Unabii Dhidi Ya Babeli
1Neno kuhusu Jangwa kando ya Bahari:
Kama upepo wa kisulisuli unaopita katika nchi hadi kusini,
mshambuliaji anakuja kutoka jangwani,
kutoka nchi inayotisha.
221:2 1Sam 24:13-16; Mwa 10:22; Za 60:3; Yer 49:34; Isa 22:6; 13:3; Yer 25:25Nimeonyeshwa maono ya kutisha:
Msaliti anasaliti, mteka nyara anateka nyara.
Elamu, shambulia! Umedi, izunguke kwa jeshi!
Nitakomesha huzuni zote alizosababisha.
321:3 Mwa 3:16; Yn 16:2; Ay 14:22; Za 48:6; Isa 26:17; Yer 30:6; Dan 7:28Katika hili mwili wangu umeteswa na maumivu,
maumivu makali ya ghafula yamenishika,
kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa.
Nimeduwazwa na lile ninalolisikia,
nimeshangazwa na lile ninaloliona.
421:4 Isa 7:4; 35:4; 13:8; Dan 5:9; Za 55:5Moyo wangu unababaika,
woga unanifanya nitetemeke,
gizagiza la jioni nililolitamani sana,
limekuwa hofu kuu kwangu.
521:5 Yer 25:16, 27; Dan 5:2-5; Isa 5:12; 23:7; Yer 46:3; 1Sam 1:21Wanaandaa meza,
wanatandaza mazulia,
wanakula, wanakunywa!
Amkeni, enyi maafisa,
zitieni ngao mafuta!
621:6 2Fal 9:17Hili ndilo Bwana analoniambia:
“Nenda, weka mlinzi,
na atoe taarifa ya kile anachokiona.
721:7 Amu 6:5; Isa 21:9Anapoona magari ya vita
pamoja na kundi la farasi,
wapanda punda au wapanda ngamia,
na awe macho, awe macho kikamilifu.”
821:8 Mik 7:7; Hab 2:1Naye mlinzi alipaza sauti,
“Mchana baada ya mchana, bwana wangu, ninasimama katika mnara wa ulinzi,
kila usiku ninakaa mahali pangu nilipoamriwa.
921:9 Isa 13:19; Ufu 14:8; Dan 5:30; Ufu 18:2; Yer 50:2; Isa 47:11; Yer 51:8Tazama, yuaja mtu anayepanda gari la vita
pamoja na kundi la farasi.
Naye anajibu:
‘Babeli umeanguka, umeanguka!
Vinyago vyote vya miungu yake
vimelala chini vikiwa vimevunjwa!’ ”
1021:10 Yer 51:33; Mt 3:12; Mik 4:13; Isa 27:12; Hab 3:12Ee watu wangu, mliopondwa kwenye sakafu ya kupuria,
ninawaambia kile nilichokisikia
kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote,
kutoka kwa Mungu wa Israeli.
Unabii Dhidi Ya Edomu
1121:11 Mwa 32:3; 1Nya 1:30; Eze 35:2; Oba 1:1Neno kuhusu Duma:
Mtu fulani ananiita kutoka Seiri,
“Mlinzi, usiku utaisha lini?
Mlinzi, usiku utaisha lini?”
12Mlinzi anajibu,
“Asubuhi inakuja, lakini pia usiku.
Kama ungeliuliza, basi uliza;
bado na urudi tena.”
Unabii Dhidi Ya Arabia
1321:13 Isa 13:1; 2Nya 9:14; Mwa 10:7; 25:3; 1Nya 1:9Neno kuhusu Arabia:
Enyi misafara ya Wadedani,
mnaopiga kambi katika vichaka vya Arabia,
1421:14 Mwa 25:15; Ay 6:19leteni maji kwa wenye kiu,
ninyi mnaoishi Tema,
leteni chakula kwa ajili ya wakimbizi.
1521:15 Isa 13:14; 31:8Wanaukimbia upanga,
kutoka upanga uliochomolewa alani,
kutoka upinde uliopindwa,
na kutoka kwenye joto la vita.
1621:16 Law 25:50; Mwa 25:13; 25:13; Isa 17:3; 16:14; Za 120:5; Law 25:50; Wim 1:5; Mwa 25:13Hili ndilo Bwana analoniambia: “Katika muda wa mwaka mmoja, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, majivuno yote ya Kedari yatafikia mwisho. 1721:17 Hes 23:19; Kum 4:27; Isa 10; 19; 1:20; 16:14; Lk 21:33; 1Sam 15:29; Mt 24:35; Mk 13:31; 1Pet 1:25Wanaume wavutao pinde walionusurika, mashujaa wa Kedari, watakuwa wachache.” Bwana, Mungu wa Israeli, amesema.