Ezekieli 6 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 6:1-14

Unabii Dhidi Ya Milima Ya Israeli

1Neno la Bwana likanijia kusema, 26:2 Eze 36:1; Mik 6:1; Eze 18:6; 4:7; 36:4; Law 26:30“Mwanadamu, elekeza uso wako kukabili milima ya Israeli, utabiri dhidi yake 3na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu. 46:4 2Nya 14:5; Yer 44:28; Eze 9:4; 14:3Madhabahu yenu yatabomolewa na madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatavunjavunjwa, nami nitawachinja watu wenu mbele ya sanamu zenu. 56:5 Hes 19:16; Za 53:5; Yer 8:1-2Nitazilaza maiti za Waisraeli mbele ya sanamu zao, nami nitatawanya mifupa yenu kuzunguka madhabahu yenu. 66:6 Mik 1:7; Zek 13:2; Law 26:30; Isa 6:11; 1Sam 5:4; Kut 12:20; Hos 10:8; Eze 30:13Popote mnapoishi, miji hiyo itafanywa ukiwa na mahali pa juu pa kuabudia miungu patabomolewa, ili madhabahu yenu ifanywe ukiwa na kuharibiwa, sanamu zenu zitavunjavunjwa na kuharibiwa, madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatabomolewa na kila mlichokifanya kitakatiliwa mbali. 76:7 Eze 9:7; 6:13; 7:4, 9; 11:10, 12; 12:15Watu wenu watachinjwa katikati yenu, nanyi mtatambua Mimi ndimi Bwana.

86:8 Za 68:20; 44:11; Yer 44:28; Mwa 11:4; Isa 6:13; Eze 7:16; 12:16; 14:22“ ‘Lakini nitawabakiza hai baadhi yenu, kwa kuwa baadhi yenu watanusurika kuuawa watakapokuwa wametawanyika katika nchi na mataifa. 96:9 Za 78:40; Yer 8:21; Isa 7:13; Mik 5:13; Kut 22:20; Ay 42:6; Eze 36:31Ndipo katika mataifa ambamo watakuwa wamechukuliwa mateka, wale ambao watanusurika watanikumbuka, jinsi ambavyo nimehuzunishwa na mioyo yao ya uzinzi, ambayo imegeukia mbali nami na macho yao ambayo yametamani sanamu zao. Watajichukia wenyewe kwa ajili ya uovu walioutenda na kwa ajili ya desturi zao za kuchukiza. 106:10 Zek 10:9; Eze 20:43; Kum 28:52; Yer 40:2Nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, sikuwaonya bure kuwa nitaleta maafa hayo yote juu yao.

116:11 Yer 42:22; Eze 22:13; 21:14-17; 25:6“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Piga makofi, kanyaga chini kwa mguu na upige kelele, “Ole!” kwa sababu ya maovu yote na machukizo yote yanayofanywa na nyumba ya Israeli, kwa kuwa wataanguka kwa upanga, njaa na tauni. 126:12 Eze 5:12; 7:15; Ay 20:23Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni, naye aliye karibu atauawa kwa upanga, naye yule atakayenusurika na kubaki atakufa kwa njaa. Hivyo ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu dhidi yao. 136:13 Isa 1:29; 57:5; Hos 4:13; Eze 18:6; Law 26:30; 1Fal 14:23; Yer 2:20; Eze 20:28Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, wakati maiti za watu wao zitakapokuwa zimelala katikati ya sanamu zao kuzunguka madhabahu yao, juu ya kila kilima kilichoinuka na juu ya vilele vyote vya milima, chini ya kila mti uliotanda na kila mwaloni wenye majani, yaani, sehemu walizofukizia uvumba kwa sanamu zao zote. 146:14 Kut 7:5; Ay 30:21; Eze 14:13; Isa 5:25; Yer 6:12; Eze 12:19; 20:34Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watakapojua ya kwamba Mimi ndimi Bwana.’ ”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

以西結書 6:1-14

責備以色列人拜偶像

1耶和華對我說: 2「人子啊,你要面向以色列的山嶺說預言,斥責它們, 3說,『以色列的山嶺啊,要聽主耶和華的話。祂對高山、丘陵、山澗、河谷說,我必親自讓刀劍臨到你們,我必毀滅你們的邱壇, 4使你們的祭壇荒廢,香壇破裂!我必把你們被殺的人扔到你們的偶像面前, 5使他們橫屍在你們的偶像面前,骸骨散在祭壇的四周。 6不論你們住在哪裡,你們的城邑必淪為廢墟,邱壇淪為荒場,祭壇荒廢,偶像被砸碎,香壇被搗毀,一切必化為烏有。 7被殺的人必橫屍你們中間,你們就知道我是耶和華。

8「『不過,我必為你們留下一些人,使他們脫離刀劍之災,四散到列國列邦。 9他們必在被擄的異地想起我怎樣為他們憂傷,因為他們背叛我,心中淫亂,眼中戀慕與偶像苟合。他們必因自己的一切邪惡行為而厭惡自己。 10這樣,他們就知道我是耶和華,我說要降災禍給他們並非空話。』」

11主耶和華說:「你要拍手頓足地呼喊,『唉!以色列人必因一切邪惡可憎的行為而倒在刀劍、饑荒和瘟疫之下。 12遠處的必死於瘟疫,近處的必喪身刀下,其餘被圍困的必死於饑荒。我必把烈怒傾倒在他們身上。 13他們必陳屍於祭壇周圍的偶像間,就是他們在各高崗上、山頂上、綠樹下和茂密的橡樹下燒香祭拜偶像的地方,那時他們必知道我是耶和華。 14我必伸手攻擊他們,使他們居住的地方都變得極其荒涼,從曠野一直到第伯拉他。這樣,他們便知道我是耶和華。』」