Hesabu 12 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 12:1-16

Miriamu Na Aroni Wampinga Mose

112:1 Kut 15:20; 2:21Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 212:2 Hes 16:3; 11:1; Mwa 29:33; Mik 6:4; 2Fal 19:4; Za 94:9; Eze 35:12Waliuliza, “Je, Bwana amesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” Naye Bwana akasikia hili.

312:3 Mt 11:29; 1Tim 6:11; 2Tim 2:25; Za 149:4; 1Pet 3:4(Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)

4Ghafula Bwana akawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njooni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda. 512:5 Kut 13:21; Hes 11:25; Kut 34:5Kisha Bwana akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele, 612:6 1Sam 3:7, 21; Mwa 15:1; 20:3; 46:2; Mt 27:19; Ebr 1:1; 1Fal 3:5; Mwa 46:2; Ay 33:15; Lk 1:11; 1:22; Mt 1:20Bwana akasema, “Sikilizeni maneno yangu:

“Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu,

nitajifunua kwake kwa maono,

nitanena naye katika ndoto.

712:7 Kum 34:5; Yos 1:1-2; Za 105:26; Ebr 3:2, 5Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;

yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

812:8 Amu 14:12; 1Fal 10:1; Za 17:15; 49:4; 140:13; Mit 1:6; Dan 5:12; Kut 20:4; 24:2; Ay 19:26; Isa 6:1Kwake nitanena naye uso kwa uso,

waziwazi wala si kwa mafumbo;

yeye ataona umbo la Bwana.

Kwa nini basi ninyi hamkuogopa

kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”

912:9 Kut 4:14; Mwa 17:22Hasira ya Bwana ikawaka dhidi yao, akawaacha.

1012:10 Kut 4:6; 40:2; Kum 24:9; Law 13:11; 2Fal 5:1, 27; 2Nya 16:12; 21:12Wakati hilo wingu liliinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia, akaona ana ukoma. 1112:11 2Sam 19:19; 24:10Kisha Aroni akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu. 1212:12 Za 88:4; Efe 2:1-5; Kol 2:13; 1Tim 5:6Usimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”

1312:13 Kut 15:26; Za 6:2; 147:3; Isa 1:6; 30:26; 53:5; Yer 17:14; Hos 6:1Hivyo Mose akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”

1412:14 Kum 25:9; Ay 17:6; 30:9-10; Isa 50:6; Law 13:46; Hes 5:2-3; Ebr 12:9; 2Nya 26:20, 21Bwana akamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.” 1512:15 Law 14:8; 13; Kum 24:9Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.

1612:16 Hes 10:12; 11:35; 15:32; Mwa 21:21Baada ya hayo, watu waliondoka Haserothi, wakapiga kambi katika Jangwa la Parani.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

民数记 12:1-16

米利暗受罚

1米利暗亚伦摩西娶了一个古实的女子而批评他,说: 2“难道耶和华只借着摩西说话吗?祂不也借着我们说话吗?”耶和华听见了这话。 3其实摩西为人十分谦和,比世上任何人都谦和。 4耶和华突然对摩西亚伦米利暗说:“你们三人都出来到会幕去。”他们就去了。 5耶和华在云柱中降临,站在会幕门口呼唤亚伦米利暗,二人就走到前面。 6耶和华说:“你们听我说,你们中间若有先知,我耶和华必在异象中向他显现,在梦中跟他说话。 7但我不是这样对待我的仆人摩西,他在我家里忠信可靠, 8我跟他面对面说话,清清楚楚,不用谜语,他看得见我的形象。你们怎敢批评我的仆人摩西?” 9耶和华向他们发怒,然后离去。 10云彩从会幕上离开的时候,米利暗身上患了麻风病,像雪一样白。亚伦见状, 11便对摩西说:“我主啊,求你不要因我们愚昧犯罪而惩罚我们。 12求你不要让她像那一出母腹便半身腐烂的死胎。” 13于是,摩西呼求耶和华:“上帝啊,求你医治她!” 14耶和华对摩西说:“如果她父亲在她脸上吐唾沫,她岂不也要蒙羞七天吗?现在把她关在营外,七天后再让她回来。” 15于是,米利暗被关在营外七天,民众等她回营后才继续前行。 16他们离开哈洗录,到巴兰旷野安营。