Kumbukumbu 31 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 31:1-30

Yoshua Kutawala Baada Ya Mose

(Hesabu 27:12-23)

1Kisha Mose akaenda akasema maneno haya kwa Waisraeli wote: 231:2 Kut 7:7; Hes 27:17; Kum 34:7; 1Fal 3:7; Kum 3:23-26“Sasa nina miaka mia moja na ishirini nami siwezi tena kuwaongoza. Bwana ameniambia, ‘Hutavuka Yordani.’ 331:3 Hes 27:18; Kum 9:3; 7:1; 3:28Bwana Mungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kama Bwana alivyosema. 431:4 Hes 21:33Naye Bwana atawafanyia watu hao kile alichowafanyia Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, ambao aliwaangamiza pamoja na nchi yao. 531:5 Kum 2:33; 7:2Bwana atawakabidhi kwenu, nanyi lazima mwatendee yale yote niliyowaamuru. 631:6 Yos 1:6-9, 18; 10:23; 1Nya 22:13; 28:20; 2Nya 32:7; Yer 1:8, 17; Eze 2:6; Mwa 28:15; Kum 1:29; 20:4; Mt 28:20; Za 56:9; 118:6; Kum 4:31; 1Sam 12:22; 1Fal 6:13; Za 94:14; Isa 41:17; Ebr 13:5Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi.”

731:7 Hes 27:23; Yos 1:6; Kum 1:38; 3:28Kisha Mose akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ile Bwana aliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao. 831:8 Kut 13:21; Mwa 28:15; Kut 33:14; Kum 4:31Bwana mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike.”

Kusoma Sheria

931:9 Kut 17:14; Hes 4:15; 1Nya 15:2Kwa hiyo Mose akaandika sheria hii na kuwapa makuhani, wana wa Lawi, waliochukua Sanduku la Agano la Bwana na wazee wote wa Israeli. 1031:10 Kum 15:1; Kut 23:16; Kum 16:13; Law 23:34Kisha Mose akawaamuru, akasema: “Mwishoni mwa kila miaka saba, katika mwaka wa kufuta madeni, wakati wa Sikukuu ya Vibanda, 1131:11 Kum 16:16; 12:5; Yos 8:34-35; 2Fal 23:2; Neh 8:2Waisraeli wote wanapokuja mbele za Bwana Mungu wenu mahali atakapopachagua, utasoma sheria hii mbele yao masikioni mwao. 1231:12 Kum 4:10; Hag 1:12; Mal 1:6; 3:5, 16Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumcha Bwana Mungu wenu na kufuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii. 1331:13 Kum 11:2; Za 78:6-7; Mit 22:6; Efe 6:4Watoto wao, ambao hawaijui sheria hii, lazima waisikie na kujifunza kumcha Bwana Mungu wenu kwa muda mtakaoishi katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

Kuasi Kwa Waisraeli Kunatabiriwa

1431:14 Mwa 25:8; Hes 27:13; 23; Kum 34:9; Yos 1:1-9; Hes 27:19; Kut 33:9-11Bwana akamwambia Mose, “Sasa siku ya kifo chako imekaribia. Mwite Yoshua, mkajihudhurishe katika Hema la Kukutania, mahali nitakapompa maagizo ya kazi.” Kwa hiyo Mose na Yoshua wakaja na kujihudhurisha kwenye Hema la Kukutania.

