Danieli 7 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Danieli 7:1-28

Ndoto Ya Danieli Ya Wanyama Wanne

17:1 Yer 36:4; Dan 1:17; Eze 40:2; Za 4:4; Dan 4:13Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita mawazoni yake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake.

27:2 Eze 37:9; Dan 11:4; 8:8; Ufu 7:1Danieli akasema: “Katika maono yangu usiku nilitazama, na hapo mbele yangu kulikuwepo na upepo kutoka pande nne za mbingu, ukivuruga bahari kuu. 37:3 Ufu 13:1; Zek 6:1-4Wanyama wanne wakubwa, kila mmoja tofauti na mwenzake, wakajitokeza kutoka bahari.

47:4 Zek 7:2; Eze 17:3; Ufu 13:2; Yer 4:2; 2Fal 24:1; Yer 4:7“Mnyama wa kwanza alifanana na simba, naye alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikatazama mpaka mabawa yake yalipongʼolewa, naye akainuliwa katika nchi, akasimama kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa binadamu.

57:5 Dan 2:39“Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, ambaye alionekana kama dubu. Upande wake mmoja ulikuwa umeinuka, na alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama mpaka ushibe!’

67:6 Ufu 13:2“Baada ya huyo, nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama mwingine, aliyefanana na chui. Juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege. Mnyama huyu alikuwa na vichwa vinne, naye akapewa mamlaka ya kutawala.

7“Baada ya huyo, katika maono yangu usiku nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama wa nne, mwenye kutisha na kuogofya, tena mwenye nguvu nyingi. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; akapondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chini ya nyayo zake chochote kilichosalia. Alikuwa tofauti na wanyama wote waliotangulia, naye alikuwa na pembe kumi.

87:8 Dan 8:9; Ufu 9:7; Za 12:3; Ufu 13:5-6“Wakati nilipokuwa ninafikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ambayo ni ndogo, iliyojitokeza miongoni mwa zile kumi; pembe tatu za mwanzoni zilingʼolewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno.

97:9 Ufu 1:14; Eze 1:15; 10:6; 1Fal 22:19; 2Nya 18:18; Mt 19:28“Nilipoendelea kutazama,

“viti vya enzi vikawekwa,

naye Mzee wa Siku akaketi.

Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji;

nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu.

Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto,

nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto.

107:10 Za 50:3; Isa 30:27; Kum 33:2; Yud 14; Ufu 5:11; Kut 32:32; Ufu 20:11-15Mto wa moto ulikuwa unatiririka,

ukipita mbele yake.

Maelfu elfu wakamhudumia;

kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake.

Mahakama ikakaa kuhukumu,

na vitabu vikafunguliwa.

117:11 Ufu 19:20; 13:5-6“Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia mpaka yule mnyama alipouawa, na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto uliowaka. 12(Wanyama wengine walikuwa wamevuliwa mamlaka yao, lakini waliruhusiwa kuishi kwa muda fulani.)

137:13 Eze 1:26; Mt 8:20; 24:30; Kum 33:26; Ufu 1:13; 14:14; Isa 13:6“Katika maono yangu ya usiku nilitazama, na mbele yangu nikamwona anayefanana na mwanadamu, akija pamoja na mawingu ya mbinguni. Akamkaribia huyo Mzee wa Siku, na akaongozwa mbele zake. 147:14 Yn 3:35; Ebr 12:28; Dan 2:44; Mt 28:18; Efe 1:22; Za 72:11; Isa 16:5Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu; nao watu wa kabila zote, mataifa, na watu wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa.

Tafsiri Ya Ndoto

157:15 Ay 4:15; Dan 4:19“Mimi, Danieli, nilipata mahangaiko rohoni, nayo maono yale yaliyopita ndani ya mawazo yangu yalinisumbua. 167:16 Dan 9:22; Zek 1:9; Dan 8:16Nikamkaribia mmoja wa wale waliosimama pale na kumuuliza maana halisi ya haya yote.

“Basi akaniambia na kunipa tafsiri ya vitu hivi: 17‘Hao wanyama wanne wakubwa ni falme nne zitakazoinuka duniani. 187:18 Isa 60:12-14; Lk 12:32; Za 16; 3; 49:14; Ebr 12:28Lakini watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana watapokea ufalme na kuumiliki milele: naam, milele na milele.’

19“Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, ambaye alikuwa tofauti na wale wengine wote, tena wa kutisha sana, na meno yake ya chuma na makucha ya shaba: mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chochote kilichosalia. 207:20 Ufu 17:12; 13:5-6Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake, na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho zaidi kuliko zile nyingine, na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno. 217:21 Ufu 13:7; 11:7Nilipoendelea kutazama, pembe hii ilikuwa inapigana vita dhidi ya watakatifu na kuwashinda, 227:22 Mk 8:35mpaka huyo Mzee wa Siku alipokuja na kutamka hukumu kwa kuwapa ushindi watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana, na wakati ukawadia walipoumiliki ufalme.

