Elihu Atukuza Wema Wa Mungu
1Elihu akaendelea kusema:
2“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha
kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu.
336:3 Ay 4:17; 8:3Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali,
nami nitamhesabia haki Muumba wangu.
436:4 Ay 6:28; 13:6; 37:5, 16, 23; 32:17Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo;
mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.
536:5 Za 31:22; 69:33; Hes 23:19; Rum 11:29“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu;
ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.
636:6 Ay 8:22; 4:10Hawaachi waovu waendelee kuishi,
bali huwapa walioteswa haki yao.
736:7 Za 34:15; 113:8; Mt 6:18; Isa 22:23Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki;
huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme
na kuwatukuza milele.
836:8 2Sam 3:34; 2Fal 23:33Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo,
wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,
936:9 Ay 15:25huwaonyesha yale waliyoyatenda,
kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.
1036:10 Ay 33:16; 2Fal 17:13; Ay 5:17Huwafanya wao kusikia maonyo,
na huwaagiza kutubu uovu wao.
1136:11 Kut 28:1; Hag 1:12; Isa 1; 19Kama wakitii na kumtumikia,
wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio,
na miaka yao katika utoshelevu.
1236:12 Law 26:38; Ay 15:22; 4:21; Efe 4:18Lakini wasiposikiliza,
wataangamia kwa upanga,
nao watakufa pasipo maarifa.
1336:13 Ay 15:12; Rum 2:5; Ay 5:2; 4:17; Amo 4:11“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki;
hata anapowafunga, hawamwombi msaada.
1436:14 Kum 23:17Wanakufa wangali vijana,
miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.
1536:15 Ay 5:15; 2Kor 12:10; Ay 33:16; 34:33Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao,
na kuzungumza nao katika dhiki zao.
1636:16 Hos 2:14; Za 23:5; 78:19“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki,
ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi,
hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.
1736:17 Ay 20:29; 22:11Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu;
hukumu na haki vimekukamata.
1836:18 Kut 23:8; Amo 5:12; Ay 34:33Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri;
usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa.
1936:19 Za 49:6; Yer 9:23Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi
vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki?
2036:20 Ay 34:20-25Usiutamani usiku uje,
ili uwaburute watu mbali na nyumba zao.
2136:21 Ay 34:33; Za 66:18; Ebr 11:25Jihadhari usigeukie uovu,
ambao unaupenda zaidi kuliko mateso.
2236:22 Isa 40:13; Rum 11:34“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake.
Ni nani aliye mwalimu kama yeye?
2336:23 Ay 34:10, 13; Rum 11:33; Mwa 18:25; Kum 32:4Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake,
au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?
2436:24 1Nya 16:24; Za 35:27; 59:16; Ufu 15:3Kumbuka kuzitukuza kazi zake,
ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
2536:25 Rum 1:20Wanadamu wote wameiona;
watu wanaikazia macho kwa mbali.
2636:26 1Kor 13:12; Mwa 21:33; Ebr 1:12Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu,
kupita ufahamu wetu!
Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
2736:27 2Sam 1:21; Za 147:8“Yeye huvuta juu matone ya maji,
ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;
2836:28 Ay 22:11; Mt 5:45mawingu huangusha chini maji yake,
nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.
2936:29 Mit 8:28; Isa 40:22Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu,
jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.
3036:30 Kut 19:16; Yer 10:13; Hab 3:11; Isa 51:10; Za 18:12, 14; 97:4Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka,
naye huvifunika vilindi vya bahari.
3136:31 1Fal 17:1; Amo 4:7-8; Isa 30:23; Mdo 14:17Hivi ndivyo atawalavyo mataifa,
na kuwapa chakula kwa wingi.
3236:32 Ay 28:24; Za 18:14Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi,
na kuuagiza kulenga shabaha yake.
33Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja;
hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.36:33 Au: hutangaza kuja kwake.