Dhambi Ya Israeli Na Utii Wa Mtumishi
150:1 Kum 24:1; Mk 10:4; Mt 18:25; Amu 3:8; Hos 2:2; Mt 19:7; Neh 5:5; Isa 1:25Hili ndilo asemalo Bwana:
“Iko wapi hati ya talaka ya mama yako
ambayo kwayo niliachana naye?
Au nimewauza ninyi kwa nani
miongoni mwa watu wanaonidai?
Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa,
kwa sababu ya makosa, mama yenu aliachwa.
250:2 Mwa 18:14; Kut 14:22; Hes 11:23; 1Sam 8:19; Isa 41:28; Za 68:35; Yer 14:9Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja?
Nilipoita, kwa nini hakuwepo hata mmoja wa kujibu?
Je, mkono wangu ni mfupi mno hata nisiweze kuwakomboa?
Je, mimi sina nguvu za kukuokoa?
Kwa kukemea tu naikausha bahari,
naigeuza mito ya maji kuwa jangwa;
samaki wake wanaoza kwa kukosa maji
na kufa kwa ajili ya kiu.
350:3 Isa 5:30; Ufu 6:12; Kut 10:21Ninalivika anga weusi na kufanya nguo ya gunia
kuwa kifuniko chake.”
450:4 Kut 4:11-12; Za 88:13; Mt 7:29; Isa 40:29; Mt 11:28Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa,
ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka.
Huniamsha asubuhi kwa asubuhi,
huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.
550:5 Isa 35:5; Eze 2:8; Ebr 10:5; Isa 48:16; Eze 24:3; Mdo 26:19; Mt 26:39Bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu,
nami sikuwa mwasi,
wala sikurudi nyuma.
650:6 Mt 27:30; Isa 53:5; Mao 3:30; Hes 12:14; Mt 26:67; Mk 14:65Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao,
mashavu yangu wale wangʼoao ndevu zangu;
sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha
na kutemewa mate.
750:7 Isa 41:10; Rum 8:31; Eze 3:8-9; Isa 48:16; 28:16; 29:22Kwa sababu Bwana Mwenyezi ananisaidia,
sitatahayarika.
Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la gumegume,
nami ninajua sitaaibika.
850:8 Ay 13:19; Rum 8:32-34; 1Kor 4:4; Isa 26:2; 49:4Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu.
Ni nani basi atakayeleta mashtaka dhidi yangu?
Tukabiliane uso kwa uso!
Mshtaki wangu ni nani?
Ni nani aliye mshtaki wangu?
950:9 Ay 13:28; Isa 41:10; Ebr 1:11-12; Rum 8:1, 34; Isa 51:8Ni Bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi.
Ni nani huyo atakayenihukumu?
Wote watachakaa kama vazi,
nondo watawala wawamalize.
1050:10 2Nya 20:20; Isa 49:3; 26:4; 1:19; Hag 1:12; Mdo 26:18; Isa 10:20Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana,
na kulitii neno la mtumishi wake?
Yeye atembeaye gizani,
yeye asiye na nuru,
na alitumainie jina la Bwana,
na amtegemee Mungu wake.
1150:11 Mit 26:18; Yak 3:6; Ay 15:20; Isa 65:13-15; Kum 21:22-23Lakini sasa, ninyi nyote mnaowasha mioto,
na kupeana mienge iwakayo ninyi kwa ninyi,
nendeni, tembeeni katika nuru ya moto wenu
na ya mienge mliyoiwasha.
Hili ndilo mtakalolipokea kutoka mkononi mwangu:
Mtalala chini kwa mateso makali.