131:1 Kum 5:18; Mt 5:18“Nimefanya agano na macho yangu
yasimtazame msichana kwa kumtamani.
231:2 Ay 16:19; 20:29Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu,
urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu?
331:3 Ay 21:30; 34:22; Rum 2:9Je, si uharibifu kwa watu waovu,
maangamizi kwa wale watendao mabaya?
431:4 2Nya 16:9; Mit 5:21; Yer 32:19; Dan 4:37Je, yeye hazioni njia zangu
na kuihesabu kila hatua yangu?
531:5 Ay 15:31; Mik 2:11“Kama nimeishi katika uongo
au mguu wangu umekimbilia udanganyifu,
631:6 Law 19:36; Ay 6:2Mungu na anipime katika mizani za uaminifu,
naye atajua kwamba sina hatia:
731:7 Ay 9:30; Hes 15:39; Eze 6:9; Mt 5:29; Mhu 11:9kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia,
kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu,
au kama mikono yangu imetiwa unajisi,
831:8 Law 26:16; Yn 4:37; Mik 6:15basi wengine na wale nilichokipanda,
nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe.
931:9 Kum 11:16; Yak 1:14“Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke,
au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu,
1031:10 Kum 28:30; Yer 8:16; Mit 14:31basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine,
nao wanaume wengine walale naye.
1131:11 Law 20:10; Yn 8:4-5Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu,
naam, dhambi ya kuhukumiwa.
1231:12 Ay 15:30; 26:6Ni moto uwakao kwa Uharibifu;31:12 Kwa Kiebrania ni Abadon (Ay 26:6; Mit 15:11).
ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.
1331:13 Kut 21:2-11; Law 25:39-46“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu,
walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,
1431:14 Ay 33:5; Hos 9:7; Za 10:13, 15; Isa 10:3; Yer 5:31nitafanya nini Mungu atakaponikabili?
Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?
1531:15 Ay 10:3; Efe 6:9Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu,
si ndiye aliwaumba?
Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote
ndani ya mama zetu?
1631:16 Law 25:17; Ay 20:19; Yak 1:27“Ikiwa nimewanyima maskini haja zao,
au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,
1731:17 Ay 6:27; 29:12kama nimekula chakula changu mwenyewe,
bila kuwashirikisha yatima;
1831:18 Isa 51:18lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya,
nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane:
1931:19 Ay 22:6; 24:4; Isa 58:7kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo,
au mtu mhitaji asiye na mavazi
2031:20 Ay 29:13; Amu 6:37ambaye wala moyo wake haukunibariki
kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu,
2131:21 Ay 22:7-9; Yak 1:27na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima,
nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani,
2231:22 Hes 15:30; Za 10:15basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu,
nao na uvunjike kutoka kiungio chake.
2331:23 Ay 10:3; 13:11; Mwa 20:11Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu,
nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo.
2431:24 Ay 22:25; Mk 10:24; Lk 12:15“Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu,
au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’
2531:25 Mwa 12:16; Isa 10:14kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu,
ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata,
2631:26 Hes 11:20; Kum 4:19; Eze 8:16kama nimelitazama jua katika kungʼaa kwake
au mwezi ukienda kwa fahari yake,
2731:27 Ay 24:15; Yak 1:14; Yer 8:2; 16:11hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri,
au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu,
2831:28 Mwa 38:24; Kum 17:2-7; Yos 24:23-27; Mit 30:9basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa,
kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana.
2931:29 Za 35:15; Mt 5:44; Mit 17:5; 24:17-18“Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu,
au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia,
30lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi
kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake;
31kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema,
‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’
3231:32 Amu 19:20; Mt 25:35; Ebr 13:2; 1Pet 4:9Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani,
kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri;
3331:33 Za 32:5; Mit 28:13; Mwa 3:8kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo,
kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu,
3431:34 Kut 23:2; Mit 29:25kwa sababu ya kuogopa umati wa watu,
na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa,
nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango:
35(“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia!
Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu:
Mwenyezi na anijibu;
mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi.
36Hakika ningeyavaa begani mwangu,
ningeyavaa kama taji.
3731:37 Ay 1:3; 21:28Ningempa hesabu ya kila hatua yangu,
ningemwendea kama mwana wa mfalme.)
3831:38 Mwa 4:10“Kama nchi yangu inalia dhidi yangu,
na mifereji yake yote imelowana kwa machozi,
3931:39 1Fal 21:19; Law 19:13; Yak 5:4kama nimekula mazao yake bila malipo,
au kuvunja mioyo ya wapangaji wake,
4031:40 Mwa 3:18; Mit 13:7basi miiba na iote badala ya ngano,
na magugu badala ya shayiri.”
Mwisho wa maneno ya Ayubu.