Wokovu Kwa Ajili Ya Wengine
156:1 Yer 22:3; Rum 13:11; Za 85:9; Dan 9:24; Yer 23:6; Isa 26:8Hili ndilo asemalo Bwana:
“Dumisheni haki
na mkatende lile lililo sawa,
kwa maana wokovu wangu u karibu
na haki yangu itafunuliwa upesi.
256:2 Kut 20:8-10; Isa 58:3; Za 119:2Amebarikiwa mtu yule atendaye hili,
mtu yule alishikaye kwa uthabiti,
yeye ashikaye Sabato bila kuinajisi,
auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.”
356:3 Law 21:20; Mdo 8:27; Kut 12:43; 1Fal 8:41; Zek 8:20-23; Yer 38:7; Kum 23:3Usimwache mgeni aambatanaye na Bwana aseme,
“Hakika Bwana atanitenga na watu wake.”
Usimwache towashi yeyote alalamike akisema,
“Mimi ni mti mkavu tu.”
456:4 Yer 38:7; Kut 31:13Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa matowashi washikao Sabato zangu,
ambao huchagua kile kinachonipendeza
na kulishika sana agano langu:
556:5 1Tim 5:13; Isa 60:18; 48:19; 55:13; Ufu 3:12; Hes 32:42; 1Sam 15:12; Isa 47:3hao nitawapa ndani ya Hekalu langu na kuta zake
kumbukumbu na jina bora
kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike:
nitawapa jina lidumulo milele,
ambalo halitakatiliwa mbali.
656:6 1Nya 22:2; Isa 61:5; Kut 12:43; 1Fal 8:41; Isa 60:7-10Wageni wanaoambatana na Bwana
ili kumtumikia,
kulipenda jina la Bwana,
na kumwabudu yeye,
wote washikao Sabato bila kuinajisi
na ambao hushika sana agano langu:
756:7 Eze 20:40; Rum 12:1; Isa 19:21; Flp 4:18; Mt 21:13; Mk 11:17; Isa 19:21; Lk 19:46hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu
na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala.
Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao
zitakubalika juu ya madhabahu yangu;
kwa maana nyumba yangu itaitwa
nyumba ya sala kwa mataifa yote.”
856:8 Eze 34:12; Yn 10:16; Efe 1:10; Kum 30:4; Isa 11:12; 60:3-11Bwana Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye
Waisraeli waliohamishwa:
“Bado nitawakusanya wengine kwao
zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”
Mashtaka Ya Mungu Dhidi Ya Waovu
956:9 Yer 12:9; Eze 34:5-8; Isa 18:6; Eze 39:17-20Njooni, enyi wanyama wote wa kondeni,
njooni mle, ninyi wanyama wote wa mwituni!
1056:10 Mt 15:14; Eze 3:17; Nah 3:18; Isa 52:8; 62:6; Yer 6:17; 31:6; 14:13-14Walinzi wa Israeli ni vipofu,
wote wamepungukiwa na maarifa;
wote ni mbwa walio bubu,
hawawezi kubweka;
hulala na kuota ndoto,
hupenda kulala.
1156:11 Yer 23:1; 8:10; Eze 34:2; Mik 3:11; Isa 53:6; Hos 4:7-8; Isa 57:17Ni mbwa wenye tamaa kubwa,
kamwe hawatosheki.
Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu;
wote wamegeukia njia yao wenyewe,
kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.
1256:12 Za 10:6; Lk 12:18-19; Law 10:9; Mit 23:20; Isa 42:25Kila mmoja hulia, “Njooni, tupate mvinyo!
Tunywe kileo sana!
Kesho itakuwa kama leo,
au hata bora zaidi.”