Jina Jipya La Sayuni
1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza,
kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia,
mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko,
wokovu wake kama mwanga wa moto.
262:2 Isa 1:26; Za 67:2; Ufu 3:12; Mwa 32:28; Ufu 2:7; Es 4:14; Za 50:12Mataifa wataona haki yako,
nao wafalme wote wataona utukufu wako;
wewe utaitwa kwa jina jipya
lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka.
362:3 Zek 9:16; 1The 2:19; Isa 28:5Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana,
taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako.
462:4 Law 26:43; 1Pet 2:10; Hos 2:19; Yer 3:14; Sef 3:17; Mal 3:12; Isa 6:12; 54:6Hawatakuita tena Aliyeachwa,
wala nchi yako kuiita Ukiwa.
Bali utaitwa Hefsiba,62:4 Hefsiba maana yake Yeye ninayemfurahia.
nayo nchi yako itaitwa Beula,62:4 Beula maana yake Aliyeolewa.
kwa maana Bwana atakufurahia,
nayo nchi yako itaolewa.
562:5 Kum 28:63; Wim 3:11; Isa 65:19; Yer 31:12; Sef 3:17Kama vile kijana aoavyo mwanamwali,
ndivyo wanao62:5 Au: wajenzi wako. watakavyokuoa wewe;
kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake,
ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
662:6 Eze 3:17; Ebr 13:17; Isa 52:8; Za 132:4Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu,
hawatanyamaza mchana wala usiku.
Ninyi wenye kumwita Bwana,
msitulie,
762:7 Mt 15:21-28; Sef 3:20; Lk 18:1-8; Isa 60:18; Kum 26:19msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu
na kuufanya uwe sifa ya dunia.
862:8 Kum 28:30-33; Yer 5:17; Mwa 22:16; Isa 14:25; 49:18Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume
na kwa mkono wake wenye nguvu:
“Kamwe sitawapa tena adui zenu
nafaka zenu kama chakula chao;
kamwe wageni hawatakunywa tena
divai mpya ambayo mmeitaabikia,
9lakini wale waivunao nafaka wataila
na kumsifu Bwana,
nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake
katika nyua za patakatifu pangu.”
1062:10 Isa 11:10-16; 57:14; Za 24:7; Isa 60:11Piteni, piteni katika malango!
Tengenezeni njia kwa ajili ya watu.
Jengeni, jengeni njia kuu!
Ondoeni mawe.
Inueni bendera kwa ajili ya mataifa.
1162:11 Amo 9:14; Kum 12:7; Yoe 2:26; Isa 1:10Bwana ametoa tangazo
mpaka miisho ya dunia:
“Mwambie Binti Sayuni,
‘Tazama, mwokozi wako anakuja!
Tazama ujira wake uko pamoja naye,
na malipo yake yanafuatana naye!’ ”
1262:12 Za 9:14; Mt 21:5; Isa 35:4; Ufu 22:12; Kum 30:4; Zek 9:9; Isa 40:10Wataitwa Watu Watakatifu,
Waliokombolewa na Bwana;
nawe utaitwa Aliyetafutwa,
Mji Usioachwa Tena.