1531:15 Kut 33:9; Za 99:7Kisha Bwana akatokea katika Hema katika nguzo ya wingu, nalo wingu likasimama juu ya ingilio la Hema. 1631:16 Mwa 15:15; Kut 34:15; Kum 4:25-28; Amu 2:12; 10:6-13; 1Fal 9:9; 18:18; 19:10; Yer 2:13; 5:19; 19:4; 2Sam 7:12; 2Fal 22:16, 17; Isa 1:4Kisha Bwana akamwambia Mose: “Unakwenda kupumzika na baba zako, nao watu hawa hivi karibuni watazini na miungu migeni ya nchi wanayoingia. Wataniacha na kuvunja Agano nililofanya nao. 1731:17 Kum 32:16; Amu 2:14; 20; 10:7; 2Fal 13:3; 22:13; Za 106:29, 40; Yer 7:18; 21:5; 36:17; Amu 6:13; 2Nya 15:2; 24:20; Ezr 8:22; Za 44:9; Isa 2:6; Kum 32:20; Isa 1:15; 45:15; 53:3; 54:8; Ay 13:24; Za 13:1; 27:9; 30:7; 104:29; Isa 50:6; Yer 33:5; Eze 39:29; Mik 3:4; Yer 4:20; Eze 7:26; Hes 14:42; Hos 9:12Siku hiyo nitawakasirikia na kuwaacha; nitawaficha uso wangu, nao wataangamizwa. Maafa mengi na shida nyingi zitakuja juu yao, nao siku hiyo watauliza, ‘Je, maafa haya hayakuja juu yetu kwa sababu Mungu wetu hayuko pamoja nasi?’ 18Nami hakika nitauficha uso wangu siku hiyo kwa sababu ya maovu yao yote kwa kugeukia miungu mingine.

1931:19 Mwa 31:50“Sasa ujiandikie wimbo huu,31:19 Wimbo huu hapa ina maana wimbo wa Mose. uwafundishe Waisraeli na uwaamuru wauimbe, ili upate kuwa ushahidi wangu dhidi yao. 2031:20 Kum 6:10-12; Za 4:2; 16:4; 40:4; Yer 13:25; Dan 3:28; Amo 2:4; Kum 8:19; 11:16-17Nitakapokwisha kuwaingiza katika nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo, nao watakapokula wakashiba na kufanikiwa, watageukia miungu mingine na kuiabudu, wakinikataa mimi na kuvunja Agano langu. 2131:21 Kum 4:30; 1Nya 28:9; Hos 5:3; Yn 2:24-25Maafa na shida zitakapokuja juu yao, wimbo huu utashuhudia dhidi yao, kwa sababu hautasahauliwa na wazao wao. Ninajua lile wanaloandaa kufanya, hata kabla sijawaingiza katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo.” 22Hivyo Mose akaandika wimbo huu siku ile na akawafundisha Waisraeli.

2331:23 Yos 1:6Bwana akampa Yoshua mwana wa Nuni agizo hili: “Uwe hodari na shujaa, kwa kuwa utawaleta Waisraeli katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo, nami mwenyewe nitakuwa pamoja nawe.”

2431:24 Kum 17:18; 2Fal 22:8; Kum 28:58Baada ya Mose kumaliza kuandika kwenye kitabu maneno ya sheria hii kutoka mwanzo hadi mwisho, 25akawapa Walawi wale waliolibeba Sanduku la Agano la Bwana agizo hili, akawaambia: 26“Chukueni Kitabu hiki cha Sheria mkakiweke kando ya Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu. Hapo ndipo kitakapokaa kama shahidi dhidi yenu. 2731:27 Kut 23:21; 32:9; Kum 9:27; 2Nya 30:8; Za 78:8; Isa 48:4; Za 32Kwa kuwa ninajua jinsi mlivyo waasi na mlivyo na shingo ngumu. Kama mmekuwa mkiasi dhidi ya Bwana nikiwa bado niko hai na nikiwa pamoja nanyi, mtaasi mara ngapi baada ya kufa kwangu! 2831:28 Kum 4:26; 30:19; 32:1; Ay 20:27; Isa 26:21Kusanyeni mbele yangu wazee wote wa makabila yenu na maafisa wenu wote, ili nipate kusema maneno haya masikioni mwao na kuziita mbingu na nchi ili kushuhudia dhidi yao. 2931:29 Kum 4:16; Ufu 9:20; 1Fal 9:9; 22:23; 2Fal 22:16Kwa kuwa ninajua baada ya kifo changu hakika mtakuwa waovu kabisa na kugeuka kutoka njia niliyowaamuru ninyi. Katika siku zijazo, maafa yatawapata kwa sababu mtafanya maovu mbele ya macho ya Bwana, na kuchochea hasira yake kwa yale mikono yenu itakayokuwa imefanya.”

