Shtaka Dhidi Ya Israeli
14:1 Mit 10:21; 24:2; Mik 6:2; Isa 1:3; Ay 10:2; Yer 2:9; 7:28; 51:5; Hos 2:20Sikieni neno la Bwana, enyi Waisraeli,
kwa sababu Bwana analo shtaka
dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi:
“Hakuna uaminifu, hakuna upendo,
hakuna kumjua Mungu katika nchi.
24:2 Isa 59:3; Hos 5:2; 6:2; 7:1; 11:12; Eze 22:2-9; 1Fal 21:16Kuna kulaani tu, uongo na uuaji,
wizi na uzinzi,
bila kuwa na mipaka,
nao umwagaji damu mmoja
baada ya mwingine.
34:3 Yer 4:25, 28; 9:10; Amo 8:8; Isa 15:6; 33:9; Sef 1:3Kwa sababu hii nchi huomboleza,
wote waishio ndani mwake wanadhoofika,
wanyama wa kondeni, ndege wa angani
na samaki wa baharini wanakufa.
44:4 Kum 17:12; Eze 3:26“Lakini mtu awaye yote na asilete shtaka,
mtu yeyote na asimlaumu mwenzake,
kwa maana watu wako ni kama wale
waletao mashtaka dhidi ya kuhani.
54:5 Eze 7:19; 14:7; Hos 2:2Unajikwaa usiku na mchana,
nao manabii hujikwaa pamoja nawe.
Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako:
64:6 Mit 10:21; Hos 2:13; 8:1-12; Mal 2:7-8watu wangu wanaangamizwa
kwa kukosa maarifa,
“Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,
mimi nami nitakukataa wewe
usiwe kuhani kwangu mimi;
kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako
mimi nami sitawajali watoto wako.
74:7 Hab 2:16; Hos 9:11; 13:6Kadiri makuhani walivyoongezeka,
ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu,
walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu.
84:8 Isa 56:11; Mik 3:11; Hos 14:1Hujilisha dhambi za watu wangu
na kupendezwa na uovu wao.
94:9 Isa 24:2; Yer 5:31; Hos 8:13; 10:10; 12:2Hata itakuwa: Kama walivyo watu,
ndivyo walivyo makuhani.
Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zao
na kuwalipa kwa matendo yao.
104:10 Mik 6:14; Isa 55:2; Hos 7:14; 9:17; Eze 22:9; Law 26:26“Watakula lakini hawatashiba;
watajiingiza katika ukahaba
lakini hawataongezeka,
kwa sababu wamemwacha Bwana
na kujiingiza wenyewe
114:11 Isa 28:7; Hos 5:4; Mit 20:1; Law 10:9; 1Sam 25:36katika ukahaba,
divai ya zamani na divai mpya,
ambavyo huondoa ufahamu
124:12 Yer 2:27; Ufu 17:2; Hab 2:19; Isa 44:20; Hes 15:39; Za 73:27wa watu wangu.
Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti
nao hujibiwa na fimbo ya mti.
Roho ya ukahaba imewapotosha,
hawana uaminifu kwa Mungu wao.
134:13 Isa 1:28; Hos 2:13; 10:9; Yer 2:20; Amo 7:17; Rum 1:28Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima
na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima,
chini ya mialoni, milibua na miela,
ambako kuna vivuli vizuri.
Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba
na wake za wana wenu uzinzi.
144:14 Mwa 38:21; Hos 9:10; Mit 10:21“Sitawaadhibu binti zenu wakati
wanapogeukia ukahaba,
wala wake za wana wenu
wanapofanya uzinzi,
kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya
na kutambikia pamoja na makahaba
wa mahali pa kuabudia miungu:
watu wasiokuwa na ufahamu
wataangamia!
154:15 Hos 9:15; 12:11; Amo 4:4; Yos 7:2“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli,
Yuda naye asije akawa na hatia.
“Usiende Gilgali,
usipande kwenda Beth-Aveni4:15 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.
Wala usiape,
‘Hakika kama Bwana aishivyo!’
164:16 Isa 5:17; 7:25; Kut 32:9; Yer 31:18Waisraeli ni wakaidi,
kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi.
Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga
kama wana-kondoo
katika shamba la majani?
174:17 Mt 15:14Efraimu amejiunga na sanamu,
ondokana naye!
184:18 Mik 3:11; 7:3Hata wakati wamemaliza vileo vyao
wanaendelea na ukahaba wao,
watawala wao hupenda sana
njia za aibu.
194:19 Hos 12:11; 13:15; Isa 1:29Kisulisuli kitawafagilia mbali
na dhabihu zao zitawaletea aibu.