Ezra 8 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ezra 8:1-36

Orodha Ya Viongozi Wa Jamaa Waliorudi Na Ezra

18:1 Ezr 7:7Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta:

28:2 1Nya 3:22wa wazao wa Finehasi, alikuwa Gershoni;

wa wazao wa Ithamari, alikuwa Danieli;

wa wazao wa Daudi, alikuwa Hatushi 38:3 1Nya 3:22; Ezr 2:3wa wazao wa Shekania;

wa wazao wa Paroshi, alikuwa Zekaria, na watu 150 walioandikishwa pamoja naye;

48:4 Ezr 2:6wa wazao wa Pahath-Moabu, alikuwa Eliehoenai mwana wa Zerahia na wanaume 200 pamoja naye;

5wa wazao wa Zatu, alikuwa Shekania mwana wa Yahazieli na wanaume 300 pamoja naye;

68:6 Ezr 2:15; Neh 7:20wa wazao wa Adini, alikuwa Ebedi mwana wa Yonathani na wanaume 50 pamoja naye;

7wa wazao wa Elamu, alikuwa Yeshaya mwana wa Athalia, na wanaume 70 pamoja naye;

8wa wazao wa Shefatia, alikuwa Zebadia mwana wa Mikaeli na wanaume 80 pamoja naye;

9wa wazao wa Yoabu, alikuwa Obadia mwana wa Yehieli na wanaume 218 pamoja naye;

10wa wazao wa Bani, alikuwa Shelomithi mwana wa Yosifia na wanaume 160 pamoja naye;

11wa wazao wa Bebai, alikuwa Zekaria mwana wa Bebai na wanaume 28 pamoja naye;

12wa wazao wa Azgadi, alikuwa Yohanani mwana wa Hakatani na wanaume 110 pamoja naye;

138:13 Ezr 2:13wa wazao wa Adonikamu, hawa walikuwa wa mwisho ambao majina yao ni Elifeleti, Yeueli, Shemaya na wanaume 60 pamoja nao;

14wa wazao wa Bigwai, walikuwa Uthai na Zakuri na wanaume 70 pamoja nao.

Kurudi Yerusalemu

158:15 Ezr 2:40; 7:7; Mdo 16:13; 20:28; Za 137:1; Mit 27:23; Ebr 13:17; Ezr 7:7; Hes 8:1Niliwakusanya kwenye mto utiririkao kuelekea Ahava, nasi tukapiga kambi pale siku tatu. Wakati nilipokagua kati ya watu na makuhani, sikuwapata Walawi. 16Basi niliwaita Eliezeri, Arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu, Elnathani, Nathani, Zekaria na Meshulamu waliokuwa viongozi na Yoyaribu na Elnathani waliokuwa wasomi, 178:17 Ezr 2:43nikawatuma kwa Ido kiongozi huko Kasifia. Niliwaambia watakayomwambia Ido na ndugu zake, watumishi wa Hekalu8:17 Yaani Wanethini (pia 8:20). huko Kasifia, ili waweze kutuletea wahudumu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. 188:18 Ezr 5:5Kwa sababu mkono wa neema wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, walituletea Sherebia, mtu mwenye uwezo kutoka wazao wa Mahli mwana wa Lawi, mwana wa Israeli, na wana wa Sherebia pamoja na ndugu zao wanaume kumi na wanane. 19Naye Hashabia, pamoja na Yeshaya kutoka wazao wa Merari na ndugu zake na wapwa wake wanaume ishirini. 208:20 1Nya 9:2; Ezr 2:43Vilevile walileta watumishi wa Hekalu 220, kikundi ambacho Daudi na maafisa walikuwa wamekiweka kusaidia Walawi. Wote walikuwa wameorodheshwa kwa majina.

