Kutoka 11 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 11:1-10

Pigo La Kumi: Kuuawa Wazaliwa Wa Kwanza

111:1 Kut 3:20; 6:1Basi Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa. 211:2 Kut 3:21-22Waambie watu wote waume kwa wake wawaombe majirani zao vitu vya fedha na vya dhahabu.” 311:3 Mwa 39:21; Kum 34:11; 2Sam 7:9; 8:13; 22:44; Es 9:4; Za 89:27(Bwana akawafanya Wamisri wawe na moyo wa ukarimu kwa Waisraeli, naye Mose mwenyewe akaheshimiwa sana na maafisa wa Farao na watu wote katika nchi ya Misri.)

411:4 Kut 12:29; Ay 34:20; Kut 12:23; Za 81:5Kwa hiyo Mose akasema, “Hili ndilo Bwana asemalo: ‘Panapo usiku wa manane Mimi nitapita katika nchi yote ya Misri. 511:5 Kut 4:23; Za 78:51; Isa 47:2Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, aketiye penye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mtumwa wa kike, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo. 611:6 Kut 12:30; Mit 21:13; Amo 5:17Patakuwepo kilio kikubwa katika nchi yote ya Misri, kilio kibaya ambacho hakijakuwepo wala kamwe hakitakuwepo tena. 711:7 Kut 8:22Lakini miongoni mwa Waisraeli hakuna hata mbwa atakayembwekea mwanadamu wala mnyama yeyote.’ Ndipo mtakapojua kuwa Bwana huweka tofauti kati ya Misri na Israeli. 811:8 Kut 12:31-33; Ebr 11:27Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao.

911:9 Kut 7:4; 3:20Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Farao atakataa kukusikiliza, ili maajabu yangu yapate kuongezeka katika nchi ya Misri.” 1011:10 Kut 4:21; Rum 2:5Mose na Aroni wakafanya maajabu haya yote mbele ya Farao, lakini Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke katika nchi yake.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

出埃及记 11:1-10

灭长子之灾

1耶和华对摩西说:“我给法老和埃及再降下一场灾难,之后他必放你们走,甚至是把你们彻底赶走。 2你要告诉以色列人,不论男女,去向邻近的埃及人索取金器银器。” 3耶和华使埃及人恩待以色列人,法老的臣仆和百姓极其尊重摩西

4摩西说:“耶和华这样说,‘今晚半夜,我要走遍埃及5埃及境内,从坐王位的法老的长子到推磨女奴的长子,以及所有头生的牲畜,都必死亡。 6那时整个埃及必充满哭号声,惨况空前绝后。 7但在以色列人中,连狗也不会向人或牲畜吠叫,这样你们就知道耶和华把埃及人和以色列人区分开了。 8到那时,你所有的臣仆都要来向我下拜,求我和跟随我的百姓离开这里。然后我才会离开。’”摩西说完便怒气冲冲地离开法老。 9耶和华曾对摩西说:“法老一定不肯听你的话,因此我要在埃及多行神迹。” 10摩西亚伦在法老面前行了这一切神迹,但耶和华使法老的心刚硬,他不让以色列人离开他的国土。