Wimbo Wa Mose

30Mose akayasoma maneno ya wimbo huu kutoka mwanzo hadi mwisho katika masikio ya kusanyiko lote la Israeli:

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

申命記 31:1-30

立約書亞做摩西的接班人

1摩西繼續對以色列人說: 2「我現在已經一百二十歲了,無法再繼續帶領你們,耶和華曾說我不得過約旦河。 3你們的上帝耶和華要親自帶領你們過河,在你們面前消滅那裡的各族,使你們佔領他們的土地。約書亞將帶領你們過河,正如耶和華所言。 4耶和華要毀滅那裡的各族,像毀滅亞摩利二王西宏及其國家一樣。 5耶和華要把他們交給你們,你們要照我的一切吩咐處置他們。 6你們要剛強勇敢,不要懼怕他們,因為你們的上帝耶和華與你們同行,祂不會撇下你們,也不會離棄你們。」

7摩西約書亞叫來,當著全體以色列人的面對他說:「你要剛強勇敢!因為你要與百姓一同進入耶和華起誓要賜給他們祖先的土地,把土地分給他們作產業。 8耶和華必帶領你,與你同在。祂不會撇下你,也不會離棄你。不要驚慌害怕。」

每七年當眾宣讀律法一次

9摩西把這律法寫好,交給抬耶和華約櫃的利未祭司和以色列的眾長老。 10摩西吩咐他們說:「每逢免除債務的第七年的住棚節, 11所有以色列人到你們的上帝耶和華選定的地方朝見祂時,你們要當眾大聲宣讀這律法。 12要招聚所有男女、孩童以及住在你們中間的外族人,讓他們聆聽這律法,學習敬畏你們的上帝耶和華,謹遵律法上的一切話。 13這樣,他們那些還不知道這律法的孩子便有機會聽到律法,在你們將要佔領的約旦河西岸的土地上,學習終生敬畏你們的上帝耶和華。」

上帝對摩西和約書亞的指示

14耶和華對摩西說:「你快要離世了。叫約書亞與你一起到會幕,我要委派他。」摩西約書亞就來到會幕。 15有雲柱停在會幕入口的上方,耶和華在雲柱中向他們顯現。

16耶和華對摩西說:「你快要與祖先同眠了。這些百姓將很快在要佔領的土地上與外族人的神明苟合,背棄我,違背我與他們所立的約。 17那時,我要向他們發怒,離棄他們,掩面不理他們。他們將被吞滅,遭遇許多禍患和災難,以致他們會說,『這些禍患臨到我們,豈不是因為上帝不在我們中間了嗎?』 18那時,我必掩面不理他們,因為他們祭拜其他神明,行為邪惡。

19「現在,你要寫一首歌,教導以色列人,讓他們吟唱,作為我指控他們的證據。 20因為當我把他們帶到我起誓應許他們祖先的奶蜜之鄉後,當他們在那裡吃飽喝足後,就會嫌棄我,違背我與他們所立的約,去供奉其他神明。 21當許多禍患和災難臨到他們的時候,這首歌就要成為指控他們的證據,因為這首歌要在他們的子孫中世代流傳。雖然我還沒有帶領他們進入我起誓應許之地,我已經知道他們的心思意念。」 22當天,摩西就寫下這首歌,傳授給以色列人。

23耶和華囑咐的兒子約書亞:「你要剛強勇敢,因為你要帶領以色列人進入我起誓應許他們的土地,我必與你同在。」

24摩西把這律法都寫在書上以後, 25就吩咐抬耶和華約櫃的利未人: 26「把這律法書放在你們的上帝耶和華的約櫃旁,作為指控你們的證據。 27因為我知道你們悖逆、頑固不化,我還活在你們中間的時候,你們尚且背叛上帝,何況我死後呢? 28把你們各支派的長老和首領招聚來,我要把這些話告訴他們,叫天地作證來指控他們。 29我知道,我死後你們會徹底墮落,偏離我吩咐你們行的道,做耶和華視為惡的事,惹祂發怒,將來禍患必臨到你們。」

30然後,摩西把這首詩歌從頭到尾讀給以色列全體會眾聽。