218:21 2Nya 9:2; Ezr 2:438:21 2Nya 20:3; Za 27:11; Law 16:29; Za 5:8; 2Nya 20:3; Law 16:29; Isa 58:3-5Kando ya Mto Ahava, hapo nilitangaza kufunga, ili tujinyenyekeshe mbele za Mungu wetu na kumwomba kwa ajili ya kutujalia safari ya amani sisi na watoto wetu, pamoja na mali zetu zote. 228:22 Neh 2:9; Yer 41:16; Kum 31:17; 2Nya 15:2; 1Kor 9:15; 1Nya 28:9; Ezr 7:6-9; Za 33:18-19; Isa 3:10; Rum 8:28; 1Pet 3:12; Za 34:16; 2Nya 15:2Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.” 238:23 2Nya 33:13; Kum 4:29; Mdo 14:23; 1Nya 5:20; Isa 19:22; Yer 29:12-13Kwa hiyo tulifunga na kumwomba Mungu wetu kuhusu jambo hili, naye akajibu maombi yetu.

24Kisha niliwatenga viongozi wa makuhani kumi na wawili, pamoja na Sherebia, Hashabia na ndugu zao kumi, 258:25 Ezr 7:15-16nami nikawapimia fedha, dhahabu na vifaa ambavyo mfalme, washauri wake, maafisa wake na Israeli wote waliokuwepo walikuwa wamevitoa sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. 26Niliwapimia talanta 6508:26 Talanta 650 za fedha ni sawa na tani 25. za fedha, vifaa vingine vya fedha vya uzito wa talanta mia moja,8:26 Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75. talanta mia moja za dhahabu, 27mabakuli ishirini ya dhahabu ya thamani ya darkoni elfu moja,8:27 Darkoni 1,000 ni sawa na kilo 8.5. na vyombo viwili vya shaba iliyosuguliwa, ya thamani kama dhahabu.

288:28 Kum 33:8; Law 21:6; 22:2-3; 2Nya 24:14; Hes 4:4; Isa 52:11; 1Nya 23:28Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu. 298:29 1Nya 26:20-26; Lk 12:38-39Vilindeni kwa uangalifu mpaka mtakapovipima ndani ya vyumba vya nyumba ya Bwana katika Yerusalemu mbele ya makuhani, viongozi na Walawi pamoja na wakuu wa jamaa za Israeli.” 30Ndipo makuhani na Walawi wakapokea fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu ambavyo vilipimwa na kupelekwa katika nyumba ya Mungu wetu mjini Yerusalemu.

318:31 Ay 5:19-24; Isa 41:10-14; Ezr 7:6-7, 28Tulianza safari kutoka Mto Ahava kwenda Yerusalemu kwenye siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza. Mkono wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, naye njiani alitulinda dhidi ya adui na wanyangʼanyi. 328:32 Mwa 40:13; Neh 2:11; Isa 56:6; 14:1Kwa hiyo tuliwasili Yerusalemu ambapo tulipumzika kwa siku tatu.

338:33 Neh 3:3, 21-24Katika siku ya nne, ndani ya nyumba ya Mungu wetu, tulipima fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu, tukakabidhi mikononi mwa kuhani Meremothi mwana wa Uria. Eleazari mwana wa Finehasi alikuwa pamoja naye, pia walikuwako Walawi wawili, Yozabadi mwana wa Yeshua na Noadia mwana wa Binui. 34Kila kitu kilihesabiwa kwa idadi na kupimwa kwa uzito, nao uzito wote uliandikwa wakati ule.

358:35 Law 1:3; 2Nya 29:21, 24; 30:24; Ezr 6:17Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo dume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi dume kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Bwana. 368:36 Ezr 7:21-24; Zek 8:1-23; Es 9:3Pia walikabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa Ngʼambo ya Mto Frati maagizo ya mfalme, ambao baadaye walitoa msaada kwa watu na kwa nyumba ya Mungu.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以斯拉记 8:1-36

