. yalikuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yalikuwa upande mwingine wa ingilio la ua, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16Mapazia yote yaliyozunguka ua yalikuwa ya kitani iliyosokotwa vizuri. 17Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha.

1838:18 2Nya 3:14Pazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano, 19likiwa na nguzo nne na vitako vinne vya shaba. Kulabu zake na tepe zake zilikuwa za fedha, na ncha zake zilikuwa zimefunikwa kwa fedha. 2038:20 Kut 35:18; 38:20; 27:10; 2Nya 3:9; Ezr 9:8; Isa 22:23; Efe 2:21, 22Vigingi vyote vya maskani na vya ua ulioizunguka vilikuwa vya shaba.

Vifaa Vilivyotumika

2138:21 Hes 1:50-53; 8:24; 9:15; 10:11; 17:7; 1Nya 23:32; 2Nya 24:6; Mdo 7:44; Ufu 15:5; Hes 4:28-33Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani, maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Mose, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni. 2238:22 Kut 31:2(Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, alifanya kila kitu Bwana alichomwamuru Mose, 2338:23 Kut 31:6akiwa pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, fundi stadi wa kutia nakshi, kubuni michoro, mtarizi kwa rangi ya buluu, ya zambarau, nyekundu na kitani safi.) 2438:24 Kut 30:12-16; 12:37; Hes 3:47Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730,38:24 Talanta 29 na shekeli 730 ni sawa na tani moja. kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

2538:25 Kut 12:37; 30:12Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775,38:25 Talanta 100 na shekeli 1,775 za fedha ni sawa na tani 3.4. kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. 2638:26 Kut 30:12-16; 12:36-37; Hes 1:46Kila mtu alitoa beka moja, ambayo ni sawa na nusu shekeli ya fedha, kwa kazi ya mahali patakatifu, kutoka kwa kila mtu aliyekuwa amehesabiwa mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi, ambao jumla yao walikuwa wanaume 603,550. 2738:27 Kut 26:19Talanta hizo 100 za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na pazia: vitako mia moja kwa talanta mia, yaani, talanta moja kwa kila kitako. 28Akatumia zile shekeli hizo 1,775 kutengeneza kulabu za nguzo, kufunika ncha za nguzo na kutengeneza vitanzi vyake.

29Shaba iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa ilikuwa na uzito wa talanta 70 na shekeli 2,400.38:29 Talanta 70 na shekeli 2,400 ni sawa na tani 2.4. 30Akaitumia hiyo shaba kutengeneza vitako vya ingilio la Hema la Kukutania, madhabahu ya shaba pamoja na ule wavu wake na vyombo vyake vyote, 3138:31 Kut 27:19; 2Nya 3:9; Ezr 9:8; Isa 22:23; Efe 2:21, 22vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya Maskani pamoja na ule ua uliozunguka.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

出埃及记 38:1-31

祭坛、院子和奉献的物品

1比撒列用皂荚木造了方形的燔祭坛,长宽各两米二,高一米三, 2在坛的四角造四个凸起的角,与坛连成一体,坛外面包上铜。 3他用铜造祭坛用的一切器具,就是锅、铲、碗、肉叉、火鼎。 4又造了一个铜网,铜网在祭坛围边的下方,向下伸展到祭坛的腰部, 5在铜网的四角铸四个铜环,以便穿横杠。 6他用皂荚木做横杠,包上铜, 7把横杠穿在坛两旁的铜环里,以便抬坛。坛是中空的,用木板制作。

8他用在会幕门口服侍的妇女们的铜镜造铜盆和盆座。

9他用帷幔围成院子,院子南面的帷幔用细麻织成,长四十五米。 10帷幔有二十根柱子,二十个带凹槽的铜底座,柱子上的钩和箍都是银的。 11北面的帷幔也是长四十五米,柱子、铜底座、钩和箍的样式都与南面的一样。 12西面的帷幔宽二十二米半,有十根柱子和十个带凹槽的底座,钩和箍都是银的。 13东面的帷幔也是宽二十二米半。 14-15入口两边的帷幔都是宽七米,各有三根柱子和三个带凹槽的底座。 16院子四面的帷幔都用细麻织成。 17柱子带凹槽的底座是铜的,柱子上面的钩和箍是银的,柱顶包银,院子所有的柱子都有银箍。 18院子入口的门帘用细麻和蓝色、紫色、朱红色毛线绣制,长九米、高两米二,与院子帷幔的高度一样。 19门帘有四根柱子和四个带凹槽的铜底座,柱子上的钩和箍都是银的,柱顶包银。 20圣幕和院子四围所有的橛子都是铜的。 21以上是安放约柜的圣幕中所用的物品,是照摩西的吩咐,由亚伦祭司的儿子以他玛指挥利未人清点的。

22犹大支派户珥的孙子、乌利的儿子比撒列做好了耶和华吩咐摩西预备的一切物品。 23他的助手是支派亚希撒抹的儿子亚何利亚伯,是雕刻家和设计师,并善用细麻和蓝色、紫色、朱红色毛线刺绣。

24按圣所的秤计算,建造圣所共用了奉献的金子两万两。 25按圣所的秤计算,从登记的人口所收到的银子是六万八千四百两。 26这是所有登记的、年龄在二十岁以上的人所缴纳的银子,共有六十万三千五百五十人,每人交六克银子,以圣所的秤为准。 27铸造圣所带凹槽的底座和帷幔柱子带凹槽的底座共用了六万八千两银子,共铸造了一百个底座,每个底座用了六百八十两银子。 28剩下的四百两银子用来制造柱子上的钩和箍以及包柱顶。 29百姓奉献的铜共有两千四百公斤, 30用来制造会幕入口带凹槽的底座、祭坛、坛上的铜网及一切器具、 31院子周围和院子入口带凹槽的底座以及圣幕、院子周围所有的橛子。