Hotuba Ya Saba Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Waovu Mara Nyingi Huenda Bila Kuadhibiwa
1Ndipo Ayubu akajibu:
221:2 Ay 13:17; 21:34“Yasikilizeni maneno yangu kwa makini;
hii na iwe faraja mnayonipa mimi.
321:3 Ay 6:14; 11:3; 16:10Nivumilieni ninapozungumza,
nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki.
421:4 Za 22:1-3; Ay 6:3, 11; 1Sam 1:16“Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu?
Kwa nini nisikose subira?
521:5 Amu 18:19; Ay 40:4Niangalieni mkastaajabu;
mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu.
621:6 Mwa 45:3; Ay 4:14Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa,
nao mwili wangu unatetemeka.
721:7 Mhu 7:15; Mal 3:15; Yer 12:1-3Kwa nini waovu wanaendelea kuishi,
wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu?
821:8 Za 17:14; Mal 3:15Huwaona watoto wao wakithibitika
wakiwa wamewazunguka,
wazao wao mbele za macho yao.
921:9 Ay 5:24; Za 73:5Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu;
fimbo ya Mungu haiko juu yao.
1021:10 Kut 23:26Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe;
ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba.
1121:11 Za 78:52; 107:41Huwatoa watoto wao nje kama kundi;
wadogo wao huchezacheza.
1221:12 1Nya 15:16; Mt 15:17Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi,
nao huifurahia sauti ya filimbi.
1321:13 Ay 24:19; Za 49:14; Isa 14:15; Ay 3:13Huitumia miaka yao katika mafanikio
nao hushuka kaburini kwa amani.
1421:14 Ay 4:17; Kum 32:15; Isa 30:11; 1Sam 11:15Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’
Hatuna haja ya kufahamu njia zako.
1521:15 Yer 9:6; Mal 3:14Mwenyezi ni nani hata tumtumikie?
Tutapata faida gani kumwomba?
1621:16 Ay 22:18; Za 1:1; 26:5; 36:1Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe,
hivyo najitenga mbali na shauri la waovu.
1721:17 Ay 18:5; 18:12; 20:22, 28“Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa?
Ni mara ngapi maafa huwajia,
yale yawapatayo ambayo Mungu
huwapangia katika hasira yake?
1821:18 Ay 13:15; Mwa 19:15; Ay 7:10; Mit 10:25; Mwa 7:23Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo,
kama makapi yachukuliwayo na dhoruba?
1921:19 Kut 20:5; Yn 9:2Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu
kwa ajili ya wanawe.’
Mungu na amlipe mtu mwenyewe,
ili apate kulijua!
2021:20 Ay 6:4; Isa 51:17; Yer 25:15; Ufu 14:10Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake;
yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi.
2121:21 Ay 14:22; 14:5; 14:21; Mhu 9:5-6Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma,
miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho?
2221:22 Za 94:12; 86:8; Rum 11:34“Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa,
iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote?
2321:23 Mwa 15:15; Ay 13:26; 3:13Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili,
akiwa salama na mwenye raha kamili,
2421:24 Mit 3:8mwili wake ukiwa umenawiri,
nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake.
2521:25 Ay 10:1Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi,
akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri.
2621:26 Mhu 9:2-3; Isa 14:11Hao wote hulala mavumbini,
nao mabuu huwafunika wote.
27“Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri,
mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya.
2821:28 Ay 1:3; 12:21; 29:25; 31:37; 8:22Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu,
mahema ambayo watu waovu walikaa?’
29Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri?
Je, hamkutafakari taarifa zao:
3021:30 Ay 31:3; Mit 16:4; Isa 5:30; Rum 5:2kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa,
kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu?
3121:31 Ay 34:11; Za 62:12; Mit 24:11-12; Isa 59:18Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake?
Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda?
3221:32 Isa 14:18Hupelekwa kaburini,
nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake.
3321:33 Ay 3:17-19; 17:16; 24:24Udongo ulio bondeni ni mtamu kwake;
watu wote watamfuata,
nao umati wa watu usiohesabika umemtangulia.
34“Hivyo ninyi mnawezaje kunifariji kwa upuzi wenu?
Hakuna kilichosalia cha majibu yenu isipokuwa uongo!”