237:23 Dan 2:40“Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote, nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda. 247:24 Ufu 17:12Zile pembe kumi ni wafalme kumi watakaotokana na ufalme huu. Baada yao mfalme mwingine atainuka, ambaye atakuwa tofauti na wale waliotangulia, naye atawaangusha wafalme watatu. 257:25 Isa 37:23; Dan 11:36; 2:21; 12:7-13; Ufu 16:6; Lk 21:8; Mdo 1:6-7; Ufu 11:2Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati.7:25 Wakati, nyakati mbili, na nusu wakati maana yake ni mwaka mmoja, miaka miwili, na nusu mwaka, yaani miaka mitatu na nusu.

267:26 Ufu 19:20“ ‘Lakini mahakama itakaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele. 277:27 2Sam 7:13; Lk 1:33; Za 22:27; 72:11; Isa 14:2; 1Kor 6:2; Mwa 14:18Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’

287:28 Isa 21:3; Dan 4:19; Lk 2:19; Za 13:2; Ay 4:15“Huu ndio mwisho wa jambo lile. Mimi Danieli nilitaabika sana katika mawazo yangu, nao uso wangu ukabadilika, lakini nililiweka jambo hilo moyoni mwangu.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

但以理书 7:1-28

但以理梦见四兽

1巴比伦伯沙撒元年,但以理在床上做了一个梦,脑中出现了异象,便把梦记录下来,讲述其中的大意。 2但以理说:“我在夜间的异象中看见天上有四股风吹来,搅动大海。 3接着,四只巨兽从海中上来,各有不同的形状。 4第一只兽像狮子,但有鹰的翅膀。我观看时,见它的翅膀被拔掉。它被扶起来,像人一样双脚站在地上,并被赋予人的头脑。 5第二只兽像熊,用两只后腿站立,牙齿间叼着三根肋骨,有声音对它说,‘起来,多吞吃肉吧!’

6“此后,我继续观看,见还有一只兽像豹,背上有四个如鸟翼般的翅膀。这兽有四个头,并被赋予权柄。 7此后,我在夜间的异象中看见第四只兽,恐怖可怕,极其强壮,长着大铁牙吞吃、咬碎猎物,用脚践踏所剩的。这兽与前三只兽不同,它有十个角。 8我观看这些角时,见其中又长出一个小角,先前的角中有三个被连根拔出,由它取而代之。这小角有人的眼睛和说狂言的口。

9“我看见宝座已设立,

上面坐着亘古长存者,

祂的衣服洁白如雪,

头发如纯净的羊毛。

祂的宝座是火焰,

宝座的轮子是烈火。

10从祂面前流出火河,

事奉祂的有千千,

侍立在祂面前的有万万。

祂坐下要审判,

案卷已经展开。

11“因为小角口出狂言,我便继续观看,一直到那兽被杀,身体被毁并被扔进火中。 12至于其余的兽,它们的权柄都被夺去,但获准再存活一段时间。

13“我在夜间的异象中看见一位像人子的驾着天上的云而来,到亘古长存者那里,被引到祂面前。 14祂得到权柄、荣耀和国度,各国、各邦、各语种的人都要事奉祂。祂的统治直到永远、没有穷尽,祂的国度永不灭亡。

解释异象

15“我但以理心灵不安,脑中出现的异象让我恐惧, 16便走近一位侍立一旁的,问他这些事的意思。他就向我解释说, 17‘这四只巨兽是指四个将要在世上兴起的王。 18但至高者的圣民必承受这国度,并永永远远拥有这国度。’

19“那时,我想知道关于第四兽的事,它与其余三兽不同,极其可怕,有铁牙铜爪,吞吃、咬碎猎物,用脚践踏所剩的。 20我也想知道有关它头上的十角及后来长出的小角的事。有三个角在这小角面前断落,这角有眼和说狂言的口,看起来比其他角更强大。 21我看见这小角与圣民争战,并占了上风。 22后来亘古长存的至高者来为祂的圣民申冤。圣民拥有国度的时候到了。

23“那位侍立一旁的说,‘第四只兽是指世上将兴起的第四个国,与其他各国不同,它将吞吃、践踏、咬碎天下。 24十角是指这国中将兴起十个王,后来又兴起一王,与先前的王不同,他将制服三个王。 25他必亵渎至高者,迫害至高者的圣民,试图改变节期和律法。圣民将被交在他手中三年半。 26然而,审判者将坐下来审判,夺去并永远废除他的权柄。 27那时,国度、权柄和天下万国的尊荣必赐给至高者的圣民。祂的国度直到永远,一切掌权者都要事奉祂,顺服祂。’

28“这就是我的梦。我但以理心中十分害怕,脸色苍白,但我没有把这事告诉别人。”