Isaya 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 17:1-14

Neno Dhidi Ya Dameski

117:1 Yer 49:23; Mdo 9:2; Kum 13:16; Zek 9:1; Mwa 14:15; Isa 25:2Neno kuhusu Dameski:

“Tazama, Dameski haitakuwa tena mji

bali itakuwa lundo la magofu.

217:2 Yer 7:33; Mik 4:4; Isa 5:17; 2Fal 10:33; Isa 7:21; 27:10; Eze 25:5; Law 26:6Miji ya Aroeri itaachwa

na itaachiwa mifugo ambayo italala huko,

bila yeyote wa kuyaogopesha.

317:3 Isa 7:8, 16; 21:16; Hos 9:11; Isa 8:4; Hos 10:14; Isa 25:2, 12Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu,

nao uweza wa ufalme kutoka Dameski;

mabaki ya Aramu yatakuwa

kama utukufu wa Waisraeli,”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

417:4 Isa 2:11; 10:16“Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia,

unono wa mwili wake utadhoofika.

517:5 Yoe 3:13; Mt 13:30; Ufu 14:15-19; Isa 33:4; Yer 51:33; Ay 24:24; Yos 17:1517:5 Yos 17:15; 1Nya 11:15Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka

na kuvuna nafaka kwa mikono yake,

kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke

katika Bonde la Warefai.

617:6 Kum 4:24; Isa 10:19; 27:12; 24:3Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki,

kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa,

kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni,

nne au tano katika matawi yazaayo sana,”

asema Bwana, Mungu wa Israeli.

717:7 Isa 9:13; 12:6; Zek 12:10; Mik 7:7; Isa 2:12; 10:20; Za 95:6Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao,

na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli.

817:8 2Nya 32:19; Ufu 9:20; 2Fal 17:10Hawataziangalia tena madhabahu,

kazi za mikono yao,

nao hawataheshimu nguzo za Ashera,17:8 Ashera hapa maana yake ni mungu mke aliyekuwa akiabudiwa pamoja na Baali.

na madhabahu za kufukizia uvumba zilizofanywa kwa mikono yao.

917:9 Isa 7:19Katika siku ile miji yao iliyo imara, ambayo waliihama kwa sababu ya Waisraeli, itakuwa kama mahali palipoachwa pa vichaka na magugu. Nayo yote itakuwa ukiwa.

1017:10 Eze 22:12; Hos 8:14; Za 68:19; Kum 6:12; Yer 2:32; Za 50:22Mmemsahau Mungu Mwokozi wenu,

hamkumkumbuka Mwamba aliye ngome yenu.

Kwa hiyo, hata ingawa mlipandikiza mimea iliyo mizuri sana

na kuotesha mizabibu ya kigeni,

1117:11 Za 90:6; Ay 4:8; Kum 28:39; Yer 10:19; 30:12; Law 26:30hata kama siku ile unapoipandikiza, unaifanya iote

na asubuhi ile ile unayoipanda, unaifanya ichipue,

hata hivyo mavuno yatakuwa kama si kitu

katika siku ile ya ugonjwa na maumivu yasiyoponyeka.

1217:12 Yer 6:23; Lk 21:25; Isa 41:11; Za 18:4; 46:6; Isa 8:7-9Lo! Ghadhabu ya mataifa mengi,

wanaghadhibika kama bahari iliyochafuka!

Lo! Makelele ya mataifa

wanavuma kama ngurumo za maji mengi!

1317:13 Kum 28:20; Isa 13:14; Ay 13:25; Dan 2:35; Za 65:7; 46:3; Ay 21:18Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi,

wakati anapoyakemea yanakimbia mbali,

yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima,

kama jani livingirishwapo na dhoruba.

1417:14 2Fal 19:35; Amu 5:31; Isa 29:5; 30:13; 33:18; 54:14Wakati wa jioni, hofu ya ghafula!

Kabla ya asubuhi, wametoweka!

Hili ndilo fungu la wale wanaotupora,

fungu la wale wanaotunyangʼanya mali zetu.