归回之人

1亚达薛西王年间,与我一起从巴比伦上到耶路撒冷之人的族长和家谱如下: 2非尼哈的子孙有革顺以他玛的子孙有但以理大卫的子孙有哈突3巴录的后裔、示迦尼的子孙有撒迦利亚及一百五十名与他一同记入族谱的男子; 4巴哈·摩押的子孙有西拉希雅的儿子以利约乃及二百名男子; 5萨土8:5 “萨土”参照《七十士译本》,希伯来文无此字。的子孙有雅哈悉的儿子示迦尼及三百名男子; 6亚丁的子孙有约拿单的儿子以别及五十名男子; 7以拦的子孙有亚他利雅的儿子耶筛亚及七十名男子; 8示法提雅的子孙有米迦勒的儿子西巴第雅及八十名男子; 9约押的子孙有耶歇的儿子俄巴底亚及二百一十八名男子; 10巴尼8:10 “巴尼”参照《七十士译本》,希伯来文无此字。的子孙有约细斐的儿子示罗密及一百六十名男子; 11比拜的子孙有比拜的儿子撒迦利亚及二十八名男子; 12押甲的子孙有哈加坦的儿子约哈难及一百一十名男子; 13稍后归回的亚多尼干的子孙有以利法列耶利示玛雅及六十名男子; 14比革瓦伊的子孙有乌太撒刻及七十名男子。

以斯拉为圣殿召集利未人

15我把他们召集在流往亚哈瓦的河边,我们在那里扎营三天。我察看民众和祭司,发现他们当中没有利未人。 16于是,我派人把首领以利以谢亚列示玛雅以利拿单雅立以利拿单拿单撒迦利亚米书兰及两位教师约雅立以利拿单叫来。 17我派他们去见迦西斐雅的首领易多,请他们告诉易多及其做殿役的亲族带一些人来我们上帝的殿里事奉。 18我们的上帝施恩帮助我们,他们给我们带来一位能干的人示利比及其弟兄和儿子共十八人。示利比以色列的儿子利未的后裔抹利的子孙。 19他们还带来哈沙比雅米拉利的子孙耶筛亚,以及哈沙比雅的弟兄和儿子共二十人。 20此外还有二百二十名殿役,他们都是被点名指派的。从前大卫和众官员曾指派殿役服侍利未人。

以斯拉带领百姓禁食

21然后,我在亚哈瓦河边宣布禁食,为要在我们的上帝面前谦卑下来,祈求祂保护我们、我们的儿女及财物一路平安。 22我羞于求王派步兵和骑兵沿途帮助我们御敌,因为我们曾经告诉王:“我们的上帝会施恩帮助寻求祂的人,但会向背弃祂的人发烈怒。” 23因此,我们为这事禁食、寻求我们的上帝,祂应允了我们。

献给圣殿的礼物

24我选出十二位祭司长:示利比哈沙比雅和他们的十个弟兄。 25王及其谋士和将领,以及所有在场的以色列人献给我们上帝殿的金银和器皿,我都秤了交给他们。 26我交给他们的有四十四万两银子、价值六万八千两银子的器皿、六万八千两金子、 27共重八公斤半的二十个金碗和两件贵重如金子的上等精铜器皿。 28我对他们说:“你们和这些器皿是献给耶和华的,金银是自愿献给你们祖先的上帝耶和华的礼物。 29你们要好好保管,护送到耶路撒冷耶和华殿的库房里,要在祭司长、利未人和以色列的各族长面前过秤。” 30于是,祭司和利未人接过这些称过的金、银和器皿,要带去耶路撒冷我们上帝的殿里。

返回耶路撒冷

31一月十二日,我们从亚哈瓦河边出发上耶路撒冷。我们的上帝施恩帮助我们,救我们脱离仇敌和路上埋伏之人的攻击。 32耶路撒冷后,我们休息了三天。 33第四天,我们在上帝的殿里把金银和器皿过秤,交给乌利亚的儿子米利末祭司。在场的还有非尼哈的儿子以利亚撒利未耶书亚的儿子约撒拔宾内的儿子挪亚底34每样东西都被数过、称过,其重量都被记录下来。

35从流亡之地归回的人又献燔祭给以色列的上帝,为全体以色列人献上十二头公牛、九十六只公绵羊和七十七只绵羊羔,并献上十二只公山羊作赎罪祭。这些都是献给耶和华的燔祭。 36他们将王的谕旨交给王的总督和幼发拉底河西的省长,众官员都为民众和上帝殿的工作提供帮助。