Adhabu Kwa Israeli
19:1 Isa 22:12-13; 24:16; Za 73:27; Hos 7:14; 10:5; Mwa 30:15Usifurahie, ee Israeli;
usishangilie kama mataifa mengine.
Kwa kuwa hukuwa
mwaminifu kwa Mungu wako;
umependa ujira wa kahaba kwenye kila sakafu
ya kupuria nafaka.
29:2 Isa 24:7; Yoe 1:10; Hos 2:9Sakafu za kupuria nafaka na mashinikizo ya kukamulia divai
havitalisha watu,
divai mpya itawapungukia.
39:3 Kum 4:26-27; Amo 7:17; Eze 4:13; Hos 7:16; 8:13; 10:5; Law 25:23Hawataishi katika nchi ya Bwana,
Efraimu atarudi Misri
na atakula chakula
kilicho najisi huko Ashuru.
49:4 Yer 6:20; 16:7; Kum 26:14; Hos 8:13; Hag 2:13-14; Yoe 2:14; Eze 4:13-14Hawatammiminia Bwana sadaka ya divai
wala dhabihu zao hazitampendeza.
Dhabihu kama hizo zitakuwa kwao
kama mkate wa waombolezaji;
nao wote wazilao watakuwa najisi.
Chakula hiki kitakuwa kwa ajili yao wenyewe;
kisije katika Hekalu la Bwana.
59:5 Isa 10:3; Yer 5:31; Hos 2:11Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa,
katika siku za sikukuu za Bwana?
69:6 Isa 5:6; 19:13; Hos 7:11; 8:13; 10:8; Yer 42:22; Isa 32:13; 34:13Hata ikiwa wataokoka maangamizi,
Misri atawakusanya,
nayo Memfisi9:6 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. itawazika.
Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma,
nayo miiba itafunika mahema yao.
79:7 Mik 7:4; Lk 21:22; Yer 10:15; 16:18; 1Sam 10:11; Mao 2:14; Isa 34:8; 44:25; Ay 31:14; Eze 14:9-10Siku za adhabu zinakuja,
siku za malipo zimewadia.
Israeli na afahamu hili.
Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana
na uadui wenu ni mkubwa sana,
nabii anadhaniwa ni mpumbavu,
mtu aliyeongozwa na Mungu
anaonekana mwendawazimu.
89:8 Hos 5:1; Eze 22:26; Yer 6:17; 31:6; Eze 3:17; 35:7Nabii, pamoja na Mungu wangu,
ndiye mlinzi juu ya Efraimu,
hata hivyo mitego inamngojea
katika mapito yake yote,
na uadui katika nyumba ya Mungu wake.
99:9 Amu 19:16-30; Hos 4:9; 8:13; 10:9; Sef 3:7Wamezama sana katika rushwa,
kama katika siku za Gibea.
Mungu atakumbuka uovu wao
na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.
109:10 Hes 25:1-5; Za 106:28-29; Yer 11:13; Hos 4:14; Wim 2:13“Nilipompata Israeli, ilikuwa kama
kupata zabibu jangwani;
nilipowaona baba zenu, ilikuwa kama kuona
matunda ya kwanza katika mtini.
Lakini walipofika Baal-Peori, walijiweka wakfu
kwa ile sanamu ya aibu,
nao wakawa najisi
kama kitu kile walichokipenda.
119:11 Hos 4:7; 10:5; Isa 17:3Utukufu wa Efraimu utaruka kama ndege:
hakuna kuzaa, hakuna kuchukua mimba,
hakuna kutunga mimba.
129:12 Hos 7:13; Kum 31:17; Eze 24:21Hata wakilea watoto,
nitamuua kila mmoja.
Ole wao
nitakapowapiga kisogo!
139:13 Eze 27:3; Za 78:67; Ay 15:22; Mao 2:22Nimemwona Efraimu, kama Tiro,
aliyeoteshwa mahali pazuri.
Lakini Efraimu wataleta
watoto wao kwa mchinjaji.”
149:14 Lk 23:29; Hos 9:11; Lk 23:29Wape, Ee Bwana,
je, utawapa nini?
Wape matumbo ya kuharibu mimba
na matiti yaliyokauka.
159:15 Hos 4:9, 15; 5:2; 7:2; Isa 1:23; Yer 12:8“Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali,
niliwachukia huko.
Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi,
nitawafukuza katika nyumba yangu.
Sitawapenda tena,
viongozi wao wote ni waasi.
169:16 Hos 5:11; 8:7; Ay 15:32Efraimu ameharibiwa,
mzizi wao umenyauka,
hawazai tunda.
Hata kama watazaa watoto,
nitawachinja watoto wao
waliotunzwa vizuri.”
179:17 Hos 4:10; 7:13; Kum 28:65; Yer 6:30Mungu wangu atawakataa
kwa sababu hawakumtii;
watakuwa watu wa kutangatanga
miongoni mwa mataifa.